sasa tofauti iko wapi baina ya mikataba iliosainiwa na bw. Kerl Peter na mfalme mSoveru tuliosoma kwenye historia? kumbe bado tuko enzi zile zile!!!!!!!!!!!!
Mzee Mtumwitu, Heshima yako mkuu
Inawezekana tofauti ipo. Mfano, mazingira yaliyokuwepo wakati wa mikataba ya wakati ule, yaani baina ya machifu wetu wa makabila na wageni mithili ya akina Karl Peter, yalikuwa tofauti ukilinganisha na mazingira ya mikataba ya miongo ya karibuni inayohusu watawala wa nchi yetu na wageni mithili ya Sinclair.
Mazingira ya mikataba ya zamani yalikuwa na utata kwa maana kuwa, wale walioridhia ile mikataba hawakujua kusoma wala kuandika. Pia, lugha ya mawasiliano ilikuwa ni tatizo, hivyo, matumizi ya alama na ishara yalighubika maafikiano baina ya pande mbili. Tatizo lilijitokeza wakati wa utekelezaji wa yale makubaliano. Matendo ya wageni yalitofautiana na jinsi machifu walivyokuwa wameelewa yale makubaliano. Walipouliza kulikoni? Walionyeshwa makaratasi ya makubaliano yaliyokuwa na madole gumba ya wale machifu. Ndipo machifu walipoanza kungaka kwamba, sivyo walivyoelewa wakati wanatia dole gumba.
Historia inatufundisha kuwa, kizazi kilichofuatia baada ya wale machifu, kilipata bahati ya kuifanyia utafiti mikataba ya zamani na kutambua kuwa ilikuwa ni ya ulaghai. Mzee Mtumwitu, naona the history lessons we recently learned at school is not a distant subject. Remember, Chief Abushiri sold his homeland by signing on a piece of paper whose contents he knew not. We were taught he did not have education. Lest these new species of "Nshomiles who sold everything to South African Companies with their Phds. Yet, I wonder what is left of our country that is genuinely ours.
Umesahau Loliondo where an area about 4666 Km square in Arusha region was reported sold or leased for hunting rights to a foreigner at a fee? Nadhani unamkumbuka fukara mmoja kwa jina la Chavda, ambaye aliwafungulia milango "wawekezaji". Waheshimiwa viongozi wetu waliilazimisha marehemu benki yetu ya NBC imkopeshe Chavda mamilioni ya fedha kwa ajili ya kununua na kufufua mashamba ya Mkonge Tanga. Kipofu aliona mwezi, kwani Chavda ambaye wakati anatia saihi mkataba hakuwa hata na senti moja, aliukwaa utajiri wa haraka kama ule wa mshindi bahati nasibu, alafu akaingia mitini na fedha zetu. Kana kwamba haitoshi, haohao waheshimiwa viongozi wetu, wakaitafutia mkataba NBC na kuibinafsisha kwa kisingizio kuwa ina madeni mengi.
Mikataba ya zamani ilisheheni maajabu ya Mussa. Mikataba ya sasa hivi inajivinjari kwa mbwembwe za filauni. Tunaambiwa vipengele "fulani ndani ya mikataba mfano ya Rada, IPTL, Richmond, ATC, madini, n.k, ndivyo vinavyoliangamiza taifa letu kwa kupitia njia ya mkato. Wanaoweka mikataba kwenye darubini, kwa maana ya kuisoma na kuhakikisha kuwa haina vipengele vya kututia matatani ni wasomi. Kumbuka, ilisisitizwa mashuleni kuwa tunasoma kuhepuka makosa waliyoyafanya akina Abushiri na wenzake. Sasa huu ufilauni unatoka wapi?
Binafsi, naamini yalikuwepo matatizo mawili enzi za machifu yaliyopelekea mikataba ya ulaghai. Moja ni tatizo la shule, ambalo tumejitahidi kulishughulikia. Pili ni tatizo la watu kutokuwa na nguvu, ambalo tulilifumbia macho. Machifu walikuwa na nguvu kuzidi watu waliowaongoza. Jamii haikuwa na nguvu za kusitisha au kurekebisha maamuzi ya machifu. Machifu walikuwa ndio chimbuko la utawala na kila kitu na kila kitu kilichohusu jamii. Walizaliwa kutawala, hivyo, maamuzi yao yalikuwa ya mwisho na wakati mwingi, hayakushirikisha mashauriano ya watu. Kwa kifupi, walikuwa ni miungu watu.
Hivi ndivyo ilivyo sasa hivi. Ingawa watu wamesoma, lakini Raisi wetu wa nchi anazo nguvu kama walizokuwa nazo machifu. Nchi inaongozwa kwa ridhaa yake. Ingawa hakuzaliwa kuongoza, lakini ni kama Mungu mtu. Uamuzi wake katika masuala ya msingi ya nchi ni wa mwisho. Katiba yetu imempa uwezo wa kupinga utashi wa watu anaopashwa kuwatumikia (kitu ambacho ni hatari sana). Katiba yetu imewafanya wabunge (ambao wanapashwa kuwa wawakirishi na watumishi wa wananchi) wasiwe na nguvu za kisheria za kuwatumikia au kuwawakilisha wananchi, badala yake wawe vikaragosi na watumishi wa Raisi.
Sioni sababu ya kungoja vizazi vya mbeleni kuifungua mikataba ya sasa hivi ili kujua hasa nini tatizo la hawa waheshimiwa viongozi wetu. Hii kazi tunaweza kuifanya sisi. Njia ya kwanza kufikia azma au lengo hili ni kuhakikishe kuwa katiba yetu inatambua kwa dhati kuwa watu ndio chimbuko la mamlaka yoyote na si vinginevyo. Iseme hivyo, na imaanishe hivyo. Hatuwezi kuendelea kulipia gharama za kuweka mustakbari wa maisha ya mamilioni ya watu chini ya fadhila za mtu mmoja ambaye ni Raisi wa nchi. Lazima mizengwe iondolewe ndani ya katiba yetu ili wabunge wafanye kazi kwa maslahi ya waajili wao, ambao ni watu wala si vyama vya siasa au Raisi wa nchi. Nasikitika kusema kuwa, sasa hivi wabunge hawana uwezo huo.
Bajameni, we have to empower the people.