Mpango wa kulifumua upya jiji la Dar na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva

Swali la msingi hayo majengo ya serikali unamuuzia nani wakati hao wenye majengo wanatafuta wakumuuzia kwani biashara zimebuma gafla mjini..Mfano zile twin towers za BOT unamuuzia nani...Hii awamu Muumba atusaidie lakini naona mkwamo mbaya sana huko mbeleni
 
Kama kweli hii hesabu hi ni EPA NA ESCROW ya awamu mpya...na ubaya wa sasa Tulya atazima kila jaribio la kuhoji
 
Swali la msingi hayo majengo ya serikali unamuuzia nani wakati hao wenye majengo wanatafuta wakumuuzia kwani biashara zimebuma gafla mjini..Mfano zile twin towers za BOT unamuuzia nani...Hii awamu Muumba atusaidie lakini naona mkwamo mbaya sana huko mbeleni
Wala usihangaike hii mi mikwara tu. Hakuna vitendo ila kuuza wanaweza kuuza hawa jamaa nchi hii ni shamba la bibi...na 2020 hela ya kampeni lazima iingie hivo zinaweza kuuzwa mbili tatu kwa bei chee
 
$ 300 Mil...? Kwa photos za angani that is not ACCEPTABLE...!! Haijawahi tokea duniani... picha za angani si ghali hivyo... kama Waziri kasema hiyo figure ni hatari sasa...!!! Nadhani $ 30 mil...!! Miji yote mikubwa duniani gharama za kupiga picha angani ni cheap sio hiyo gharama...!!

$ 30 Mil nadhani, ambayo still ni kubwa sana sana tu bado...!!
 
Dola milioni 300??!!!!!

Jamani jamani.......

Pampja na umuhimu wa kuipanga upya dsm....

Hizo fedha zingesaidia kuboresha hospitali za wilaya...muhimbili...ocean road...vifaa tiba.....au hata madarasa na maabara

Anyway

Nawatakia mboresho mwema..ikiwezekana mje huku rufiji jamani
 
Mbona munaacha kwa makusudi"na kutengeneza mpango mji utakaokuwa wa kisasa?
Inamaana ni kupiga picha na kutengeneza master plan,kudizani ni kazi ya ubunifu ambayo inachukua muda mrefu na changamoto nyingi,ni kazi ya kutengeneza na kufuta mpaka ikubalike.
 
Mizuka haijaisha tu kwa mawazir, kila siku wanaaamka na jipya leo naona wamekuja na dili la mpango wakufumua dar na watapiga $300mln kwaajir yakupiga picha tu.
 
Nyumba zilizokwishajengwa zitasogezwa sogezwa-sogezwa tu, hii iende pale na ile isogee kule basi...Kama gharama za picture tu kiasi hicho je hizo za ujenzi zitakuwaje. Isije kuishia kama simulizi za akina Sakabona na ndoto zake.
Mpaka sasa hivi Kigamboni is a dead project
 
"Rolu modo wetu ni rwanda" Madhara yake ndio haya!!!

Mmeishindwa dodoma kwa miaka 30 mahali ambapo hapakuwa na ufumuaji, leo mnavamia kutaka kuotesha ghorofa kwenye mkondo wa nungwi!!!

Mungu ni mvumilivu sana.
 
Hii habari imeandikwa na mtu ambaye bado sana kupanga fikra zake. Anaandika kuhusu "mchakato wa kupanga mpango....". Anaelezea "kufumua upya jiji la Dar es Salaam". Kwani lilishafumuliwa tena?

Dar tayari ni kitovu cha biashara. Kwa hiyo "mchakato" wa kutumia dola milioni 300 ili kulifanya jiji la Dar liwe kitovu cha biashara unaweza kuwa mchakato wa kutuibia.

Taifa limegubikwa na vihiyo kila kona. Waandishi wa habari wawe watu wenye umakini.
we utakuwa una chuki binafsi na mleta mada
 
$300 MILION....? Hii mi deal...
Uki google na fast internet unaiweka Dar kwenye kiganja.
Hii haiko sawa


Wanaweza kuwadanganya watanzania kadhaa kwa muda wote na wanaweza kuwadanganya watanzania wote kwa muda kadhaa lakini kamwe hawawezi kuwadanganya watanzania wote kwa muda wote
 
Wanaweza kuwadanganya watanzania kadhaa kwa muda wote na wanaweza kuwadanganya watanzania wote kwa muda kadhaa lakini kamwe hawawezi kuwadanganya watanzania wote kwa muda wote
Ha ha ha maneno kuntu kabisa
 
Huwajui kumbe? Wakishasema hivyo Ndio basi wamemaliza, utaona hiyo Dec kama kuna jipya, hapo Ndio wameshamaliza kazi mbona
Kweli mkuu. Nikifikiria zile treni za haraka ambazo walidai reli itatandazwa wiki 3 tu kutoka city center hadi Airport huwa nacheka sana na kuwa sina hamu nao tena.
 
Back
Top Bottom