Mpango wa kulifumua upya jiji la Dar na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva

Ahsante sana Mkuu, historia ya Serikali ya CCM kwenye miradi mikubwa ya Kitaifa siku zote hawaweki maslahi ya Taifa mbele. Ukiangalia ununuzi wa Rada, IPTL, Richmond/Dowans, ndege ya Rais, mikataba ya rasilimali za nchi, Escrow n.k. Hivyo hapa pia watakwapua mabilioni ya pesa na ndiyo sababu Magufuli alianza mkwara wa kutaka kumuondoa CAG ili aondoe kizingiti kikubwa na kumuweka CAG uchwara. Kuna uzi ulianzishwa humu na msaliti Mwanakijiji wa kumshambulia CAG na kumshinikiza ajiuzulu.

Na hii miradi ya kutumia pesa nyingi sana uhamiaji wa Dodoma, mkopo wa Trilioni 16 toka Exim bank, ununuzi wa ndege haijadiliwi Bungeni na Wabunge ndiyo ambao wanastahili kuidhinisha matumizi yote ya Bunge na si Rais wa nchi. Sababu nyingine ya kuwafungia Wabunge makini na kamati uchwara ya maadili Bungeni wakati huo huo mafisadi akina Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengineo ndani ya Bunge hilo hawajaguswa na hiyo kamati uchwara ya maadili.

Mkuu nakupongeza kwa kuona mbali katika michango yako humu nakupa salute.
 
Ahsante sana Mkuu, historia ya Serikali ya CCM kwenye miradi mikubwa ya Kitaifa siku zote hawaweki maslahi ya Taifa mbele. Ukiangalia ununuzi wa Rada, IPTL, Richmond/Dowans, ndege ya Rais, mikataba ya rasilimali za nchi, Escrow n.k. Hivyo hapa pia watakwapua mabilioni ya pesa na ndiyo sababu Magufuli alianza mkwara wa kutaka kumuondoa ili aondoe kizingiti kikubwa na kumuweka CAG uchwara. Kuna uzi ulianzishwa humu na msaliti Mwanakijiji wa kumshambulia CAG na kumshinikiza ajiuzulu.
Mkuu ume hit pale pale,watakaochukia kuhusu ngosha sisi hatujali kabisa,ukweli na usemwe tu,leo nchi ina mambo mengi yalio nyuma kupita dunia ya tatu,nchi zote zilizokuwa nyuma ya Tanzania leo zipo mbele yetu,na hii imetokana na viongozi kuingia madarakani ili kuiba tuuu,sababu kubwa ni uoga wa wananchi kuikemea serikali hata kama kuna kifo,lakini wapi hakuna shida kuisha Tanzania mpaka wananchi waamue kwamba sasa baasi inatosha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nashukuru now watz tuko makini, kwa hili wamechemsha. Kuna mipango midogo haijatekelezwa sembuse huu mradi mdogo. Wafiri nje ya box na zaidi wafikiri bila box
 
Ahsante sana Mkuu, historia ya Serikali ya CCM kwenye miradi mikubwa ya Kitaifa siku zote hawaweki maslahi ya Taifa mbele. Ukiangalia ununuzi wa Rada, IPTL, Richmond/Dowans, ndege ya Rais, mikataba ya rasilimali za nchi, Escrow n.k. Hivyo hapa pia watakwapua mabilioni ya pesa na ndiyo sababu Magufuli alianza mkwara wa kutaka kumuondoa CAG ili aondoe kizingiti kikubwa na kumuweka CAG uchwara. Kuna uzi ulianzishwa humu na msaliti Mwanakijiji wa kumshambulia CAG na kumshinikiza ajiuzulu.

Na hii miradi ya kutumia pesa nyingi sana uhamiaji wa Dodoma, mkopo wa Trilioni 16 toka Exim bank, ununuzi wa ndege haijadiliwi Bungeni na Wabunge ndiyo ambao wanastahili kuidhinisha matumizi yote ya Bunge na si Rais wa nchi. Sababu nyingine ya kuwafungia Wabunge makini na kamati uchwara ya maadili Bungeni wakati huo huo mafisadi akina Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengineo ndani ya Bunge hilo hawajaguswa na hiyo kamati uchwara ya maadili.
mkuu umetisha sn! hata wao waliimba kw CCM NI ILE ILE so hawawezi kubadilika watz tumeshaingia choo cha kike tena kwa propaganda za muda mfupi tukamuona mtendaji kazi oooh jembe ila nothing else wote ni wale wale

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Wakati Serikali ikiwa katika mchakato wa kuhamia rasmi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, imeweka wazi kwamba mpango wa kulifumua upya jiji la Dar es salaam na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika ujenzi jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema mchakato wa kupanga mpango mpya wa mji 'City Master Plan' wa Dar es salaam tayari umeanza.

Alisema mpango mpya wa Mji wa Dar es salaam unatarajiwa kupatikana kabla ya Desemba mwaka huu ambapo kampuni kutoka Italia kwa kushirikiana na watanzania wanaifanyia kazi.

"Pamoja na kuhamia Dodoma ni lazima tuifumue Dar es salaam na kuifanya kuwa kitovu cha biashara kwa kuwa majengo ya kisasa yatakakuza uchumi wetu.

"Tunatarajia kutumia Dola milioni 300 kwa ajili ya kupiga picha angani kwa ndege ili kuipata Dar es salaam vizuri na kutengeneza mpango mji utakaokuwa wa kisasa "alisema Lukuvi

Pia Waziri Lukuvi aliwahamasisha wadau hao kujiandaa kuwekeza Dar es salaam na Dodoma kwa kuwa Serikali itakapohama jijini majengo yote ya Serikali yatahitaji uwekezaji

" Hii ni fursa ambayo mnatakiwa kuiangalia kwa karibu kwani kwa upande wa Dodoma kutahitajika huduma nyingi ikiwamo ya majengo ambayo yanakuwa ya makazi, ofisi na huduma nyingine za kiuchumi.

"Na wakati huo huo Serikali itakapohamia Dodoma, jijini hili litatakiwa kuwa na mwonekano wa kisiasa ili liwe na mvuto wa kibiashara na kukuza uchumi wetu "alisema Lukuvi

Pamoja na kuwahamasisha wadau hao ambao wengi ni wamiliki wa makampuni ya ujenzi, Waziri Lukuvi aliwataka kuhakikisha wanaotumia teknolojia za kisasa na kuwa na majengo yenye ubora na imara.

Chanzo :Mtanzania


Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Wilayani Kahama una thamani ya dola milioni 300 , sasa kwa nini kama tunazo hizo tusiununue au kuwekeza kwenye Mgodi mwingine au hata kujenga copper smelter au mtambo wa kuyeyushia chuma hapa kwetu ili kuongeza thamani ya rasilimali zetu? Hiyo Dar hamuwezi kuipanga bila kuvunja nyumba zoezi ambalo limeshindikana kwa maana chadema wanashirikiana na wananchi walipovunja Sheria za nchi kugomea!
 
$ 300 Mil...? Kwa photos za angani that is not ACCEPTABLE...!! Haijawahi tokea duniani... picha za angani si ghali hivyo... kama Waziri kasema hiyo figure ni hatari sasa...!!! Nadhani $ 30 mil...!! Miji yote mikubwa duniani gharama za kupiga picha angani ni cheap sio hiyo gharama...!!

$ 30 Mil nadhani, ambayo still ni kubwa sana sana tu bado...!!
Upo right Jay 1.. waziri alisema ni $3mil. Huyuu jamaa ameongezaa "00" zake...
 
Hammjui Lukuvi. Wakati Waziriwa Ujenzi Jiohn Magufuli amekataza waliojenga ndaniya hifadhi ya barabara Kilwa Road Lukuvi akatoa pesa za Mkoa akaenda kuwalipa marafiki zake Kongowe. Akapanda ngazi kutoka ukuu wa mkoa hadi ubunge na uwaziri. Fadhiriķeni hizo mtakutana nazo katika hizi bil. 600/ zinazosemwa.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Dola mil.300 itatumika kupanga jiji ikiwemo kupima viwanja vya jiji zima,kupiga picha na vitu vinavyofanana na hayo kwa uelewa wangu
 
Sijajua upangaji huu mji inamaana watatubomolea sie walala hoi
Mm nadhani hizo $300m..ni kwa ajili ya kuwalipa watu watakaobomolewa..haiwezekani hizo pesa zote ziteketee...kwa kupiga picha za juu...that's stupid!nchi hii itakuja kuwa na watu wenye weledi mzuri lini ..ili waweze kutuandikia kitu kinachoeleweka?
 
tunapoteza faza nyingi kwa kukalia dar es salaam na hii inapelekea wote tanzania kulundikana dar es salaam hata kisabisha maendeleo hafifu kwa mikoa mingine na fursa kukosa katika mikoa mengine.jalibuni kujenga mikoa mingine ili watu wakaone fursa kwa mikoa mingine kama walivo fanya marekani.mtu ana aja ya kuishi sehemu fulani wakati kila jambo lipo sehemu yake
 
Watanzania kwa sasa hatuhitaj kutumia pesa nyingi kwaajil ya master plan....... Tunataka viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa watu wengi
 
Back
Top Bottom