Angalia takwimu hizi:
kwa hawa watu uliowataja (Mourinho na Guardiola): Mourinho katoka FC Porto kaja Chelsea 2004-05 akawakuta Lampard, Terry, Makelele, Joe Cole, Gallas, Geremi, Veron, Adrian Mutu, Wayne Bridge, Glenn Johnson, Damien Duff na wengine katika ubora wao; akawaongeza Drogba, Petr Czech, Ricardo Carvalho, Tiago, Arjen Robben, Cole, Essien, Obi Mikel na wengineo wakiwa katika ubora wao. Hakuwa na kazi ngumu kuchukua EPL. Akaenda Inter Milan 2007 akawakuta wakina Sebastian Cambiaso, Maicon, Zanetti, Zlatan Ibrahimovic, Materrazi, Balotelli na Adriano wakiwa katika ubora wao; akawaongeza Eto'o, Milito, Quaresma na Muntari katika ubora wao. hakuna ambacho kingeshindikana kwa yeye kuchukua Scudeto na Italian Super Cup. Akaenda Madrid 2010-11 akawakuta Cassilas, Ramos, Ronaldo, Marcelo, Pepe, Arbiol, Arbeloa, Guti, Benzema, Kaka, Alonso, Ronaldo na wengineo katika ubora wao; akawaongeza Carvalho, Khedira, Ozil, na Di Maria katika ubora wao. Haikumpa shida kuchukua Copa del Rey msimu huo na La Liga msimu uliofata. Amerudi Chelsea kawakuta Hazard, azpiliqueta, Ivanovic, Luiz, Oscar, Ramires, Cahil na wengineo katika ubora wao; akawaongeza Willian,Schurle, Nemanja Matic na Demba Ba katika ubora na Eto'oo ambaye hachuji. Katika timu zote alizopitia forward line yake iliundwa na wakina Drogba, Eto'o, Ibrahimovic, Milito, Ronaldo, Benzema na sasa Eto'o na Torres.
Guardiola anaichukua barca 2008 aliwakuta Valdes, Marquez, Puyol, Iniesta, Xavi, Messi, henry, Abidal, Eto'o, Toure Yaya, Bojan na wengineo katika ubora wao kabisa; akawaongeza Dani Alves, Seydou Keita, Gerald Pique, Busquets, Rodriguez wakiwa katika ubora wao. Hii ikawa dream team. Forward line yake kutokana na mfumo wake iliongozwa na Messi ambaye ni mchezaji bora mara 4 wa dunia akiwa amevunja rekodi karibu zote unazozifahamu. Ameenda Bayern kawakuta wakina Robben, Muller, Ribbery, Schweinsteiger, Neuer, Mandzutic, Dante, Boateng, Alaba na Lahm katika ubora wao kabisa. Kaongeza Gotze na Alcantara, tegemea ushindi tu.
Moyes ameichukua Utd amewakuta Evra (32), Ferdinand (35), Vidic (32), Carrick (32) na Giggs (40). Evans, Smalling, Jones, Cleverly, Young, Valencia, Kagawa, Welbeck Rooney, RvP. Kutokana na na umajeruhi wa Rooney na RvP foward line ya Moyes kwa muda mrefu sasa ni Welbeck akipokezana na Chicharito.
Kwa takwimu hizo hapo juu ndio maana nasema hata Mourinho au Guardiaola akipewa Utd hii hali itakuwa ni ileile Kwani ulishawahi kusikia mmoja wao ametaja jina la Welbeck au Chicharito kuwa anataka saini yake? Na ndivyo hivyo ambavyo Moyes angepewa Chelsea, Barcelona au Bayern angekuwa na uhakika wa kushinda vikombe vyote tu. Suala la ubora wa kocha tuliangalie baada ya kuwa tumempa muda wa kusajili na kukaa na timu yake anayoiamini yeye.