Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,332
- 10,913
Habari wakuu.
Maisha yanahitaji akili sana na maarifa hasa kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha yetu moja kwa moja. Mambo kama ya fedha, mapenzi, na utawala ni mambo yanayogusa maisha yetu moja kwa moja.
Upo msemo usemao ngoma ikilia sana ujue kupasuka kuko karibu. Msemo huu ndio unabeba uhalisia wa maisha kwa kiasi kikubwa. Na ndio unaonifanya niandike hivi leo.
Nina mpenzi wangu tunapenda sana, tena sana. Huu ukiwa mwaka wa nne tokea tuwe kwenye mapenzi. Mahusiano yetu yamepitia hatua mbali mbali ambazo zimeyafanya yawe imara yenye nguvu. Upendo wetu umewashangaza wengi hasa wale walidhani kuwa tutaachana mapema tuu.
Kutokana na mapenzi kuongezeka zaidi na zaidi jambo hili limenipa tafakuri nyingi ukizingatia mimi ni Joka ambaye ni mwerevu toka mwanadamu akiwa uchi. Ongezeko la mahaba kutoka kwa mke wangu siwezi kulichukulia kama jambo jema hata kidogo kwani upo msemo usemao ikivuma sana jua kupasuka kuko karibu. Wengi hawatanielewa lakini wenye akili za kijoka wataelewa nazungumzia nini.
Nimeandaa mpango mpya ambao uta-replace mpango wa zamani. Nimeanza taratibu za kujihami na matokeo ya mvumo huu wa mapenzi. Nimemuandaa msichana mmoja ambaye tayari taratibu zote za kiitifaki yamekamilika. Ili ngoma ikipasuka basi mimi kama mwamba ngoma nisikose pakuvuta.
Kila kitu kina Rise and fall. Hakuna kilichodondoka bila kupanda. Ukiona kitu kinapanga sana ujue kilele kipo karibu na matokeo yake kitadondoka kwa kasi ya kustaajabisha. Baadhi hawatanielewa.
Hata ni biashara ukiona imekuwa sana kupita kiasi jua anguko lipo karibu unashauriwa uanzishe biashara nyingene itakayo replace.
Nimetafuta kitoto kipya kizuri kwa ajili ya kujihami na anguko ambalo mimi kama joka naliona. Siwezi kupumbazwa na mapenzi moto moto ya kiwango hiki nikajisahau kuwa ngoma ikilia sana ujue itapasuka muda si muda. Na mapenzi yakifikia hatua hii ukiachwa unaweza ukajiua kama hukujipanga. Nami nimejipanga na wala sitatetereka hata ikitokea Great depression.
Wengi hudhani kuwa Maisha yanapokuwa mazuri na kustawi sana basi hujisahau na kudhani hayatadondoka. Na hapo ndipo magonjwa kama stroke na ukichaa huwakumba.
Mpango mpya nimeuseti kukabiliana na furaha hii ambayo inalengo la kunihadaa. Samahani sana Mpenzi wangu ila ndio akili za Joka Jeusi zilivyo.
Joka Jeusi
Ni Mstaafu wa Masuala ya Mapenzi