Mpaka Sasa hivi kuna haja ya kuwa na mfumo wa vyama nyingi vya siasa?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Mpaka Sasa hivi kuna haja ya kuwa na mfumo wa vyama nyingi vya siasa?

Nafikiri huu ni wakati watanzania tuchague mfumo wa kifalme,au mfumo kama ule wa China,au mfumo kama ule wa Korea ya Kaskazini la sivyo wenye maoni tofauti na Serikali kwa tafsiri ya sasa ya neno uchochezi baadhi ya watanzania wataishia magezezani,kwa mujibu wa sheria ya uchochezi.

Pili lawama nyingi za utawala huu kwa wapinzani wanasema waziwazi kuwa kazi ya wapinzani ni kupinga maendeleo,tena wameenda mbali zaidi wanasema wafugwe jela,wapotezwe na kadhalika,kwa maneno na tafsiri kama hizi kwanini tusiige mfumo kama wa China ili tusifungane kwa makosa ya uchochezi?

Au inawezekana mwl,nyerere aliumiwe kwa kutuletea vyama nyingi vilivyokuja kutucheleweshea maendeleo? Tumlamu nani aliyeleta mfumo huu ambao kwa sasa unaonekana kama unakwamisha maendeleo?

Mwinyi,mkapa,Kikwete au Mwl Nyerere?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimuuliza mtu kama Jingalao et al, watakuambia ufutwe tu maana hauna maana yoyote ile zaidi ya kuleta tu vurugu na bla bla nyingine.

Kwa wapenda maendeleo ktk nyanja zote, tutasema mfumo wa vyama vingi uendelee daima ili kukifanya chama kilichopo madarakani na viongozi wake, waweze kujisahihisha kupitia wale wapinzani wao. Sasa kama upo kwenye mfumo wa vyama vingi, halafu unataka kuiendesha nchi kama ya chama kimoja, basi hapo lazima utundulisu utatamalaki.
 
Kazi Moja wapo ya Vyama vya Upinzani Ni kupambana Na Udikteta wa Kidola sio kutaka Kila kitu kiwe Sawa ndio wao wafanye Siasa

Kazi Moja wapo ya Vyama vya Upinzani ni kushinikiza Dola kupitia Umma kuheshimu Utawala wa Sheria
Na Ukiona tofauti tambua Kila Mtu ana Makosa

Wao wameshindwa kutengeneza Ushawishi kwa Umma Na Dola inatumia udhaifu huo kuendelea kujiimarisha

South Africa wangekuwa legelege Kama Wapinzani wetu Basi uhuru wangeusikia kwenyw Tamthilia
 
Sijawahi kumwona binadamu anayekimbilia utumwa, ila kizazi hiki yaonekana kinapenda kuishi katika laana ya utumwa. Tunaishi katika karne ya kipekee sana. Tunashuhudia binadamu wa aina zote wakipambana kufa na kupona ili wawe huru, kuanzia Saudia mpaka Vatican kwa Papa Francis.

Ajabu ni hawa wanadamu ambao Mungu kawaumba katika nchi ya Tanganyika wanaotamani kutawaliwa kiimla huku wakitekwa na kama kuku. Tamaa ya aina hii yawezekana ni kukata tamaa kulikopitiliza ambapo mtu anaona kuliko kuamua hatima yake, ni bora akaishi utumwani tu mradi ameshibisha tumbo na kulala.

Kama watanganyika tuna mawazo haya, hakika nchi bado ina laana na inapaswa kufanyiwa maombi mwaka mzima bila kikomo.
 
Nini kifanyike?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom