Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,654
- 2,002
Waungwana naomba anayekumbuka jina la movie hii anikumbushe niitafute. Niliwahi kuiona zamani na ningeipenda kuitafuta ili niipakue kwenye Internet. Baba mmoja baada ya kutalikiana na mkewe, mkewe alitoa tangazo la kuhitaji kuajiri yaya kwa ajili ya kumsaidia kuwatunza watoto wake. Kwa kuwa baba huyo hakupenda watoto wake waje kulelewa na baba wa kambo, aliamua kujifanya mwanamke na akaomba kazi hiyo ili awatunze wanawe. Taratibu watoto walimtambua na hata siku moja mkewe alikuja kumtambua. Napenda sana ujuzi wake wa kuweza kuficha identity yake halisi kwa muda mrefu vile. Anayekumbuka title ya movie ile anisaidie tafadhali!!