Mwaka wa Fedha 2022/2023 Serikali Ilishindwa Kukusanya Shilingi 1.76 Trilion Ili kutimiza Malengo ya Bajeti ya Kukusanya Shilingi 28Trilion

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu akiahirisha Bunge ni kwamba Hadi kufikia June 30 2023, Serikali ilifanikiwa kukusanya sh.26.24T sawa na 93.7% ya malengo ya Kukusanya 28Trilioni kama Malengo ya Bajeti Kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

Kwa hesabu hizo kiasi Cha sh.Trilion 1.76 hazikuweza kupatikana licha ya kuwa committed kwenye miradi mbalimbali kwenye Bajeti ya Nchi.Hizo ni pesa nyingi sana kiasi kwamba miradi Mingi itakuwa imeathirika Kwa kutopewa pesa.

Swali: Hivi Kwa nini Serikali haijawahi Kusanya mapato sawa na malengo yaani 100% au zaidi? Kila mwaka tunakusanya pesa kidogo Sana.

Mwaka wa Fedha ukioisha ndio mwaka ambao Serikali imefanya vibaya sana kwenye utekelezwaji wa Bajeti yake ambapo imetekeleza Kwa Asilimia 90% tuu wakati mwaka wa 2021/2022 ilitekeleza Kwa Asilimia zaidi ya 95%.

Mwisho kama uwekezaji unamiminika Kwa nini hatufikii malengo ya makusanyo na kutekeleza Bajeti kama tulivyopanga? Tujifunze kufanya tathmini.

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1700444262658142301?t=YSuJyCdek19acDAk9Hun1w&s=19
 
Back
Top Bottom