Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,512
- 40,197
Wana JF, hii taarifa inastua lakini ndivyo ilivyopangwa itokee na itatokea tu!
Nimekuwa katika kufuatilia kuunganishiwa umeme mtaani kwetu kutoka TANESCO. Nimefanya ufuatiliaji wa muda mrefu hadi kujenga urafiki na baadhi ya watu ndani ya shirika hili. Sasa nina uhakika wa kupata huduma hii katika miezi michache ijayo.
Nimepata taarifa nyingi za kusikitisha kuhusu shirika hili na moja imenistua sana. Kuna mpango kamambe wa viongozi wetu wa juu nchini kulihujumu shirika kwa kutumia mbinu chafu.
Kwanza; kwa kutumia vibaraka wao waliowachomeka shirikani na wizarani watahakikisha TANESCO inafanya kazi chini ya viwango ili kujenga taswira mbaya mbele ya jamii.
Pili watapendekeza na kuhamasisha kubadilisha mfumo wa shirika kwa kutolibinafsisha bali kuligawanya kiutendaji kwa kutoa kandarasi kwa makampuni binafsi kuchukua vitengo vya shirika. Namna ilivyopangwa ni kuligawanya shirika katika vyanzo vikuu vifuatavyo,
Tatu, Utekelezaji wake umeshaanza kwa kuhakikisha kwamba shirika halifikii viwango vinavyokidhi uwezo wa kusambaza umeme ili kuingiza long term deal ya kubinafsisha huduma za shirika kupitia vitengo vyote muhimu. Haya yote yanafanyika kwa uzoefu walioupata kupitia ubinafsishaji wa shirika la Reli (TRL) na mashirika mengine kama vile TTCL/ Celtel, Air Tanzania na kadhalika.
Tayari msigano wa kiutendaji baina ya TANESCO na wapiga deal hao umeshaanza chinichini ambapo lolote linaweza kulipuka muda wowote sasa. Inawezekana kabisa kwamba kuendelea kutumia mitambo ya dharura ya kuzalisha umeme kwa kipindi kirefu kutaharakisha dili hili la wakubwa.
Habari ndiyo hiyo. #JustSaying

- kuhakikisha TANESCO wananunua umeme mwingi na kuuingiza kwenye gridi ya Taifa kutoka kwenye makampuni yao,
- kubinafsisha huduma ya ugavi wa umeme kwa kampuni binafsi watakayoyapendekeza (kama ilivyokuwa NET SOLUTIONS)
- kubinafsisha huduma ya wateja na uuzaji wa unit za umeme kwa kampuni watakayoipendekeza
- kubinafshisha huduma ya ukarabati kwa kampuni watakayoipendekeza.
- Kubinafsisha ugavi wa vipuri vya umeme wa msongo mkubwa (wauziwe TANESCO) kwa kampuni yao.
- Huduma ya dharura (Emergency) kubinafsishwa pia