Mpango na Bajeti ya Mwaka 2021/2022 kufumuliwa na Awamu ya Sita

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Inadaiwa mojawapo ya jambo kubwa lililokuwa linapita bila hata kujadiliwa katika bajeti hii na hata Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walishajulishwa na wakanyamaza kimya ni kutokuwa na nyongeza ya mishahara. Vyama vya wafanyakazi kwa kupitia TUCTA walishakuwa kimya kama wamenyeshewa mvua kwa kuacha tu awamu ya tano ifanye ifanyavyo na mpaka ingeamua yenyewe ni lini ingepandisha mishahara.

Mabaraza ya Wafanyakazi ambayo huhusisha Waajiri, wafanyazi na vyama vyao yalishakaa kwa nchi nzima, wizara hadi Taasisi na kupitisha mpango kazi na bajeti zao ambazo hazikuwa hata na nyongeza za mishahara hata kiduchu tu na kwenye vikao woga ulikuwa ni mwingi mno mno kuhoji. Wapangaji Bajeti wanadai walipewa ukomo wa bajeti hizo toka Wizara ya Fedha - kwa Doto James, yaani yule kaka yake na Heri James wa UVCCM, na hakuna mtu aliyekuwa akidiriki kuhoji kuhusu nyongeza. Hata Mei Mosi ilitarajiwa kuja ikiwa imepooza sana sana. Pengine awamu hii inaweza ikaichangamsha!

Sasa je kwa ujio wa awamu hii ya sita - tutaendelea na dude hilo hilo la awamu ya tano? Waziri wa Utumishi Mohamed Mchengerewa umeongea kwa maana kubwa sana baada ya kuapishwa - je huoni kwa kutumia taaluma yako ya sheria na kwa nafasi yako sasa una haja ya kuifanya serikali ifikiri na hilo isiwe mambo ya kupandishana vyeo tu ndiyo yanastahili nyongeza. Tafadhali tamka kitu angalau hiyo bajeti ipanguliwe na nyongeza hata 0.5% ikiwekwa itasaidia sana hawa wafanyakazi angalau waweze hata kukopa benki. Inasemekana tayari Mh. Dkt. Mwigulu tayari ameshadokeza kufanyia mabadiliko baadhi ya mambo katika Mpango Kazi na Bajeti 2021/2022 na hili basi liwe mojawapo!
 
Bajeti isiwasahau vijana wanaosota mtaani bila ajira za kueleweka huku wana taaluma zao, mbaya zaidi huduma katika sekota mbalimbali zinadorora kwa kukosa wataalam.
Nina jamaa yangu ni dr anajitolea katika ki dispensary flani kwa ujira wa 150 k per month, can you imagine?
Halafu awamu ilopita ilikuwa bize kuwaasa vijana wajiajiri ilihali wao wanangangania kwenye nafasi zao na wakitumbuliwa wanalia na kugalagala ref. Rc wa Moro.
Mama aziangalie kada zote mf ualimu, udakitari, uuguzi etc.
 
Hilo la ajira pia ni muhimu sana!
 
Inadaiwa mojawapo ya jambo kubwa lililokuwa linapita bila hata kujadiliwa katika bajeti hii na hata Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walishajulishwa na wakanyamaza kimya ni kutokuwa na nyongeza ya mishahara. Vyama vya wafanyakazi kwa kupitia TUCTA walishakuwa kimya kama wamenyeshewa mvua kwa kuacha tu awamu ya tano ifanye ifanyavyo na mpaka ingeamua yenyewe ni lini ingepandisha mishahara.

Mabaraza ya Wafanyakazi ambayo huhusisha Waajiri, wafanyazi na vyama vyao yalishakaa kwa nchi nzima, wizara hadi Taasisi na kupitisha mpango kazi na bajeti zao ambazo hazikuwa hata na nyongeza za mishahara hata kiduchu tu na kwenye vikao woga ulikuwa ni mwingi mno mno kuhoji. Wapangaji Bajeti wanadai walipewa ukomo wa bajeti hizo toka Wizara ya Fedha - kwa Doto James, yaani yule kaka yake na Heri James wa UVCCM, na hakuna mtu aliyekuwa akidiriki kuhoji kuhusu nyongeza. Hata Mei Mosi ilitarajiwa kuja ikiwa imepooza sana sana. Pengine awamu hii inaweza ikaichangamsha!

Sasa je kwa ujio wa awamu hii ya sita - tutaendelea na dude hilo hilo la awamu ya tano? Waziri wa Utumishi Mohamed Mchengerewa umeongea kwa maana kubwa sana baada ya kuapishwa - je huoni kwa kutumia taaluma yako ya sheria na kwa nafasi yako sasa una haja ya kuifanya serikali ifikiri na hilo isiwe mambo ya kupandishana vyeo tu ndiyo yanastahili nyongeza. Tafadhali tamka kitu angalau hiyo bajeti ipanguliwe na nyongeza hata 0.5% ikiwekwa itasaidia sana hawa wafanyakazi angalau waweze hata kukopa benki. Inasemekana tayari Mh. Dkt. Mwigulu tayari ameshadokeza kufanyia mabadiliko baadhi ya mambo katika Mpango Kazi na Bajeti 2021/2022 na hili basi liwe mojawapo!
Acha zako, huna lolote, wewe unayetabiri Bashiru kuwa PM wakati katiba haiko upande wake ndo uje kutudanganya kirahisi? Endelea na tetesi zako.
 
Back
Top Bottom