Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,474
Reaction score
45,045
Huyu mpangaji wangu nimemvumilia sana, ni mwaka wa pili sasa anasema mambo yake hayako vizuri, nikienda kumdai kodi yeye na mkewe wanalia sana kwamba nizidi kuwavumilia.

Kuna binti yao yupo form four huyo naye anajiunga nao kunililia anasema baba tusaidie tu babaa tutakulipa huku kanipigia magoti kushika viatu vyangu na suruali.

Imefikia hatua mke wa jamaa ananiandikia sms kuniomba niendelee niwavumilia, hata binti naye anaandikia sms kunipa shikamoo na kuniambia baba naomba tuvumilie tu maana baba yangu hana hela kabisa hata mimi nasoma kwa shida sana babangu.

Anapofanyia kazi huyo jamaa napajua na anapofanyia kazi huyo mkewe napajua ila siwezi kuwaambia sababu ya kulinda maudhui ya hapa JF.

Nipeni ushauri ila mimi naona ni kuwatimua tu tarehe 30th November hii, kifupi kila mtu atabeba sanduku lake mwenyewe na hapa mjini kila mtu kaja kivyake.
 
Na Mimi na wengine humu wenye moyo wa huruma tunaomba uwavumilie, ukiona mkewe amefikia huko ujue 'no more option', wavumilie Mungu atakuepushia vitu ambavyo vingekugharimu pesa kubwa kuliko hiyo, na usifanye kitu kwa mkewe au mtoto wake hata wajipendekeze,najua wapo katika wakati mgumu sana..

ASANTE KWA NIABA YAO.
 
Daah nimebeb kama ndo mimi vile nkajikuta tuu naumia ..ukiona hadi mtoto amejaribu kukuomba nakushauri amini hili maana kama ingekuwa ni starehe anafanya baba basi mkewe na mtoto ungeona wanaonesha utofauti
 
Na Mimi na wengine humu wenye moyo wa huruma tunaomba uwavumilie,ukiona mkewe amefikia huko ujue 'no more option',wavumilie Mungu atakuepushia vitu ambavyo vingekugharimu pesa kubwa kuliko hiyo,na usifanye kitu kwa mkewe au mtoto wake hata wajipendekeze,najua wapo katika wakati mgumu sana..ASANTE KWA NIABA YAO.
kabisa mkuu tunaomba wape muda au wapunguzie walipe nusu ya bei tu.
 
Endelea kuwavumilia....Mungu aliyewapa ugumu huo wa maisha ndiye aliyesikia kilio chako na ukapata nyumba, huyu Mungu ndiye anayekujaribu sasa akupime imani yako kwake.
Amna bhana. Kitu kama icho kwann kila ujinga au uzembe wa mwanadamu mnamshirikisha mungu
 
Sasa kama wanafanyakazi na wanalipwa iwaje watake kukaa bure? Wameifanya hiyo nyumba ya kanisa au, bora wangekuja hata na hela ya mwezi mmoja mmoja, hao watimue. Binti wa form four akimaliza pepa watimue watafute pa kwenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom