Moyo wa kusaidia

Iam Lupa

Member
Sep 22, 2023
37
75
Ilikuwa 2002, nikiwa na miaka 8 tunilipata ajali mbaya tena mzaingira ya mbali na nyumbani.

Kwa wakazi wa mtoni mtongani kuna sehemu panaitwa ngazi mia kule relini. io siku mimi na jamaa zangu baada ya maumziko ya shule tulienda kutembea maeneo ya relini,zile ngazi zilikuwa nyingi sana takribani 100 hivi (ingawa kuna zingine zilishavunjika) zilijengwa zamani sana (in history ni toka kipindi cha mkoloni wakati wanajenga reli).

Basi bwana tulifanikiwa kuzipanda ngazi zote hadi juu kabisa ya reli ila wakari wa kurudi chini mwenzangu mmoja akanisukuma(kama unavojua michezo ya watoto tena)nilijipiga kwenye ngazi tokea juu mpaka chini na mwisho nikapoteza fahamu.

Sikujua nini kiliendelea mpaka niliposhtuka nikiwa hospitali nimefanyiwa matibabu. Ilipita siku nzima hadi taarifa zilipofika nyumbani sababu mmoja wapo wa watu nilioenda nao alikuwa ndugu yangu.

Basi siku iliyofuata kabla ya wazazi kufika alifika mama mmoja hivi na kikapu ndani yake aliweka chakula sikuwa namfahamu ila alinipa chakula nikala badae akaja daktari akawa anazungumza nae, basi baada ya muda kidogo wakaja wazee wangu baba na mama ila nikaona wanaongea na yule mama.

Ile siku nikaruhusuiwa kutoka pale hospitali tulifika nyumbani lakini yule mama halikuwa anakuja mara kwa mara. ila badae nilikuja kujua yule mama ndo mtu alonisaidia toka siku niliopata ajari alikuwa na moyo safi sana.

NI MUDA SASA UMEPITA NA NIMEMKUMBUKA YULE MAMA ILA NIMEMSAHAU JINA NILIKUWA NAMUITAGA..
 
Humanity bado ipo. Jitahidi na wewe urudishe fadhila, sio lazima kwa yule maza wala ndugu yake, kwa mtu yoyote.

Hafu yule dogo aliekusukuma ulimsamehe?
 
Humanity bado ipo. Jitahidi na wewe urudishe fadhila, sio lazima kwa yule maza wala ndugu yake, kwa mtu yoyote.

Hafu yule dogo aliekusukuma ulimsamehe?
hakika ndugu inabidi fadhila iendelee kuishi nami.
yule dogo yaliishaga ni michezo ya utotoni ingawa imekuwa na affect kubwa kwenye afya
 
Kuna mama aliniokoaga kwenye shoti ya umemee niliganda kabisa...akankbika na mti mkavu nikadondoka,sikuwai kumjua huyo mama,wala majirani hawamjui,wazazi walijaribu kumtafuta hawakumpata.
 
Kuna mama aliniokoaga kwenye shoti ya umemee niliganda kabisa...akankbika na mti mkavu nikadondoka,sikuwai kumjua huyo mama,wala majirani hawamjui,wazazi walijaribu kumtafuta hawakumpata.
kuna watu wanatokeaga tu vile mungu amependa kuja kusaidia wengine.
 
Back
Top Bottom