Pambana utazipata๐Sina pesa
Kukusaidia kwetu wajibu,MOYO UNA MENGI.
Kiukweli ni mapito haya napitia
Moyo umeshindwa hauwezi kutulia
Mbona kutamka nafusi yanizuia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Natamani kusema na kuyasimulia
Lakini sijui nani nitamuambia
Ayaweke moyoni nayo akatulia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni
Kitu nilichojifunza kwenye kwa dunia
Upige mkelele nani atasikia
Hakuna mtu atakaye kuhurumia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Watasema tulisema na kumuambia
Na tulimkanya kisha tukamuusia
Mwacheni aumie kesho hatorudia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Acha nijikaze na pia kuvumilia
Na niwaeleze muende kuhadithia
igeuke fimbo kwangu ya kunichapia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Mtanicheka na sio kunisaidia
Na msonipenda mzidi kufurahia
Kisha ninao wapenda watanikimbia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
[emoji2398]ibn kimweri.
Ooh pole...kalamu ya mtenziNi kweli
Kalamu inaandika inayohisi
Hatimae Kalamu imepata liwazo zuri๐๐Kukusaidia kwetu wajibu,
Kwa maswali yaso majibu,
Elezea yanayo kusibu,
Waungwana tuweze kujibu
Fukuto Kama motoni,
Kubeba kero moyoni
Furaha tele usoni
Machungu tosha rohoni
We toa yanayokuchoma,
Waungwana tutakusoma
Ushauri bila kukoma
Uchungu upate kukoma
Kalamu ya mwandishi Ina hisia Kali.Hatimae Kalamu imepata liwazo zuri๐๐
Hakika naww ni mkali wa vina umelenga mule mule..uko aliko mwenye kalamu hana hali๐๐Kalamu ya mwandishi Ina hisia Kali.
Sisy umetisha.Kukusaidia kwetu wajibu,
Kwa maswali yaso majibu,
Elezea yanayo kusibu,
Waungwana tuweze kujibu
Fukuto Kama motoni,
Kubeba kero moyoni
Furaha tele usoni
Machungu tosha rohoni
We toa yanayokuchoma,
Waungwana tutakusoma
Ushauri bila kukoma
Uchungu upate kukoma
Kwetu vipaji ni urithi๐๐si unaona unavyolipeleka goma kuleSisy umetisha.
Uko vizuri.๐
Nasubiria atuelezee waungwana yanamsibu tumpe tibaHakika naww ni mkali wa vina umelenga mule mule..uko aliko mwenye kalamu hana hali๐๐
Jinsi ulivyo flow..tayari tiba kashaipata uko na Kipaji cha asili ๐๐Nasubiria atuelezee waungwana yanamsibu tumpe tiba