Mpaka wa bahari watikisa Muungano

Mpaka wa bahari watikisa Muungano

Status
Not open for further replies.
written by amini // 19/01/2012 // habari // no comments

dsc047671-564x272.jpg
na mauwa mohammed, zanzibar
wajumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar wamehoji hatua ya serikali ya jamhuri ya muungano ya tanzania kupeleka maombi umoja wa mataifa (un) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari.
Kauli hiyo imewasilishwa na mwakilishi wa mji mkongwe (cuf), ismail jussa ladhu na kutaka kutoa hoja ili baraza hilo lijadili katika kikao kinachoendelea mjini zanzibar.
Alisema hatua hiyo ya serikali ya muungano ni nzito inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vema kwani waathirika wakuu huenda wakawa ni wazanzibari.
Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa leo katika ofisi za umoja huo new york, marekani.
Spika wa baraza la wawakilishi, pandu ameir kificho, alitumia busara kubwa na kuwataka wajumbe wasubiri na kuiagiza serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa tanzania.
Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa muungano kupeleka maombi hayo kwa umoja wa mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.
Aliitaka serikali ya mapinduzi ya zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya umoja wa mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo.
Naye mwakilishi wa kuteuliwa, ali mzee ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, profesa anna tibaijuka, anayedaiwa kusimamia na kuwasilisha hoja hiyo un, hakuweza kupatikana kutoa maelezo ya jambo hilo.
Jitihada za tanzania daima kuonana na tibaijuka ofisini kwake zilikwama baada ya kupewa maelezo kuwa waziri huyo alikuwa nje ya ofisi kwa shughuli za kikazi na kwamba asingeweza kurudi. Aidha, simu yake ya mkononi iliita mara nyingi bila kupokewa.
Chanzo tanzania daima
kwani wao hawamo kwenye serkali ya muungano? Katika watu waliokwenda newyork ni pamoja na mjumbe mmoja kutoka zanzibar au jussa hakulijua hilo?
 
Hatutuna sababu ya kukubaliana katika hilo, kwani hata tukiamua sasa muungano ukavunjika, Zanzibar haiwezi kutambulia kama nchi mpaka sisi tukubali, kwa umbali ambao Zanzibar ipo, Sheria za Kimataifa za mipaka ya bahari haiitambui zanznibari kama nchi.
Hivyo achaneni na ndoto za mchana, hilo lingewezekana ingeanza Taiwan kutambuliwa kama nchi.
Sema ujinga wa viongozi wetu ndiyo unawapa kichwa na kuwajazeni ujinga, ila endeleeni kulalamika bila ya kuona, mwisho haitukuwa mzuri kwenu.

Maajabu haya, kumbe hadi leo karne ya 21 wanaweza wakatokezea watu wenye mawazo kama haya!
 
Jusa hana jipya, anachokitafuta hapa ni umaarufu tu.
 
Kwani wakati wanapeleka hilo ombi la kuongeza eneo la bahari kulikuwa hakuna mawasiliano na SMZ? Mbona jambo hili linaleta utata. Mi nilifikiri SMZ ingefurahia jambo hilo?

Sio mawasiliano na SMZ kwani kitu kizito kama hichi kinachogusa maslahi ya nchi ni lazima kipite Bungeni na Baraza la wawakilishi.

Utaona fika Bunge la Muungano limeshirikishwa na ndio maana mbunge wa Mafia yupo pale lakini halijapitishwa barazani BLW kwa ajili ya kuijadili.

Na hapo ndipo Jussa anapouliza. Ni haki kitu kama hichi kijadiliwe na upande mmoja pasi na mwingine kujadili. Kumbuka ni maamuzi makubwa sana hayo na pasi na shaka yoyote yana nia ya kumeza eneo la Znz kuliingiza katika Tanganyika.

 
Katika kikao cha leo Waziri wa ardhi na makaazi ametamka ya kwamba Kuhusu hili Baraza la mapinduzi halikupewa taarifa yeyote.

Lazima kieleweke hapo.

Kwani kuna namna hapo na hila za kutaka kupora eneo huru la Zanzibar la rasilimali za bahari.

Hongera Jusa kwa kuona mbali.

 
kwenye timu iloenda UN alikuwepo shah wa mafia na zakiah meghiji wa zanzbar,wamewakilishwa vizuri,ombi limeobwa na JMT na si upande mmoja kama huyu paka alichosema
 
kwenye timu iloenda UN alikuwepo shah wa mafia na zakiah meghiji wa zanzbar,wamewakilishwa vizuri,ombi limeobwa na JMT na si upande mmoja kama huyu paka alichosema

Zakhia Hamdani oops Meghji si mwakilishi kutoka Baraza la wawakilishi. Ni mbunge viti maalum Ikulu ya muungano.

Kwa kuwa jambo hilo linahusu pande mbili za muungano basi ni lazima Bunge na Baraza la wawakilishi wajadili. Kwani hiyo ni rasilimali kwa wote.

Kwa kupitia mlango wa pembeni nashawishika kusema kuna namna hapo. Na jusa kaona rafu hiyo.

Tusubiri sasa baada ya BLW kuamua tusikie majibu ya SUK na SMTz wanasemaje.

 
Lazima kieleweke hapo.

Kwani kuna namna hapo na hila za kutaka kupora eneo huru la Zanzibar la rasilimali za bahari.

Hongera Jusa kwa kuona mbali.


Na Baraza limekubaliana Jumaatatu lilijadili suali hili kama hoja ya dharura. Jussa mwakilishi makini na mkombozi wa Zanzibar na Wazanzibari na ndio maana CHADEMA wakawa wanamchukia!.
 

View attachment 45798
Kutoka kulia ni Mhe. Zakhia Meghji ( Mb), Bw. Sergei Tarassenko ambaye ameshika sehemu ya nyaraka za Andiko la kudai eneo la maili 61,000 za bahari, Mhe. Waziri Anna Tibaijuka ( Mb), Mhe. Ombeni Sefue, Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Abulrahman Hassan Shah (Mb) na Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ardhi, Makazi na Madini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia alimwakilisha Waziri wake katika hafla hiyo
Katika kikao cha leo Waziri wa ardhi na makaazi ametamka ya kwamba Kuhusu hili Baraza la mapinduzi halikupewa taarifa yeyote.

Lazima kieleweke hapo.

Kwani kuna namna hapo na hila za kutaka kupora eneo huru la Zanzibar la rasilimali za bahari.

Hongera Jusa kwa kuona mbali.


INAONYESHA HATA VIONGOZI WENU HAMWAFAHAMU-NIMEWAWEKE AMANENO KWENYE PICHA HAPO MUONE KINA NANI WANA WALIWAWAKILISHA,
WENGINE MPO DSM,MNAJIDAI KUFATILIA MAMBO YA ZANZIBAR,WAPI NA WAPI
 
Hongera sana Ismail Jussa.

Kwani huo ni uvunjifu wa Katiba zote mbili ya Muungano na ile ya Znz. Ni lazima kieleweke hapo na kumjuza Prof Tibaijuka kuwa Znz ni nchi anapaswa kuiheshimu kwa dhati kabisa.

Hongera sana mwakilishi wangu.

Wewe ndio maana ndio maana ulikamatwa JKNIA, kwa kauli zako za kipuuzi kama hizi.
 
Watanganyika bado mnaendelea kuwacheyea WaZANZIBARI? Subiri muone kali yao, sio wale mambumbumbu tena. Yangu macho.

Tulia mkeketwe nyie Wazanzibari, kwani mnajua hata lile ombi lina contents gani ndani yake?. Kama ndio mnasituka sasa wakati document ziko UN mlikuwa wapi wakati zinaandaliwa kama mna inteligency yoyote ya kukusanya habari yenye maslahi yenu?. Kwa kuwa mmelalamika, siyo mbaya subiri mnyama akichinjwa nanyi damu itawarukia kidogo.
 
Hongera sana Ismail Jussa.

Kwani huo ni uvunjifu wa Katiba zote mbili ya Muungano na ile ya Znz. Ni lazima kieleweke hapo na kumjuza Prof Tibaijuka kuwa Znz ni nchi anapaswa kuiheshimu kwa dhati kabisa.

Hongera sana mwakilishi wangu.


mbona matiba ya zanzibar imevunja katiba ya muungano kwa kusema kuwa zanzibar ni nchi/
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom