Mpaka leo hakuna kitu. Huwa wanamtisha nani??? Au ni kuwa hawakuonewa??

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,129
4,712
1. Kutajwa kwenye madawa ya kulevya, Mbowe aliwaka kuwa atamshtaki Makonda mahakamani kutokana na kuchafuliwa jina.

MPAKA LEO HAKUNA KITU

2. Kuharibiwa kwa miundombinu ya shamba lake, Mbowe akasema atamshtaki Byakanwa mahakamani na kudai fidia ya Milioni 500

MPAKA LEO HAKUNA KITU

3. Kutajwa kama Mtu hatari kwa taifa hili, Yerico Nyerere aling'aka na kusema kuwa atampeleka Musiba mahakamani.

SIJUI KAFIKIA WAPI?

4. Kalist Lazaro, baada ya kuwekwa ndani masaa 48 kutokana na kupeleka rambirambi St Lucky Vicent na Mla Rambirambi, Mr Gambo, akatoa siku saba za kuombwa msamaha la sivyo atampeleka Gambo mahakamani.

MPAKA LEO HAKUNA KITU

5. FATMA KARUME baada ya kughasiwa na askari na kumsababishia maumivu ya bega, alifungua kesi dhidi ya askari yule na kudai bilioni moja

MPAKA LEO SIJUI KESI IMEFIKIA WAPI??

Nimewataja hawa watu kwa kuwa ni VIOO VYA JAMII, kama wao wanashindwa kudai haki zao mahakamani, vipi kuhusu raia wa kawaida ambao kutwa wanaonewa na vyombo vya serikali??

Je watu hawa hawaoni kuwa iwapo kesi zao zingeunguruma na mwisho mahakama kutoa haki, ingewasaidia raia wengi sana kufunguka macho dhidi ya uonevu wanaofanyiwa???
 
Back
Top Bottom