Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Hapo Inatakiwa akili pia, kwanza nikupongeze kwa moyo mzuri wa uvumilivu.
Pili hao ukisema uwafukuze haita pendeza pia wakiondoka kulipa deni dahau.
Cha kufanya nafikir kaa nao wakulipe nusu ya deni kwa mkupuo then kaeni andikishaneni awe analipa miezi 3 kabla. Huo utakua mkataba mpya.
Ila mmh najiuliza tu kweli hajawahi pitia hako ka binti au,
Any way utani tu hapo!!
 
Kila mwezi wanaokaa unapoteza 300,000/-. Hata huyo jamaa akipata kazi kukulipa 7m+ sio rahisi. Watafutie vyumba viwili vya 30,000/- ambavyo kodi kwa mwezi itakuwa jumla 60,000/- halafu walipie miezi mitatu wakaanze upya.

Kwa kufanya hivyo wewe utaweza kuweka mpangaji mwingine atakaekupa at least kodi ya miezi 6 ambayo ni 1.8m
 
Wapi huko dsm chumba elfu 30000..?
 
Bwana FUSO wape notice ya miez mitatu wasipolipa watafukuzwa.ikibidi husisha na mwenyekiti wa mtaa husika.Mjini huruma pia ina kipimo chake.
 
Nakushauri ongea nao wote baba,mama na mtoto wao kwa upole ili wakueleze tatizo kubwa hasa linalowakabili ni lipi,ili uligawante hilo deni kwa awamu ambapo wawe wanakulipa kila mwezi na mtiliane saini hati ya makubaliano juu ya makubaliano hayo,sasa wakishindwa hili waondoe kwa kuzingatia sheria za nchi
 
hawatoweza kujakulipa kwamwe, mana deni lina accumulate
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Miaka miwili Ni mingi Sana, Walifaa wawe wamejipanga hata Kama Ni kutafuta Nyumba watakayoimudu.
Umeonesha ubinadamu wa kutosha kuvumilia huo muda wote hata Mungu anaona.
Kama Maisha yakiwashinda warudi kijijini, ukiendelea kujifanya mother Theresa Wewe ndo utaumia sababu hiyo Nyumba ni biashara inafaa ikulipe.
Waambie wajipange unataka Nyumba yako.
 
M
waandikie notice
 
ni kweli kabisa, kwa hili lazima waniewe tu - masuala ya mjini kila mtu alifika na sanduku lake !! Sema kuna wakati imani inanijaa moyoni hasa nikiwacheki watoto wao.

Lakini safari hii wanaondoka tu - shaamua.
 
FUSO kwa heshima kubwa nakuomba uwe na roho ya kibinadamu, wavumilie ila wapige mkwara kuwa wasipitishe mwaka huu bila kulipa kodi. Na kubali wawe wanalipa hata mwezi mmoja mmoja. Asante
 
FUSO kwa heshima kubwa nakuomba uwe na roho ya kibinadamu, wavumilie ila wapige mkwara kuwa wasipitishe mwaka huu bila kulipa kodi. Na kubali wawe wanalipa hata mwezi mmoja mmoja. Asante
kaka nishapiga mikwara saana, cha msingi tupishane na wakishindwa kitakachofuata ni kupiga vitu mnada - Notice tayari nishawapa inaisha 30th Nov Siku ya timbwili.. Maana ni kwenda mahakanani kuikazia notice na kuomba tupige mnada vitu kufidia kodi.

Ushauri tu kwa wasomaji wangu - Maisha yakibadilika na wewe badilika; ishi kutokana na kipato chako cha wakati huo.. kutoka kwenye nyumba ya vyumba vitatu Sinza na kwenda Magomeni chumba kimoja watoto kulala sebureni si dhambi.

Sasa jamaa wengi wanataka ku-maintain status wakati mambo yameshavurugika..sasa haya ndiyo matatizo yake.
 
Mkuu usifanye hivyo tafadhali wacha mwaka huu uishe. Kisha amua jambo tena kiungwana.
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Mkuu tukijitolea kuwachangia kiasi kwa niaba yao,itafaa?
 
Mkuu tukijitolea kuwachangia kiasi kwa niaba yao,itafaa?
Kaka hakuna haja, hujawaleta town na wala hawakukushirikisha wakati wanaongeza famiia....cha msingi walipe tu na kama hawawezi basi wachomoke fasta kabla ya 30th Nov, bado siku 15 tu toka leo..siku za kuwa mstraabu zishaisha.
 
. Mkuu endelea kuwahurumia tu ipo siku wata kulipa fadhila zako usijali.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…