Moyo Ulioonja Maumivu

SEHEMU YA 74

Hilo likamfanya mke wake kuhisi kwamba mume wake alikuwa na stresi kwa sababu ya mtoto wake aliyekuwa kitandani akiugua. Moyo wa Violeth uliumia zaidi, ni kweli aliumia kuona mtoto wake akiwa kwenye hali hiyo lakini suala la Theo kuanza kunywa pombe kuondoa stresi ilimuumiza zaidi.

*** Daktari waliendelea kumfanyia matibabu Rachel, hakuonyesha nafuu yoyote ile kitu kilichowafanya kuitana na kuanza kuijadili afya yake.

Hakukuwa na dalili zozote za kupona na kurudi kwenye hali yake ya kawaida kitu kilichowafanya kuwasiliana na madaktari wa Hospitali ya Munich Medcal Centre ambayo ilikuwa na watalaamu wa magonjwa ya moyo na kuwataka Theo na mke wake wamuhamishie mtoto wao huko Ujerumani.

Iliwaumiza mno, kitendo cha madaktari wa India kushindwa kumtibu mtoto wao waliona kabisa kwa sehemu nyingine isingewezekana.

Waliambiwa kuhusu hospitali hiyo iliyokuwa jijini Munich nchini Ujerumani kwamba ilikuwa na watalaamu wengi lakini bado hawakutaka kuamini.

Kibali cha Rachel kupelekwa huko kikatolewa na watu hao walitakiwa kuondoka naye haraka sana kuelekea nchini huko.

Kichwa cha Theo hakikumuwaza mtoto wake wala safari hiyo, alichukua muda mwingi kumuwaza Iyanya, alitakiwa kumfuata na kuzungumza naye, alitakiwa kumwambia kila kitu kuhusu safari hiyo .

Hakujua angezungumza naye vipi kwani waliambiwa kwamba ni siku hiyohiyo ndiyo ambayo wangeondoka kuelekea nchini Ujerumani haraka iwezekanavyo.
“Ngoja niende chooni,” alimwambia mke wake.

Akainuka na kuelekea chooni, huko kama kawaida yake akapata nafasi ya kuzungumza na Iyanya, alimwambia kuhusu kile walichoambiwa na daktari hivyo msichana huyo kutakiwa kurudi Afrika Kusini.

“Kwa hiyo nirudi nyumbani?” aliuliza Iyanya.
“Ndiyo! Haina jinsi! Ila nitakukumbuka sana,” alisema Theo huku akionekana kuwa mnyonge mno.

“Na mtarudi lini?”
“Bado sijajua! Ila nadhani hivi karibuni.”
“Sawa. Kwa hiyo unaniachaje?” aliuliza msichana huyo.

“Nakutumia dola elfu tano kwenye akaunti yako mpenzi!” alisema Theo.
“Sawa. Nashukuru mpenzi!” alisema Iyanya na kukata simu.
 
SEHEMU YA 75

Kwa Iyanya hakuwa na kipingamizi, alimpenda sana msichana huyo na alikuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yake, akamtumia kiasi hicho cha pesa na kuondoka kuelekea nchini Ujerumani usiku wa siku hiyo.

Njiani, muda wote mke wake alikuwa akilia, aliumia moyoni mwake kila siku, hakukuwa na kipindi kilichomuumiza moyo wake kama kipindi hicho.

Walichukua saa kadhaa, wakafika Ujerumani ambapo tayari gari la wagonjwa lilikuwa mahali hapo na kuwachukua kuwapeleka katika Hospitali ya Munich Medical Cenntre.

Baada ya kufika, kitu cha kwanza madaktari wakachukua ripoti ya Rachel na kuanza kuiangalia, ilikuwa ni lazima waangalie jinsi matibabu yake yalivyofanyika na hata mambo mengine ili wajue ni mahali gani wangeanzia.

“Moyo umevimba! Mungu wangu! Inakuwaje tatizo hili kumpata mtoto mdogo hivi?” aliuliza daktari mmoja huku akionekana kushangaa.

Hiyo ilikuwa kazi nyingine waliyotakiwa kufanya, ilikuwa ni lazima wapambane kuhakikisha mtoto huyo anapata nafuu na kupona kabisa.

Hali yake ilitisha na kila walipomwangalia, hawakuona kama angeweza kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida.

Walimuomba Mungu, Rachel alikuwa mdogo mno kufanyiwa upasuaji mara kadhaa kama ilivyotakiwa kuwa lakini hawakuwa na jinsi, ili kuyaokoa maisha yake, ilikuwa ni lazima upasuaji mwingine ufanyike haraka sana.

*** Bado Iyanya alikuwa bonge la demu, aliendelea kuwatingisha wanaume wengi, hakukuwa na aliyesalimika mara tu baada ya kumuona msichana huyo.

Wengi walimpapatikia, chuoni wanafunzi wa kiume walikoma, walichanganyikiwa na umbo lake, wakachanganyikiwa na sura yake na wengi kumfuata na kutaka kutoka naye kimapenzi lakini msichana huyo hakutaka kukubali.

Alichokiangalia kilikuwa ni pesa tu, hakuwa tayari kutembea na mwanaume asiyekuwa na pesa na ndiyo maana alikuwa radhi kufanya lolote lile kwa mwanaume ambaye alimpa kiasi fulani cha pesa baada ya kufanya mapenzi.
 
SEHEMU YA 76

Siku zilikatika, alirudi nchini Afrika Kusini na kuendelea na maisha yake. Watu wenye pesa waliendelea kumfuata na mwanaume mwengine ambaye alionekana kudatika naye alikuwa bilionea Ezekiel Khone, mwanaume aliyekuwa na pesa nyingi sana hapo Afrika Kusini.

Siku ya kwanza alipomuona Iyanya, alichanganyikiwa, alimwangalia msichana huyo mara kibao, hakupata jibu kama alikutana na binadamu au malaika aliyeshushwa kutoka Mbinguni.

Alimwangalia, Iyanya alikuwa maana halisi ya mwanamke aliyekamilika, kwenye kila idara alivutia na kulikuwa na kila dalili kwamba ndiye alikuwa msichana mrembo kuliko wote hapo Afrika Kusini.

Hakutaka kuchelewa, haraka sana akamwambia kijana wake kwamba alihitaji kuzungumza na msichana huyo kwa kuwa alionekana kuwa na sifa zote za kulala naye katika kipindi hicho.

Kijana huyo akatumwa na kwenda kuzungumza na Iyanya, alipomfikia, hakutaka kumwambia maneno mengi, akatoa pesa, kiasi cha dola elfu mbili na kumpa msichana huyo aliyekuwa amekaa na wenzake kwenye mgahawa mmoja.

“Nimetumwa nikupe hizo,” alisema kijana huyo huku akimpa msichana huyo pesa hizo, marafiki zake wote wakashangaa.

“Zimetoka wapi?”
“Kwa bosi wangu!”
“Nani?”
“Aliyepaki ile Lamborghin hapo nje!” “Mh!” aliguna Iyanya huku akiziangalia hizo pesa.
 
SEHEMU YA 77

Hakutaka kujivunga, akazichukua na kuziweka kwenye mkoba wake, kijana huyo akampa na kikaratasi na kalamu.
“Amesema anahitaji namba yako!” alisema kijana yule.
“Ya nini?”

“Nadhani kuwasiliana!”
Iyanya hakutaka hata kuchelewa, akachukua kalamu ile na kuandika namba yake ya simu na kumpa kijana huyo ambaye akaondoka kuelekea kwa bosi wake ambaye hakumjua kabisa.

Kwake, akili yake ilimwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa na pesa, isingewezekana kwa mwanaume wa kawaida kumpa dola elfu mbili halafu asiwe na pesa, ila ukiachana na hilo pia aliambiwa kwamba alikuwa na gari aina ya Lambornghin, moja ya magari gharama duniani, hivyo akajua kabisa kwamba alikuwa na pesa.
Baada ya kumaliza kula, wakaondoka na kurudi nyumbani.

Alipofika huko, hakukaa sana, mara simu yake ikaanza kuita, alipoagalia kioo, ilikuwa namba ngeni, alijua tu kwamba alikuwa mwanaume huyo, akaipokea.

“Halo!” ilisikika sauti ya mwanaume kutoka upande wa pili.
“Naonge na nani?”
“Mr Khone!”
“Ndiye nani?”
“Nilimtuma kijana wangu akuletee pesa, ulizipata?”

“Oh! Kumbe ni wewe! Asante sana, nilizipata!”
“Safi sana. Hivi unaihsi wapi? Naweza kuonana na wewe?” aliuliza mwanaume huyo kwenye simu.

“Kuonana na mimi? Kuna nini?”
“Nataka nizungumze nawe!”
“Zungumza nakusikia!”
“Kwenye simu?”

“Ndiyo!”
“Hapana bwana! Naomba tuonane sehemu yoyote ile,’ alisikika mwanaume huyo.

“Sawa. Nitakutaarifu!”
“Sawa!” alisema mwanaume huyo na Iyanya kukata simu.
|
|
|

Nipo bize kuandaa kukimalizia kitabu cha DILI LA DOLA BILIONI NNE ambacho kitatakiwa kuingia sokoni mwezi ujao. Kitakuwa sh. 10,000/= na kitakuwa na kurasa 380. Kama utahitaji kuweka oda yako mapema, njoo kwenye meseji za kawaida 0718069269.....USITUME KWA WHATSAPP KWA KUWA SIPO HUKO KWA MUDA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom