mottor and dynamo kwa umeme wa bure

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
hallo people,kwa siku kadhaa sasa nimekua nikiwaza jambo ili niweze kutengeneza umeme bila running costs kubwa,hivi kwa mfano nikawa na motor yangu kubwa inayotumia battery za gari then niiwekee fan-belt,na hiyo fan belt izungushe a bigger dynamo,because ile dynamo itaform umeme,ule umeme wake niugawanye urudi kwenye zile battety za motor ili kuongeza charge,na surplus yake niitumie kwa matumizi yangu binafsi,,,,je hii itafaa kweli?nahitaji maoni yenu kwani ni muhimu sana kwangu,,,,,,ahsanteni
 
wazee,tupeane ma-idea ya kupata cheap energy maana tanesco wanatuua,2nafanya kazi 15 days per month sababu ya mgao wao,na bado we cant mek the ends meet
 
tuliposoma physics kule form 1 walisema
IN A CLOSED SYSTEM, ENERGY CAN NEITHER BE CREATED NOR DESTROYED
hii maana yake ni kuwa huwezi kupata perpetuating machine au machine yenye kujiendesha wenyewe kwa wenyewe huku weye unyonye umeme. lazima upate source ya umeme from outside of your system. hutoweza kupata umeme mkubwa wa kutosha kuicharge battery, utakaotolewa na battery yenyewe. kwa kifupi unaweza kufanya kitu hicho, ila umeme utaoupata hautaweza tena kuicharge battery.
hilo ni jambo rahisi sana kufikirika ila ukija kwenye practice ndio unafeli hapo. wazungu wangelikuwa tayari wameshafanya hayo katika vyanzo vingi.
umeme wao wa upepo wameshindwa kuurecharge kwa kuugawa
solar pannels na systems zake nazo pia wangeli-i-recharge battery kwa power iliyozalishwa.
generators zingepunguza kula mafuta kwa ku create systems ya ku recharge.
ila ndio hivyo. huwezi kukata kipande cha mkate halafu kipande hicho kikawa kikubwa kuliko ule mkate wa asili,
kurecharge maana yake unahitaji power kubwa zaidi kuliko ile source yako.
 
wazee,tupeane ma-idea ya kupata cheap energy maana tanesco wanatuua,2nafanya kazi 15 days per month sababu ya mgao wao,na bado we cant mek the ends meet
dawa ya muuaji na weye uwe muuwaji kuliko yeye. wachakachue tu.
cheap kwa sasa ni solar power au windmill (umeme wa upepo) pekee. maana diesel , na petrol ni expensive.
solar panel zinakuwa ghali kama utanunua ready made, jaribu kuagiza materials za panel and than DIY= do it yourself
kama hutumii umeme wa ampere nyingi hapo ofisini pako, nakushauri tumia power backup system.
 
kwa kukupa moyo, na piece of information , kuna electronics circuit inaitwa power converter. sio power inverter.
inverter inageuza umeme wa dc kuwa ac
converter inageuza volt ndogo iwe kubwa , au umeme mdogo uwe mkubwa.
kama utaipatia vyema itakusaidia ku recharge ila battery life will be significantly shortened.
battery yako itakufa baada ya miezi kidogo kuliko inavyotarajiwa. but you will do it man
 
Nimeipenda topic hii, nimekuwa nikijaribu njia mbali mbali za kupata energy nje ya Taa Nesco. Mwaka jana nilianza kutengeneza biogas kutokana na organic matters( eg animal excretion from cattle,chicken,pig etc) na kuitumia kwa kupikia, kuwasha taa na kuendesha Biogas generator inayotoa 100kW. Kama watanzania tukianza na mpango kama huu nategemea torture tunayoipata kutokana na mgao itapungua sana. Uzoefu unaonyesha asilimia kubwa ya watanzania wanatumia umeme kwa ajili ya taa, pasi na kupikia kidogo ambapo biogas itamudu kabisa, zaidi ya hapo biogas inatunza mazingira badala ya sasa tunachoma mikaa na kuangamiza misitu iliyotunzwa na babu zetu.
 
Idea yako ina violate basic laws of physics, kwa hiyo haiwezekani.
 
Nimeipenda topic hii, nimekuwa nikijaribu njia mbali mbali za kupata energy nje ya Taa Nesco. Mwaka jana nilianza kutengeneza biogas kutokana na organic matters( eg animal excretion from cattle,chicken,pig etc) na kuitumia kwa kupikia, kuwasha taa na kuendesha Biogas generator inayotoa 100kW. Kama watanzania tukianza na mpango kama huu nategemea torture tunayoipata kutokana na mgao itapungua sana. Uzoefu unaonyesha asilimia kubwa ya watanzania wanatumia umeme kwa ajili ya taa, pasi na kupikia kidogo ambapo biogas itamudu kabisa, zaidi ya hapo biogas inatunza mazingira badala ya sasa tunachoma mikaa na kuangamiza misitu iliyotunzwa na babu zetu.

watanzania tulivyo ma chekibob tuavyoogopa kinyesi mhhhh. Tena nadhani execretion product ya binadamu inaweza kutoa energy zaidi hata ile ng'ombe Maana niliwai ona alitumbukia wenye shimo mguuu ulitoka umeungua.

Je mtaalam
  • kuna njia ya kufanya kinyesi cha binadamu kiwe harufu friendly? ili kitumike bila kinyaa.
  • Au nini tufanye binadamu tuone kinyesi chetu kama tunavyoona cha ng'ombe
kenya nasikia kuna maeneo nynya mav*** ikijaa w kuchua mzigo wao ndio wanalipa kulingana na ujazo. vice versa na bongo

teh teh teh
 
Ninachofahamu ukubwa wa biogas plant inakuwa determined na kiasi cha excretion unachoweza ku-replenish kila siku ili ku-maintain gas delivery, sasa binadamu kama familia haiwezi labda kwa wanafunzi, wafungwa au choo cha stend. Kwa China mtindo wa kutapisha vyoo hivi kwa kazi hii ni kawaida sana ingawa hawana mgao wa umeme kama sisi lengo lao ni kupunguza gharama za maisha.
Huu uchekibob wa watanzania utaisha wenyewe muda si mrefu kwa kuwa hata hao waliotutangulia walikuwa machekibob isipokuwa hali ngumu kweli ya maisha ilipowapata uchekibob ukaisha.
 
Mkuu Paje, this is a statement of 'Shirk', think about it.

nimefikiria mpaka basi , sijaona, please nioneshe njia. maana walivyotufutisha ujinga sisi walitwambia kuwa:
Shirk means associating a partner with God. au kwa kikwetu ni ANTAJAL li ILAHI NIDDA FY ULUHIYATIHY
na kwa kishirazi ni : kumfanyia Mungu mshirika katika uungu wake. nayo imegawika sehemu tatu katika dhati yake, sifa zake au majina yake. hawajatufundisha zaidi ya hiyo
 
hallo people,kwa siku kadhaa sasa nimekua nikiwaza jambo ili niweze kutengeneza umeme bila running costs kubwa,hivi kwa mfano nikawa na motor yangu kubwa inayotumia battery za gari then niiwekee fan-belt,na hiyo fan belt izungushe a bigger dynamo,because ile dynamo itaform umeme,ule umeme wake niugawanye urudi kwenye zile battety za motor ili kuongeza charge,na surplus yake niitumie kwa matumizi yangu binafsi,,,,je hii itafaa kweli?nahitaji maoni yenu kwani ni muhimu sana kwangu,,,,,,ahsanteni
Mkuu that is impossible hapo utakuwa unataka kutengeneze perpetual machine (yaani mashine ambayo ikiwashwa haiwezi kuzimika) its impossible to input less energy ili upate energy kubwa (the energy difference must come from somewhere) There are is no such thing as free lunch am afraid na wewe sio wa kwanza kufikiria hivi angalia hapa The Museum of Unworkable Devices
 
Kifupi,., fikiri bwawa la Mtera na Nyumba ya Mungu kwa nini wasingetumia umeme wanaouzalisha kuzungushia hiyo mitambo yao ya kufua umeme na badala yake wana2mia maji kuzungushia hiyo mitambo.,. bado kazi ipo, tuendelee kuumiza kichwa
 
nimefikiria mpaka basi , sijaona, please nioneshe njia. maana walivyotufutisha ujinga sisi walitwambia kuwa:
Shirk means associating a partner with God. au kwa kikwetu ni ANTAJAL li ILAHI NIDDA FY ULUHIYATIHY
na kwa kishirazi ni : kumfanyia Mungu mshirika katika uungu wake. nayo imegawika sehemu tatu katika dhati yake, sifa zake au majina yake. hawajatufundisha zaidi ya hiyo

Mkuu nimekuletea private message regarding this, cause I think it will be inappropriate to discuss shirk here.
 
Je na hii nayofikia mm inawezekana??? Kwamba kazi ya invetor ni kugeuza umeme wa dc kuwa ac sasa basi kama ntatumia invetor kubwa ili niweze kutumia vitu vingi nahitaji betri kubwa, na betri kubwa zina bei kubwa na hata hivyo inahitaji chaji mara kwa mara. KAMA ntatumia kajenerator kadogo ambako kanatumi a lita moja kwa masaa 5 kupeleka katika invetor kubwa wakati huo nitatoa umeme wa dc ktoka katika generator. Haiwezi kifanikiwa kupata umeme wa kutosha kwa gharama nafuu?????
 
hallo people,kwa siku kadhaa sasa nimekua nikiwaza jambo ili niweze kutengeneza umeme bila running costs kubwa,hivi kwa mfano nikawa na motor yangu kubwa inayotumia battery za gari then niiwekee fan-belt,na hiyo fan belt izungushe a bigger dynamo,because ile dynamo itaform umeme,ule umeme wake niugawanye urudi kwenye zile battety za motor ili kuongeza charge,na surplus yake niitumie kwa matumizi yangu binafsi,,,,je hii itafaa kweli?nahitaji maoni yenu kwani ni muhimu sana kwangu,,,,,,ahsanteni

Yaani unachekesha kweli. Huwezi kupata energy from nowhere!!! Sawa sawa na jamaa fulani alisema kwa kuwa bwawa la Mtera limejaa maji na kufurika, kuliko kuacha yamwagike, watumie umeme kuya pump back bwawani. Hivyo bwawa litachelewa kwisha!!! Ambachi hakuelewa ni kuwa atatumia lita 100 za maji ya ziada kwenda downstream kurudisha lita 80 upstream. Net effect kapoteza lita 20 zaidi za maji.
 
Wakuu,chonde,chonde naombeni mnisaidie kwenye hili suala la umeme wa kinyesi cha binadamu.Kwani nimewahi kusikia watu mtaani wanasema huo umeme unawezekana kwa 100% ila tatizo serikali inakataa!
 
kuwezekana inawezekana wala serikali haijakataa; In short ukiwa na any organic matter (iwe mabaki ya mimea au kinyesi chochote) in absence of oxygen kuna bacteria watakibreak down na kutengeneza methane gas..., hii gasi inawaka na ni efficient sana kwa kupia ukitaka tena kuibadilisha kuwa umeme itakuwa inefficient sababu kupata umeme either utumie heat kwa kutengeneza steam ambapo kutakuwa na loss of energy, na kupata hii unaweza hata kutumia pipa na some pipes na kutengeza a biodigester
 
Back
Top Bottom