Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Hii ni zaidi ya kuimbiwa....
Mwisho wa juma hili nilikumbuka nyumbani, nikaja na ndege ya jioni na alfajiri nikaanza safari, kuna kiota kimoja nilikitembelea nje ya jiji la Dar es Salaam. Nilikuwa mwenyewe kwenye safari hii na nilitumia usafiri wa jumlati yaani mabasi.
Nilifika salama na baada ya ku check in hapo kwenye kiota nikaenda kaa kwenye bustani ili nianze tafakuri na kuipatia chakula akili.
Nikiwa kati kati ya kufikiri akaja mhudumu na kuniuliza kinywaji. Nikatoa oda yangu na nikaagiza na chakula kabisa maana mchana ulikuwa umeshaingia. Baada ya tafakuri kadhaa na kupata mlo na vinywaji nikachukua kitabu changu nikaanza kusoma. Nilipoona naanza kusinzia nikamuita mhudumu anipe bili nisaini kisha niingie chumbani kupumzika kidogo ili usiku niwe na wakati mzuri wa kufurahia.
Mhudumu alipokuja nikamwambia nipe bili nisaini kisha ntalipa siku ya kutoka, akaniambia dada samahani bili yako imeshalipwa... nikamuuliza nani kalipa akasema yule palee akionesha mkaka mmoja hivi ile kumtizama vizuri looh mapigo ya moyo yakaanza kushuka, nikaanza kurojeka hadi nikashindwa kuinuka, yule mhudumu aliiona ile hali na akanisaidia hadi chumbani kwangu.
Wajua ni nani aliyenilipia bili? Sam....yule yule aliyenipenda tangu tuko chuo...
Ilikuwa kuwaje naye akawa pale ni habari ingine ila kwa sasa ni kuwa tulikuwa na wakati mzuri na tulikuwa pamoja muda wote tuko kwenye kile kiota. Leo mchana tumerudi na gari ya Sam na njia nzima nilikuwa naimbiwa nyimbo ila huu ndo umenikaa hadi saa hii.
Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti
Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme) Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosaga
(Wacha waseme) Nimekupendea nini.
Namshukuru maulana nimemaliza juma hili kwa raha na afya niko mwepesiiii na nguvu mpya kwa ajili ya wiki ijayo.
Alamsiki.