Fundi manyumba
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 3,799
- 8,103
- Thread starter
- #161
Mkuu niseme nashukuru sana sana sana tena sana kwa ushauri wako...Inaonekana uko kwenye uhusiano wenye changamoto, hasa kutokana na hisia zako za kutothaminiwa au kupewa muda na mwenzako.
Hii hali inaweza kusababisha kutoelewana na kukufanya ujihisi kama wewe ndiye unayejitoa zaidi.
Kupata ufumbuzi wa kadhia hiyo, unapaswa kuzingatia mambo kadhaa yafuatayo:-
Weka wazi hisia zako
Weka wazi hisia zako kwake, lakini kwa namna ya utulivu na yenye lengo la kuelewa na kutatua changamoto zenu.
Pima Matarajio Yenu
Pengine wewe na mwenzako mko na matarajio tofauti kwenye mahusiano yenu.
Hivyo, zungumzeni kuhusu malengo na matarajio yenu ili kuona kama mpo kwenye ukurasa mmoja.
Je, ana Dalili za Kukupenda?
Kama tabia yake inaonesha ukosefu wa kujali kwa muda mrefu, inaweza kuwa ishara ya kutokuwepo uwekezaji wa kihisia kwake.
Jaribu kuangalia kama kuna ishara nyingine zinazoonyesha kutopendezwa kwake na uhusiano wenu.
Thamini Nafasi Yako
Kama unajihisi kutopewa thamani unayostahili, pengine ni wakati wa kutathmini kama uhusiano huo unakidhi haja zako au yanaongeza thamani kwako.
Ova
Natamani hata nikupe namba ili uweze kunifanyia solution kwa hili jambo...
Kuna mda nilikaza week nzima bila kumchek ila cha ajabu na yeye akawa kimya hana habari na mimi...
Sasa hvi nataka nikitoka nitoke mazima yaani mazima sitaki kurudi nyuma na najua huyu kwa sasa anajua kuwa kwake sichomou sasa nataka nimshangaze kama muhindi anavoshangaza watu...
Nataka niwe kama Natafuta Ajira tuu nafata principal zote