Hatimaye wakili wa Mwakinyo kafika mahakamani leo

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Hapa sasa Mwakinyo kaanza kuwa mwelewa kwa sababu huko nyuma alikataa wito wa mahakama mpaka kupelekewa wito kupitia gazeti la Mwananchi. Pia wakili wake kakubali kusuluhisha mambo yao nje ya mahakama. NB; Hata kama una-connections, lazima uwe makini na sheria.

Dondoo muhimu,

Bondia Mwakinyo ameiomba mahakama impe siku 21 ili aandae majibu ya madai yaliyofunguliwa dhidi yake.

Mwakinyo ametoa ombi hilo leo Novemba 20 kupitia wakili wake Azadi Athumani baada ya kuitikia wito wa mahakama.

Katika kesi hiyo ya madai namba 227/2023 kampuni ya PAF Promotion imewasilisha madai nane likiwemo la Mwakinyo kuilipa TSH 150 Milioni kama madhara ya jumla waliyoyapata.

Katika maelezo yake, wakili wa Mwakinyo amekiri kuwa taarifa ya wito ameipata na ndio maana amekuja mahakamani leo.

Hakimu baada ya kusikiliza hoja za pande zote amehairisha kesi hiyo mpaka Disemba 11, 2023.

Nje ya Mahakama;

Baada ya kesi kuhairishwa, wakili wa Mwakinyo na PAF Promotion walifanya majadiliano na kukubali kufanya usuluhishi nje ya mahakama.

"Kama majadiliano yatakwenda vizuri, tutaifahamisha mahakama na tarehe ijayo ya kutajwa kwa kesi, tunaweza kuiondoa kesi hii mahakamani na kuisikiliza nje ya mahakama" Amesema wakili Kauki

Chanzo; Gazeti la Mwananchi

PIA SOMA:
- Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni


- Bondia Hassan Mwakinyo amepata pigo la kwanza katika kesi aliyofunguliwa na Promota
 
Mabondia wengi ni maskini sababu ya kudhulumiwa /kunyonywa na hawa mapromota.Naona suala la Mwakinyo kujitambua tafauti na mabondia wengine ndio limepelekea haya yote!
 
Back
Top Bottom