Movie Reviews

ukitaka kulia angalia za kidosi kama VEER ZARA ile muvi inatia huruma hadi kupitiliza
Series za kidos za kiboya sana yani series haziishi halafu story inachanganywa na kila aina ya vikorombwoizo kama mihogo, wali, kachumbari, maembe yani vitu havieleweki inaanza hivi inaenda hivi ili mradi tu.
Kama vipi tazama Chuno ya Kikorea. Ila watu mna machozi nitazame series eti nilie haijawahi tokea
 
Katika maisha yangu huwa nadhani moja ya vitu ninavyopenda ktk ulimwengu wa entertainment upande wa movies n series ni kuangalia zenye maadhi ya kusikitisha na si kusikitisha tu kikawaida ila napenda kuangalia movie/series initoe machozi kweli kweli.

Napenda movie/series za namna hii maana zina mafunzo mengi sana ndani yake ambayo si ya kuigiza ila unaona kbsa hii movie/series akili ilitumika ktk utungaji wa story na ktk story hizo huwa naondokaga na mafunzo makubwa sana ya maisha.

Kwa sasa naangalia drama moja ya korea inaitwa BAD THIEF,GOOD THIEF naenda mwishoni sasa ila kusema ukweli hii movie imeniliza zaidi ya mara 5 yani unaangalia movie inafika mahali unaweka pause kidogo Unalia weeee then ukimaliza unarudi unaendelea iangalia.

sitamani kukosa movie ya kuangalia baada ya hii kuisha naomba yeyote anaejua series/movie yenye mahadhi ya namna hii anisaidie kunipa Jina tu la hiyo movie,namba isiwe movie yenye mabunduki mabunduki.

NOTE: iwe inaliza kweli kweli,sio niishie kusikitika tu na kuwaonea huruma,movie flani ambayo ukiiangalia unaishia tu kushusha machozi na kutafakari maisha yalivyo,binadamu walivyo,nk vitu vya namna hiyo.

Asanteni kwa wote mtakaochukua muda wenu ku comment jina la movie,naweza nisikushukuru kwenye comment ila naomba yeyote ataechuka muda wake kunitajia tu aina hiyo ya movie nimpe Asante na Mungu alie juu akubariki.
Kuna hii ya kusikitisha/ kuhuzunisha ila kuhusu kuweza kukuliza sina hakika- ni ya kituruki kwa tafsiri isiyo rasmi "Miracle in the Cell No. 7 celda"
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Dah nilitaka kukutajia we were soldiers ya Mel Gibson au courage under fire kumbe mtu mwenyewe unalizwa na vitu laini.laini..basi we endelea tu
mkuu ushawahi angalia hiyo Bad Thief Good THIEF?

Hii soldiers na courage under fire zinaliza chief kweliii?
 
Naam.. hadi Father, i will take care for you!! Ila sijui why niliziona za kawaida tu.. lkn kawaida tu watu tunatofautiana kiongozi
acha nizitafute hizi zako mkuu nione kwann umezipaisha kiasi hicho

nisipolia itabd nkutafute unidunde hata makofi ili nilie kwakweli... ...
 
Nani alipata kuielewa hii movie wajomba THE GUEST 2014 binafsi sikuielewa mpaka leo
Inasimulia hadithi ya askari wa USA aliyeitwa David ambaye anatembelea familia ya Peterson bila kutarajia, akijitambulisha kama rafiki wa mtoto wao ambaye alikufa katika vita huko Afghanistan.
Baada ya kukaa nyumbani kwao kwa siku kadhaa, mfululizo wa vifo hutokea, na binti Anna (Monroe) anamhutumu David anahusuka na vifo hivyo.
 
Binafsi Deception ya Leonard Dicaprio inanichanganya sana
Nahisi inaelewaeka ila inahitaji concetration ya hali ya juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom