Mpaka hapa tulipo,US ndio taifa linaloogopeka Duniani

Mpaka hapa tulipo,US ndio taifa linaloogopeka Duniani

Ila shangazi yako anatumia ARV za USAID, Mwanao anatumia Chandarua Cha Msaada. Akiugua malaria anapewa mseto.

Bibi yako na Wazazi wako tasaf ya wamarekani yasababisha waishi.

Wewe mwenyewe msaada wa marekani

Amefanikiwa kukufanya uwaze na kuwa na akili ya kwamba, bila ya mareakani hata hewa unayovuta haitapatikana.
 
Kwanza, nimejiuliza kuhusu vita ya Russia na Ukraine, kwamba pasingekuwa na mkono wa US tayari biashara ingeisha mapema sana. Saa hizi Ukraine yote ingekuwa imepambwa kwa bendera za Urusi tu.

Pili nimejiuliza inakuwaje, Putin alitoa ahadi ya kumshughulikia kikamilifu yoyote atakae jiingiza kwenye hiyo vita kwa namna yoyote.

Lakini mbaka sasa US anaonyesha waziwazi ushiriki wake lakini sioni action yoyote Putin anayochukuwa kwa aliewaonya kujihusisha na vita hiyo.

Tatu najiuliza, kwanini US wanatoa taarifa ya kila kitu wanacho peleka Ukraine,Yani vifaa vya kijeshi.
Wanasema wazi kabisa, mwezi huu tunapeleka silaha flani,mweziujao tunapeleka silaha flani nakweli zinakwenda waziwazi bila kificho.

Sasa tushangae wote, kwanini nchi nyingine hawatangazi kumsaidia Putini kijeshi waziwazi?.

Kwanini hatakama wanamsaidia kwa kificho,kwanini US anawafuatilia na akiwataja kwamba wanamsaidia Putin wao wanakimbia haraka kwenye Media kukanusha kwamba hawajasaidia chochote.
Wanakataa kata kata, wanaogopa nini kusema ndio tunamsaidia bwana Putini kujilinda.

Mbona US wanatangaza wenyewe kwamba tunapeleka silaha na wanapelekakweli.
Inamaana hawa muhofii mtu yoyote. Kwanini?

Hapo sijaweka tukio la Taiwan sababu wote tunajua kilicho tokea.
Hilo taifa unalolisifia limekaa Afghanistan miaka ishirini limeshindwa kuwatoa wanamgambo wa Wataleban. Russia anapigana na NATO Nchi 20 usiwe kama kipofu au kiziwi we buda
 
ushakuwa mwl wa kiswahili muda huu ? [emoji23][emoji23] ebu jikite kwenye mada tutolee upopoma wako humu sio darasa la uandishi
Hujui kwamba kuandika neno (kukosea) vibaya kunaweza kubadili maana yake lengwa? Angalia kiasi/kiazi, kazi/kasi nk

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Alimpora au Russian Tsar alimuuzia hiyo territory USA kama Mexico alivyouza Northern Mexican territories zilizokuwa chini yake kama New mexico ,Nevada ,Arizona na California Kwa USA baada ya vita kati ya Mexico na USA federation ?
Yale yalikuwa mauziano au uhun
 
Hilo taifa unalolisifia limekaa Afghanistan miaka ishirini limeshindwa kuwatoa wanamgambo wa Wataleban. Russia anapigana na NATO Nchi 20 usiwe kama kipofu au kiziwi we buda
Mimi sija sifia taifa mkuu, nimeeleza kinachoendelea katika nchi zinazo shiriki kusaidi vita kati ya Russia na Ukraine.
 
Ok, sasa itakuwaje kama Ukraine akipata misaada ya kijeshi ambayo itamlazimisha Putin kupoteza majeshiyake kwa wingi na kunyang'anywa maeneo yote aliyo yateka.

Yani Zelensky akiweza kuwatimua warusi mbaka Crimea kwa nguvu ya misaada kutoka kwa US na NATO, itakuwaje,Putin atakubali?.
Hiyo hali ya kukimbizwa kimbizwa haitamchukiza kiasi cha kutumia uwezo wake wote?.

Putin atakubali kuvumilia hasara na aibu kama hiyo?

Kutokana na sababu zilizo pelekea hii vita, Putin atakubali kushindwa na kuwambia warusi tumejaribu tumeshindwa?then watamuona Shujaa' ama watamuona aliingiza nchi kwenye matatizo bila sababu?.

Hapo nawaza,Putin anauonaje mwisho wa hiivita hukombeleni ikitokea ameshindwa.

Ama ataamua kumaliza uwezowake wote hatakama utakuwa na hasara kubwa kwa maadui na kwake Ilimradi afe kiume?.
Mkuu hapa kuna kitu ambacho wengi hawajakiona. Marekani yeye anachokitaka ni kukuona Russia ikitumia Silaha za nuclear ili aweze kumaliza mchezo.
Urusi imeshazingirwa na makombora ya nuclear kila pande na hakika nawambia Russia akianzisha vita ya nuclear basi Russia itafutwa kabla ya hayo madhara mnayoyahofia hayajatokea.

Tatizo tunaichukulia us kirahisi
 
Kwa hiyo aliuza kwa wababe au?
Miezi kama miwili hivi ilIyopita nilisikia kuna mbunge mmoja wa Russia alisema US wakiendelea kujihusisha na vita ya Ukraine, warusi wafikirie kurudisha jimbolao la Alaska sababu US walilipata kwa ulaghai.
 
Kwaio wanaifuta urusi na raia zake ama?
 
Miezi kama miwili hivi ilIyopita nilisikia kuna mbunge mmoja wa Russia alisema US wakiendelea kujihusisha na vita ya Ukraine, warusi wafikirie kurudisha jimbolao la Alaska sababu US walilipata kwa ulaghai.
Kwa akili yako unahisi wataweza kurudisha?
 
Back
Top Bottom