MPANDO/MTEREMKO uitwao CHANGALAWE

MPANDO/MTEREMKO uitwao CHANGALAWE

amigod

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2018
Posts
345
Reaction score
264
Habari zenu jf wanachama na wapenzi
MPANDO huu upo mafinga barabara ya iringa- njombe ajari za maroli eneo hilo si kitu cha ajabu mnato kushindwa kuzuia gari ni eneo hatarishi mno kwa wapitao
Mkandarasi ameweka mwendo kikomo wa 50 km ph jambo ambalo linahatarisha sana usalama wa watumiaji wa mabasi na gari ndogo
Ni wakati ukiwa nyuma ya roli umezuiwa kulipita na nyuma yako kuna roli linakufuatia kwa karibu ikitokea mnato wa roli kushindwa kuzuia mwenye gari ndogo yupo hatarini kuwa kizuia kabla ya roli la mbele kuzuia mwinamo ni mkali sana
Wito/ombi langu kwa wanao husika naomba busara na hekima itumike kutengua mwendo kikomo na msitari uruhusu gari moja kulipita lililo mbele kwa kuwa pana unyoofu wa kutosha kufanya hivyo eneo hilo ukiwa kwenye gari ndogo nyuma unafuatiwa na roli panaogofya sana chonde chonde kwa wanao husika kuliangalia upya kabla hatujadhurika kwa kupandwa na roli ikitokea nyuma sababu ya kutekeleza sheria ya mwendo kikomo wa 50 kmph
Ushauri wangu binafsi roli litekeleze mwendo kikomo na basi la abilia/gari ndogo ziruhusiwe kutoka haraka kwenye eneo hatarishi kwa kutokufuata mwendo kikomo huo ni mtizamo wangu binafsi kwa waliopita hapo watachanganua waonavyo
Nawasilisha karibu kwa maoni
 
Back
Top Bottom