Mpango wa kulifumua upya jiji la Dar na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Wakati Serikali ikiwa katika mchakato wa kuhamia rasmi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, imeweka wazi kwamba mpango wa kulifumua upya jiji la Dar es salaam na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika ujenzi jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema mchakato wa kupanga mpango mpya wa mji 'City Master Plan' wa Dar es salaam tayari umeanza.

Alisema mpango mpya wa Mji wa Dar es salaam unatarajiwa kupatikana kabla ya Desemba mwaka huu ambapo kampuni kutoka Italia kwa kushirikiana na watanzania wanaifanyia kazi.

"Pamoja na kuhamia Dodoma ni lazima tuifumue Dar es salaam na kuifanya kuwa kitovu cha biashara kwa kuwa majengo ya kisasa yatakakuza uchumi wetu.

"Tunatarajia kutumia Dola milioni 300 kwa ajili ya kupiga picha angani kwa ndege ili kuipata Dar es salaam vizuri na kutengeneza mpango mji utakaokuwa wa kisasa "alisema Lukuvi

Pia Waziri Lukuvi aliwahamasisha wadau hao kujiandaa kuwekeza Dar es salaam na Dodoma kwa kuwa Serikali itakapohama jijini majengo yote ya Serikali yatahitaji uwekezaji

" Hii ni fursa ambayo mnatakiwa kuiangalia kwa karibu kwani kwa upande wa Dodoma kutahitajika huduma nyingi ikiwamo ya majengo ambayo yanakuwa ya makazi, ofisi na huduma nyingine za kiuchumi.

"Na wakati huo huo Serikali itakapohamia Dodoma, jijini hili litatakiwa kuwa na mwonekano wa kisiasa ili liwe na mvuto wa kibiashara na kukuza uchumi wetu "alisema Lukuvi

Pamoja na kuwahamasisha wadau hao ambao wengi ni wamiliki wa makampuni ya ujenzi, Waziri Lukuvi aliwataka kuhakikisha wanaotumia teknolojia za kisasa na kuwa na majengo yenye ubora na imara.

Chanzo :Mtanzania
 
Watatumia dola million 300 kupiga picha ya angani?

Hata mimi nimejiuliza. Kumbe hii kitu ina gharama kiasi hiki au mwandishi amekosea???
 
Hii habari imeandikwa na mtu ambaye bado sana kupanga fikra zake. Anaandika kuhusu "mchakato wa kupanga mpango....". Anaelezea "kufumua upya jiji la Dar es Salaam". Kwani lilishafumuliwa tena?

Dar tayari ni kitovu cha biashara. Kwa hiyo "mchakato" wa kutumia dola milioni 300 ili kulifanya jiji la Dar liwe kitovu cha biashara unaweza kuwa mchakato wa kutuibia.

Taifa limegubikwa na vihiyo kila kona. Waandishi wa habari wawe watu wenye umakini.
 
1471127230543.jpg
Tuko katika mchakato, tuko katika mpango.. Kwanini msiplan kimya kimya halafu mkaja kutangaza tayari mradi umekamilika..!?
 
Wakati Serikali ikiwa katika mchakato wa kuhamia rasmi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, imeweka wazi kwamba mpango wa kulifumua upya jiji la Dar es salaam na kulifanya kuwa kitovu cha biashara sasa umeiva.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika ujenzi jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema mchakato wa kupanga mpango mpya wa mji 'City Master Plan' wa Dar es salaam tayari umeanza.

Alisema mpango mpya wa Mji wa Dar es salaam unatarajiwa kupatikana kabla ya Desemba mwaka huu ambapo kampuni kutoka Italia kwa kushirikiana na watanzania wanaifanyia kazi.

"Pamoja na kuhamia Dodoma ni lazima tuifumue Dar es salaam na kuifanya kuwa kitovu cha biashara kwa kuwa majengo ya kisasa yatakakuza uchumi wetu.

"Tunatarajia kutumia Dola milioni 300 kwa ajili ya kupiga picha angani kwa ndege ili kuipata Dar es salaam vizuri na kutengeneza mpango mji utakaokuwa wa kisasa "alisema Lukuvi

Pia Waziri Lukuvi aliwahamasisha wadau hao kujiandaa kuwekeza Dar es salaam na Dodoma kwa kuwa Serikali itakapohama jijini majengo yote ya Serikali yatahitaji uwekezaji

" Hii ni fursa ambayo mnatakiwa kuiangalia kwa karibu kwani kwa upande wa Dodoma kutahitajika huduma nyingi ikiwamo ya majengo ambayo yanakuwa ya makazi, ofisi na huduma nyingine za kiuchumi.

"Na wakati huo huo Serikali itakapohamia Dodoma, jijini hili litatakiwa kuwa na mwonekano wa kisiasa ili liwe na mvuto wa kibiashara na kukuza uchumi wetu "alisema Lukuvi

Pamoja na kuwahamasisha wadau hao ambao wengi ni wamiliki wa makampuni ya ujenzi, Waziri Lukuvi aliwataka kuhakikisha wanaotumia teknolojia za kisasa na kuwa na majengo yenye ubora na imara.

Chanzo :Mtanzania

Samahani. Aliyeelewa naomba anieleweshe. Pengine sijasoma vizuri au mwandishi kakosea.

Ni dola za wapi millioni miatatu za kupigia picha?
 
$300 MILION....? Hii mi deal...
Uki google na fast internet unaiweka Dar kwenye kiganja.
Hii haiko sawa
 
Hivi nchi yetu hii inatoaga muda wa wananchi haswa waishio wanapozungumzia? Sababu ni muhimu wananchi kuangalia mipango hiyo kabla ya kupitishwa, ili waweze kuweka maoni yao mbalimbali wanapoamua.
 
Naiona Tanzania ya viwanda ikiota mbawa hivi hivi..haya mambo hayakuwepo kwenye vipaombele
 
Back
Top Bottom