Mpango mchafu dhidi ya TANESCO

Mpango mchafu dhidi ya TANESCO

TANESCO hawaeleweki na wizara yote ya nishati hivi sasa MVUA zaina nyesha maeneo mengi nchi nzima lakini mgao wa umeme kama kawa,wasiwasi ni kwamba hata GAS ya Mtwara ikiunganishwa kwenye GRID hiyo ya Richmond bado hujuma za ki Richmond zitaendelea tu, sasa tutaambiwa mitambo michakavu,gas inavuja njiani,bomba limepasuka,na kadha wa kadha, tusubiri hii ndio Tanza-nia , ni maajabu ya dunia haya hakuna nchi lelemama kama hii!
 
Sishangai kwa maana,
Ofisi za umma zimegeuzwa maduka ambamo bidhaa zinazouzwa ni dhamana ambayo viongozi wamepewa na wananchi.

Kwakweli nashangaa sana watu wanaipenda CCM.

Alafu wale wanaccm humu jamvini kwenye issue kama hizi hawachangii kabisa, wao wanawaza kuwa hizi ni propaganda za cdm.

Ritz, unasemaje juu ya huu uzi?
 
kwa kweli Tanzania kimekuwa kichaka cha wezi, hv inakuwaje wizara inafanya deal za kijasusi huku usalama wa taifa wapo? Raic kikwete anapokea ripot zip za utekelezaji km watu hawa wanataka kuhujumu shrika la umeme wakati wakijua kuwa ndo kitengo muhimu ktk uchumi wa taifa.? Pumbavu@
 
Watanzania tunapaswa sasa kuirejesha nchi kwenye mstari.
Huku tulipofika sasa ni wazi nchi inaendeshwa kama kampuni binafsi.

Sheria zilizopo zinatumika against na raia, pia wakibanwa sana na sheria hao wajanja wanatunga sheria kuhalalisha upuuzi wao.

Ni budi sasa tutafakuri namna ya kuirejesha nchi kwenye misingi tuliyokuwa nayo hapo awali
 
Mkuu mbona nilikuwa naona Ulaya mambo yanayo husu umeme yanagawanywa katika makampuni matatu tanzu: Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji zote hizo zinafanya kazi independently kwa ufanisi wa hali ya juu, hata kazi nyingine zinakuwa outsourced; kwani Taifa letu ligihiga kutoka kwa wenzetu waliofanikiwa kuna ubaya GANI?

Nakubali kuna mambo mengine yanayo fanyika ndani ya Taifa letu ambayo hayapendezi, lakini haipendezi vile vile kuona kila kitu kinacho pendekezwa na Serikali yetu kina walakini hata kama kina manufaa kwa TAIFA i.e sio kila pendekezo la Serikali liko embedded kwenye UCHAFU.
 
Tanzania zaidi ya unavyo ifahamu...

Wana JF, hii taarifa inastua lakini ndivyo ilivyopangwa itokee na itatokea tu!

Nimekuwa katika kufuatilia kuunganishiwa umeme mtaani kwetu kutoka TANESCO. Nimefanya ufuatiliaji wa muda mrefu hadi kujenga urafiki na baadhi ya watu ndani ya shirika hili. Sasa nina uhakika wa kupata huduma hii katika miezi michache ijayo.

Nimepata taarifa nyingi za kusikitisha kuhusu shirika hili na moja imenistua sana. Kuna mpango kamambe wa viongozi wetu wa juu nchini kulihujumu shirika kwa kutumia mbinu chafu.

Kwanza; kwa kutumia vibaraka wao waliowachomeka shirikani na wizarani watahakikisha TANESCO inafanya kazi chini ya viwango ili kujenga taswira mbaya mbele ya jamii.

Pili watapendekeza na kuhamasisha kubadilisha mfumo wa shirika kwa kutolibinafsisha bali kuligawanya kiutendaji kwa kutoa kandarasi kwa makampuni binafsi kuchukua vitengo vya shirika. Namna ilivyopangwa ni kuligawanya shirika katika vyanzo vikuu vifuatavyo,
  1. kuhakikisha TANESCO wananunua umeme mwingi na kuuingiza kwenye gridi ya Taifa kutoka kwenye makampuni yao,
  2. kubinafsisha huduma ya ugavi wa umeme kwa kampuni binafsi watakayoyapendekeza (kama ilivyokuwa NET SOLUTIONS)
  3. kubinafsisha huduma ya wateja na uuzaji wa unit za umeme kwa kampuni watakayoipendekeza
  4. kubinafshisha huduma ya ukarabati kwa kampuni watakayoipendekeza.
  5. Kubinafsisha ugavi wa vipuri vya umeme wa msongo mkubwa (wauziwe TANESCO) kwa kampuni yao.
  6. Huduma ya dharura (Emergency) kubinafsishwa pia

Tatu, Utekelezaji wake umeshaanza kwa kuhakikisha kwamba shirika halifikii viwango vinavyokidhi uwezo wa kusambaza umeme ili kuingiza long term deal ya kubinafsisha huduma za shirika kupitia vitengo vyote muhimu. Haya yote yanafanyika kwa uzoefu walioupata kupitia ubinafsishaji wa shirika la Reli (TRL) na mashirika mengine kama vile TTCL/ Celtel, Air Tanzania na kadhalika.

Tayari msigano wa kiutendaji baina ya TANESCO na wapiga deal hao umeshaanza chinichini ambapo lolote linaweza kulipuka muda wowote sasa. Inawezekana kabisa kwamba kuendelea kutumia mitambo ya dharura ya kuzalisha umeme kwa kipindi kirefu kutaharakisha dili hili la wakubwa.

Habari ndiyo hiyo. #JustSaying
 
Matatizo ya Tanesco (umeme) ni dili la watawala wetu wakishirikiana na maswahiba wao wafanyabiashara. Hawatakaa wakubali yawe resolved.
 
Mkuu mbona nilikuwa naona Ulaya mambo yanayo husu umeme yanagawanywa katika makampuni matatu tanzu: Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji zote hizo zinafanya kazi independently kwa ufanisi wa hali ya juu, hata kazi nyingine zinakuwa outsourced; kwani Taifa letu ligihiga kutoka kwa wenzetu waliofanikiwa kuna ubaya GANI?

Nakubali kuna mambo mengine yanayo fanyika ndani ya Taifa letu ambayo hayapendezi, lakini haipendezi vile vile kuona kila kitu kinacho pendekezwa na Serikali yetu kina walakini hata kama kina manufaa kwa TAIFA i.e sio kila pendekezo la Serikali liko embedded kwenye UCHAFU.
Mkuu
wenzetu huko Ulaya, wana sheria kali na wanazisimamia kweli ukizingatia hakuna aliye juu ya sheria,
Hapa kwetu ukishakuwa kiongozi unatetemekewa hata na sheria zenyewe.

Inabidi kwanza tupate pa kuanzia ili kuzuia upuuzi wa kifisadi halafu ndipo tuzikabidhi huduma muhimu kwenye mikono binafsi.
 
Hakuna siku nitafurahi kama huo mtaji wa mafisadi unaoitwa TANESCO ukifa,acha hili shirika life halina faida yeyote na likifa ndio matatizo ya umeme yatakwisha haraka sana,serikali has no business kuendesha mashirika ya kibiashara kama haya...au weka fair play 100% na makampuni mengine washindane kwenye hiyo biashara ya umeme then utaona litakavyokufa kifo cha mende na umeme wa kuaminika na bei chee kuanza kumwagika tena...TANESCO must die!!!!
 
Mkuu
wenzetu huko Ulaya, wana sheria kali na wanazisimamia kweli ukizingatia hakuna aliye juu ya sheria,
Hapa kwetu ukishakuwa kiongozi unatetemekewa hata na sheria zenyewe.

Inabidi kwanza tupate pa kuanzia ili kuzuia upuuzi wa kifisadi halafu ndipo tuzikabidhi huduma muhimu kwenye mikono binafsi.

Acha uwoga,mashirika ya simu,ndege,mahotel,factories etc zilizokuwa mali za serikali mbona viliuzwa na vingine kufa lakini maisha yanaendelea tuu vizuri na hivyo vitu sio issue tena...ikifa Tanesco replacement itakuja haraka sana as long as demand ipo,kuna watu/makampuni overseas yana technology/big money yanatafuta pa kuwekeza then leo uwape fair play na wateja millioni 40 unafikiri nini kitatokea?
 
Kuigawa TANESCO hakuna ubaya, maana hiyo inaongeza efficiency. Ila inatakiwa ifanyike kizalendo na kufuata mising corporate governance. Hiyo itatusaidia lakini kama utaingiza ------ Company Ltd kwa ajili ya ujasiatumbo ni ugaidi
 
Back
Top Bottom