Mpaka wa bahari watikisa Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka wa bahari watikisa Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jan 19, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by amini // 19/01/2012 // Habari // No comments

  [​IMG]na Mauwa Mohammed, Zanzibar
  WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamehoji hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupeleka maombi Umoja wa Mataifa (UN) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari.
  Kauli hiyo imewasilishwa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu na kutaka kutoa hoja ili baraza hilo lijadili katika kikao kinachoendelea mjini Zanzibar.
  Alisema hatua hiyo ya Serikali ya Muungano ni nzito inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vema kwani waathirika wakuu huenda wakawa ni Wazanzibari.
  Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa leo katika ofisi za Umoja huo New York, Marekani.
  Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, alitumia busara kubwa na kuwataka wajumbe wasubiri na kuiagiza Serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa Zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa Tanzania.
  Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa Muungano kupeleka maombi hayo kwa Umoja wa Mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.
  Aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo.
  Naye Mwakilishi wa Kuteuliwa, Ali Mzee Ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, anayedaiwa kusimamia na kuwasilisha hoja hiyo UN, hakuweza kupatikana kutoa maelezo ya jambo hilo.
  Jitihada za Tanzania Daima kuonana na Tibaijuka ofisini kwake zilikwama baada ya kupewa maelezo kuwa waziri huyo alikuwa nje ya ofisi kwa shughuli za kikazi na kwamba asingeweza kurudi. Aidha, simu yake ya mkononi iliita mara nyingi bila kupokewa.
  chanzo Tanzania Daima
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  We jusa acha kiherehere
  usijifanye unajua kila kitu, kwanza
  we si mzawa.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  Hongera sana Ismail Jussa.

  Kwani huo ni uvunjifu wa Katiba zote mbili ya Muungano na ile ya Znz. Ni lazima kieleweke hapo na kumjuza Prof Tibaijuka kuwa Znz ni nchi anapaswa kuiheshimu kwa dhati kabisa.

  Hongera sana mwakilishi wangu.
   
 4. s

  saddam Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa wahindi vip? analinda maslahi ya india hyu jusa
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Siku inakuja wakuja woo
  te mtakiona, kiherehere
  kitafika mwisho.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongera Jusa.
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ndo maana kama katiba mpya itachezewa basi tujue kuwa CCM na CUF waweza kufarakana wakati wowote huko zanzibar na majibu yake yakamwangusha vibaya kikwete ndani na nje
   
 8. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani wakati wanapeleka hilo ombi la kuongeza eneo la bahari kulikuwa hakuna mawasiliano na SMZ? Mbona jambo hili linaleta utata. Mi nilifikiri SMZ ingefurahia jambo hilo?
   
 9. k

  kamimbi Senior Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli uelezwe kwa kujibu swali la kwanini wanataka kufanya hivyo? huenda kunasababu za msingi kitaifa, anaye jua sababu naomba anijuze ndo nisapoti au nikanushe.
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Ndugu Wazanzibari, jambo hili si la waziri wa ardhi peke yake bali limepata baraka za baraza la mawaziri ambalo miongoni mwa wajumbe wake ni Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mzanzibari na wazanzibari wengine ambao ni mawaziri karika SMT. Sasa mnataka mshirikishwe namna gani? Jussa kama hujui haya hufai kuwa mwakilishi!
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,031
  Likes Received: 7,430
  Trophy Points: 280
  Hatutuna sababu ya kukubaliana katika hilo, kwani hata tukiamua sasa muungano ukavunjika, Zanzibar haiwezi kutambulia kama nchi mpaka sisi tukubali, kwa umbali ambao Zanzibar ipo, Sheria za Kimataifa za mipaka ya bahari haiitambui zanznibari kama nchi.
  Hivyo achaneni na ndoto za mchana, hilo lingewezekana ingeanza Taiwan kutambuliwa kama nchi.
  Sema ujinga wa viongozi wetu ndiyo unawapa kichwa na kuwajazeni ujinga, ila endeleeni kulalamika bila ya kuona, mwisho haitukuwa mzuri kwenu.
   
 12. G

  Gongolo Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya tusubiri tuone. Inashangaza kuona mambo hayaendi au kuna upinzani kwenye mambo ambayo ni ya nchi moja japo serikali mbili. Nilidhani faida itakuwa kwa ajili ya watz wote kumbe kuna wengine ambao hawahusiki. Basi itakuwa shida na maendeleo yetu yatakuwa yanasuasua kama sisi wenyewe tutakuwa tunalumbana kwenye vitu ambavyo tungeweza tu tukaelezana mezani. Mungu ibariki Tanzania!
   
 13. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jussa hajui,na hajui anaozungumza nao-hata wananchi wake wengi hawana uwezo wa kupambanua maswala kama haya
  somam hapa,upate kuelewa
  https://www.jamiiforums.com/hoja-nzito/209835-kwanini-jussa-anawajaza-ujinga-wazanzibari-wenzie.html


  hawana mawasilaino pale serikali ya tz inapokuwa inafanya mambo ya watanganyika,ambao ndo wengi,ni kama vile viongozi wameshuka kidogo wakaona wao ni watanganyika-bora wafanye maswala ya taifa lao.
  hii ikipita swala la mafuta halitapigiwa kelele na wazanzibar,maana lazima yawe ya share au ya tanganyika
  soma hapa
  https://www.jamiiforums.com/hoja-nzito/209835-kwanini-jussa-anawajaza-ujinga-wazanzibari-wenzie.html
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kaka wewe si ulisema sio Mtanzania.......na ukaniambia kuwa uliwahi kuishi tu kisha ukarudi kwenu sasa Jusa mwakilishi wako kivipi? Au unalengo la kurudi baada ya zenj kujitenga? Mie huwa sikuelewi ndugu wewe ni Mzenj? Mwarabu wa Oman....au wewe wa wapi hasa? Kuna athread moja ulitumia maneno ya kujiondoa kuwa mtz uliposema taifa lenu....nchi yenu......wewe ukajiondoa sasa unawakilishwa vipi na Jussa. Kama wewe mzamiaji then acha usokorokwinyo
   
 15. L

  Logician Senior Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Je swala ili halikupita kwenye baraza la mawaziri?!
   
 16. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,773
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Kwa haraka sana nilifikiri Watanzania wa Wazanzibar wangefurahia hoja ya kuomba kuongezewa eneo jambo ambalo lingewaweza pia hata wao (Wanzania waishio zanzibar )kujitanua kiuchumi katika shughuli za baharini.

  Halafu hii kauli ya "Upande mmoja wa Muungano" sijaielewa. Hawa watanzania wa Zanzibar wanataka kutuaminisha Kuwa JMT ni serikali ya Tanganyika.
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi barua ya maombi ya Wazanzibari waliowakilisha UN kwa Ban Ki Moon kujitenga imeshajibiwa?

  Itabidi Serikali ya JMT ifanye robbing kubwa kwa kutumia influence za Prof. Tibaijuka (former boss UN Habita)
  na Asha Rose Migiro (Deputy UN Secretary), ili hili jambo la mipaka ya bahari lipite haraka, na pia kwa
  kutumia token hiyo hiyo, serikali ya JMT iwatumie watu hao influencial kwenye Siasa za UN kuhakikisha
  ombi la Zanzibar kujitenga na Tanganyika lina gonga mwamba kama unachama wa Zanzibar FIFA!
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Vifungu vipi vya katiba vilivyovunjwa!
  Btw: UN walitoa muda kwa nchi zinazotaka kuongezewa eneo toka ile sehemu ya kimataifa na deadline imefika huyo Jussa alikuwa wapi kutoa maoni yake?
   
 19. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Watanganyika bado mnaendelea kuwacheyea WaZANZIBARI? Subiri muone kali yao, sio wale mambumbumbu tena. Yangu macho.
   
 20. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 881
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Usipojipongeza mwenyewe unamsubiri nani akupongeze.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...