Movies tano kali ambazo bado hujazitazama.

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,677
24,741
Itsa WEEKEND. Tuanze nayo hivi basi ...

1BR
-5922686367505171631_120.jpg
Sarah anatafuta makazi mapya hapa jijini Los Angeles lakini kazi hii inakuwa ngumu sana. Kwanini? Pesa ndogo.
Akipata panapofaa, basi kodi ni kubwa, na akipata pa mfuko wake, basi ni pabaya ama kupo mbali na kazi. Yani alimradi tabu.

Lakini mtafutaji hachoki, na kwenye kutafuta huku Sarah anakuja kuipata ngekewa yake kama kuku anavyoparura udongo na kuokota funza.

Anapata apartment kali.

Ni karibu na kazi. Kodi ya kumudu na kama haitoshi, majirani wake ni wema mno. Utake nini tena?

Sarah anajiweka hapa na maisha yake yanaendelea. Kila jirani anatabasamu akimwona. Anamsalimu na wanazungumza kwa furaha.

Lakini asichojua Sarah, hapa anapokaa si makazi ya watu, bali mradi maalum wa kundi linaloitwa CDE properties.

Kundi hili kazi yake ni kuwafuga watu kwenye maeneo yao kisha wanawabadilisha kuwa vile wanavyotaka wao ili kutengeneza kitu kinachoitwa 'perfect community'.

Zoezi hizi linaambatana na mateso, kunyimwa usingizi, kutengwa, vitisho na hata kifo unapoleta ukaidi.
8e24460af700907e81b91f4f575ef014.png
Maskini Sarah, kumbe hakupata makazi rahisi, bali jela rahisi.
Sasa anajifanya anaelewa somo. Sasa anajifanya na yeye anabadilika ili ajipe muda wa kujinusuru na wauaji hawa na pia maadui walojivika ngozi ya majirani.

Lakini kazi hii si nyepesi.

Tembea naye humo.

THE VIGIL
-5927011987982762395_120.jpg
Kisa cha movie hii kimetokana na utamaduni wa kale wa huko Israel. Hapo zamani watu wa huko walikuwa na utaratibu fulani wa mazishi. Mtu akifa, basi muda ule kabla hajazikwa, kuna mtu anayeteuliwa kuutazama na kuuchunga mwili kwa usiku mzima mpaka pakuche.
Kwanini?

Walikuwa wanaamini mtu akifa na akiwa bado hajazikwa, basi nafsi yake huwa inatapatapa huku na kule, hivyo kuna ulazima wa kuwa na mtu karibu usiku mzima kwaajili ya kumpatia kisomo, haswa Zaburi na kitabu cha Ayubu, mpaka pale watakapokuja wahusika wa kumlaza kaburini.
6a8e2bf9249e3f0696136192f747f01c.png
Mtu huyu anaitwa 'shomer', na kwa kawaida anakuwa ni mtu wa karibu na marehemu, na kama hayupo basi anaweza akatumika mtu yoyote kama mbadala.
Hapa sasa ndo' anakuja bwana huyu, kwa jina Yakov. Yeye amekumbwa na mengi yanayomsumbua huko nyuma lakini kwa hivi sasa kinachomsumbua zaidi ni PESA.

Ana shida na kodi, hana hela. Hata pesa za kujinunulia dawa hana.

Linapokuja dili la kuwa 'shomer' wa bwana Litvak ambaye amefariki muda si mrefu, anashindwa kulikataa. Analibeba kama lilivyo ili apate pesa.

Marehemu huyu, bwana Litvak, mtu pekee wa karibu aliyenaye ni mke wake ila ni mgonjwa wa Alzeihmer, hivyo anahitajika mtu timamu wa kumtazama.

Shida inakuja, katika usiku huu mmoja kabla hapajakucha, Yakov anajikuta matatani.
a5c42297c73c97be8bb1e4e970defb39.png
Anaanza kuona vitu vya ajabu.
Usiku huu mmoja unageuka mwaka kwake anapojikuta anapambana na roho inayomuwinda marehemu (Litvak) na mambo yake ya nyuma.

SATAN'S SLAVES
40192ac197e6d3962949cb5bdb5a660d.png
Mwalimu Nyerere aliposema maadui wa taifa ni watatu; umasikini, maradhi na ujinga, hakukosea hata chembe.
Lakini katika maadui hawa, kubwa lao ni UMASKINI. Huyu akifika atamuita maradhi na pia atamwalika ujinga na hautakuwa na chochote cha kufanya.

Umaskini k*manyoko.

Na ukitaka kuona vizuri, basi tazama familia ya binti Rini humu ndani. Anaishi na wazazi wake, bibi na wadogo zake watatu wa kiume kwenye nyumba chakavu, tena pembezoni mwa makaburi.
6d1f1086c280af5664445cc9bdd9b610.png
Mama ni mgonjwa hoi, hajiwezi. Bibi ni mlemavu. Baba ni fukara, hajimudu kitu. Mdogo wao wa mwisho (Ian) hana uwezo wa kuzungumza, yani alimradi tabu.
Si muda mrefu ugonjwa unammaliza mama na hapo ndo' maruweruwe yanaanza kuandama nyumba hii. Nyumba haikaliki.

Ni baadae Rini anakuja kubaini kumbe mama yake hakuwa na uwezo wa kushika mimba hivyo alijiunga na kikundi cha kuabudu shetani, huko akapata watoto wote hawa, watoto wanne.
492350a4a6b27ca5dff01ca2ec8ae376.png
Sasa mama aliyeenda, anarudi kudai watoto wake aende nao kwa bwana 'shetty'. Wa kwanza anayemtaka akiwa ni mtoto Ian.

Alooh!

THE CANAL
images(6).jpg
David ni mkutubi wa filamu ambaye hapa karibuni maisha yake hayako sawa kabisa sababu ya mkewe.
Anahisi mkewe anamcheat na mteja wa kazini kwao (Alex) na hili linamnyima raha.

Isitoshe kule kazini anakumbana na video ya kale inayoonyesha kuwa nyumba anayoishi hivi sasa ni eneo ambalo hapo zamani yalitokea mauaji ya kikatili.

Jambo hili linamfanya ahisi kuna 'roho' ipo nyumbani kwake. Kidogo anamfuatilia mkewe mpaka eneo fulani ambalo kuna mtaro mpana unaopitisha vyombo vya maji (canal), na huko anathibitisha ni kweli mkewe anamcheat na bwana Alex.

Haikupita muda mrefu, mkewe anakuja kupotea. Hajulikani alipo. Anatoa taarifa polisi lakini ajabu kadiri muda unavyosogea polisi wanazidi kuamini kuwa David ndo' kamuua mkewe.

Sasa David anaanza kupambana kwa nguvu zote kuutafuta ushahidi kuwa yeye si muuaji, bali kuna kitu eneo hili, aidha hapa nyumbani ama kule kwenye mtaro mkubwa wa maji, ambacho kinahusika na mauaji haya na mengine mengi yalowahi kutokea huko nyuma.

Mzigo unaitwa the CANAL.

DEVIL
-5922686367505171662_120.jpg
Asubuhi ya mapema, bwana mmoja asiyejulikana, anajirusha toka ghorofa ya thelathini na tano na kufa papo hapo.
Baadae, katika jengo hili, watu watano wanaingia ndani ya lifti moja lakini punde lifti inapata hitilafu na kugoma katikati ya floors mbili, ya juu na chini. Watu wanapanick na kukwazika.

Security, aliyekuwa ndani ya lifti, anawatoa hofu, wasijali, muda si mrefu mambo yatakuwa sawa.

Lakini ni kweli?

Sasa kwasababu ya kisa kile cha mtu kujirusha ghorofani, mpelelezi (Bowden) anafika hapa kufanya uchunguzi wake. So mpelelezi huyu anakutana na kisa hiki cha lifti.

Sasa kwenye macho ya kila mtu, kesi hii ya lifti si kubwa. Ni ‘system’ tu. Lakini anapokufa mmoja baada ya mwingine ndani ya hii lifti ndo' mambo yanageuka na kuonekana si utani.

Anayeua hajulikani ni nani lakini ni bayana yupo humu ndani! Kila taa inapozima, mtu mmoja anakufa.
c38394707c85766cd2308dd29abd5845.png
Sasa mpelelezi anapata kazi mpya. Kazi ya kuwaokoa watu humu ndani kabla hawajaisha, na tena kazi ya kumtambua muuaji ni nani miongoni mwao.

Kula chuma hiko.
 
Watu waongo waongo huwa siwapendi sana..... Wewe ni nani mpaka useme hazipatikani kokote wakati zipo zimejaa tele mtandaoni?

Screenshot_2024-05-17-19-36-51-346_com.android.chrome-edit.jpg


Screenshot_2024-05-17-19-38-19-572_com.android.chrome-edit.jpg

Screenshot_2024-05-17-19-39-00-406_com.android.chrome-edit.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom