Yaliyojiri Ukumbi wa Hyatt Regency: Frederick Sumaye atangaza nia kugombea Urais

Status
Not open for further replies.

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,159
9,242
Waziri mkuu mstaafu muda huu anatangaza nia akiwa katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es salaam, huku akiwa na kauli mbiu 'UONGOZI BORA, KOMESHA RUSHWA, JENGA UCHUMI'. Anasema huwezi kukemea rushwa na halafu na wewe upo ndani ya rushwa.

============
Sumaye.jpg
Anaongelea mafanikio katika katika kipindi yuko madarakani ikiwemo televisheni ya taifa, uboreshaji elimu ya msingi. Anasema leo badala ya sekondari nayo kupanda ndio hio imeshuka.

Anaongelea sera ya ubinafsishaji, anasema sera hio ilikuwepo kabla ya uongozi wa Mkapa. Hivyo wao walikuwa watekelezaji na hawawezi kulaumiwa. Ubinafsishaji kama sera ni kitu muhimu na ni vizuri ilifanyika. Mashirika zaidi ya asilimia 45 yamenunuliwa na watanzania, mengine kwa ubia na wageni na asilimia ishirini pekee yalinunuliwa na wageni kwa asilimia 100.

Nimekumbana na mambo magumu katika miaka hio kumi ikiwemo ajali ya MV Bukoba na ajali ya treni, ukame wa mwaka 1997. Niliunda kamati ya kushughulikia jambo hilo na kuchimba visima zaidi ya 300 Dar es Salaam. Mambo magumu yalinikomaza katika uongozi. Mvua za El nino zilifata baada ya ukame, ilikuwa hali ya hatari lakini tulijikwamua na tuliendelea na kazi wa kujenga taifa letu. Kifo cha baba wa taifa, mimi sikulala siku tatu nzima hata kwa nusu saa, sijawahi kuona kipindi cha amani kama kili, polisi waliripoti hata uhalifu haukuwepo.

Wakati waziri mkuu, sikuweza kusikia watu wanapigana, asubuhi nisiwepo pale, leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita sasa. Mfano mgogoro wa waancholi na wahadzabe.

Huwezi kuzungumzia amani wakati watu wana njaa, tatizo la uchumi, watu wanaangalia takwimu badala ya uhalisia. Tunatakiwa tuendeleze kilimo, hata wakati wa Nyerere tulileta matrekta lakini tuliendelea? Kuleta matrekta ni jambo jema sasa nitalima heka 50, lakini uwezo wa mbegu heka 3 na kupalilia heka 3.

Eneo lingine muhimu ni masoko, lazima kiendelezwe katika ukubwa wake. Wakulima watauza kwa bei ya hasara na bei ikiwa vizuri hawana tena mazao. Leo viwanda vya sukari, hatuwezi kuingiza sukari kutoka nje bila kodi, lazima tulinde viwanda vyetu vya ndani. Mazao yetu yote, kama tutakua na juhudi za kusindika mazao, hili tatizo la ajira ambalo tunapiga nalo kelele sana, litapungua. Pia pengo kati ya walionacho na wasio nacho litapungua.

Nimeona shule binafsi wanafanya vizuri, wanataka wazipunguze nguvu, ongeza juhudi nawe umfikie. Katika miaka miwili au mitatu tutapunguza kwa kiasi kikubwa wanaoenda nje.

Rushwa na ufisadi, hili jambo sina utani nalo. Ukituhumiwa kwa rushwa ndani ya wiki moja unachunguzwa na wiki mbili mahakama imekuhukumu na kama ni viboko unapokea kabisa.

Nawashukuru ndugu zangu waandishi wa habari, nimezungumzia Dar es Salaam na naamini mtafikisha nchi nzima ili tumpokee rais Kikwete kijiti ambae amefanya vizuri. Kama kuna maswali pia niko tayari.

Matangazo haya yalikuwa yanarushwa na ITV, Star TV, Mlimani TV, Radio free Africa, radio one ila bahati mbaya sehemu kubwa ya nchi umeme hamna ikiwemo mikoa mitano
=========
MASWALI
Tanzania Daima: Katika awamu hio ufisadi mwingi ulitokea, uuzwaji NBC, EPA, Radar Kiwira Kama mshauri mkuu wa rais na mtendaji

Mwananchi: Umenukuliwa mara kwa mara kuwa ikitokea ameteuliwa mla rushwa kupitia CCM wewe utajitoa

Mariam Mziwanda, gazeti la Uhuru: Kabla hujaachia uongozi wa uwaziri mkuu ulitajwa kama kiongozi unaemiliki mali nyingi, kupitia fursa hii

MAJIBU


Swali la Kwanza
Kwanza kama waziri mkuu naweza kumshauri wa rais, Ameziita kashfa lakini mimi siziiti kashfa. Kama NBC ni ubinafsishaji wa kawaida. Sijui watu wanatoa wapi taarifa kuwa walikuwa wanapata faida, regulator wa benki zote ni BOT hivyo ndio ana taarifa sahihi. Hakuna kwamba tuliuziana benki hotelini Hizo zingine zote zinafanana, Radar na ndege ya rais, unatakiwa utofautishe maamuzi ya serikali na kama kuna ufisadi, nchi ilikuwa haina radar. Katika ununuzi ule kama kuna mtu alifanya foul anatakiwa akamatwe, ilimradi imethibitika mtu alifanya ovyo ni jukumu la serikali kumkamata sio Sumaye,

Swali la michezo ni muhimu ni ukosefu wa muda ndio maana sikuigusa ila katika kitabu changu cha sasa mtaiona.

Mimi na wala rushwa ni maji na mafuta, nitatoka ndio lakini naamini chama changu hakiwezi kuchagua mla rushwa. Sitegemei kutoka kwa sababu hawatachagua mla rushwa.

Sasa Mariam, muda unatoa jawabu, mimi leo watanzania wananijua, watoto wangu mnawajua wanafanya kazi za kawaida za serikali. Mtikila ambae alinituhumu mambo mengi sana, baadae akasema watu wasafi nchi hii ni Sumaye, Warioba na Mwakyembe. Hela nyingine ambayo nilipata nilisomesha waandishi wa habari nyie mnajua. Mimi nina moral authority kwa muda mrefu.

Kuhusu nani tishio katika mbio za urais, hakuna hata mmoja.

MASWALI
Pendo: Katiba mpya kuna mkwamo, ukipata ridhaa unawaahidi nini wananchi ambao maoni yao yametupwa

Mtanzania: Uumekua unaongelea umiliki wa ardhi bila faida, wewe unatuhumiwa kumiliki maeneo makubwa na mengine hayajaendelezwa

Radio Iman: Umezungumzia vipaumbele vingi, walimu wana kilio cha muda mrefu tangu wewe ukiwa madarakani kuhusu stahiki zao

Kubenea: Nyumba za serikali ziliuzwa wakati uko madarakani, tamko lako!

Mimi sidhani tatizo ni katiba, tatizo ni usimamizi wa sheria, kwa mfano kiongozi mla rushwa, katiba haikupi fursa ya kumuhukumu? Tatizo sio katiba, hatuhitaji li-document likubwa kama tuliloliandika.

Swala la ardhi, wapo watanzania wengi tu wana ardhi kubwa kuliko mimi, haya mambo yanakuzwa tu, nimeshindwa kuendeleza baadhi ya maeneo kwa sababu sijapewa hati bado. Hela ya kujenga kibanda Dar unaweza kununua ardhi kubwa sana mikoani.

Swala la kuboresha walimu, tulifanya hayo na msiwe na wasiwasi nalo kwa upande wa mafao.

Nyumba za serikali ni uamuzi wa serikali, sababu yake kubwa ilikuwa ni nini, kwa sababu ungozi wa Mkapa ulikuwa ni uwazi na ukweli. Kamati ilisema nyumba za serikali ni nyingi mno hivyo pesa nyingi zinaingia kuzikarabati. Tulikua kwenye ubinafsishaji, mashirika yalikuwa na nyumba nyingi, nyumba nyingi tuliamua kuziondoa. The highest bid secured, tulijaribu kutetea hata ma-general managers lakini ilishindikana.

Rushwa ni rushwa, mtu hata uwe mkubwa namna gani, yani mnipe Urais nimshindwe, hakuna mkubwa kuliko Rais, wote nitawashughulikia.

HOTUBA YOTE YA MHESHIMIWA SUMAYE AKITANGAZA NIA KILIMANJARO HOTELI, MASWALI NA MAJIBU YAKE KWA WANAHABARI. JUNE 2, 2015.

UTANGULIZI.

Nimetangaza nia hapa Dar es salaam sio kwasababu sina kwetu, ni kwasasababu nafasi ninayoitafuta ni ya kuongoza watanzania wote.

Nimejiandaa kupokea kijiti kutoka kwa Rais Kikwete mnamo mwezi October iwapo chama changu kitaridhia, kwa kuwa nafasi ya Urais ni nafasi kubwa hatuhitaji kukimbizwa au kuswagwa kama mbuzi.

Mtu anayetaka nafasi ya Urais lazima ajipime, ajitafakari kwamba anatosha katika mambo yafuatayo.
Kiafya, kiakili, kimaadili na kifhamira na lazima asipungukiwe hata moja kati ya hayo na mtaka Urais yeyote lazima awe tayari Umma umpime katika hayo.

Watanzania wanataka Rais Mtiifu na Mwaminifu, anayefikiri na kushaurika na atakayetuwekea maslahi ya taifa mbele na sio maslahi yake binafsi.
Tunataka Rais mwenye uwezo wa kusimamia uchumi na kuondoka matabaka na pengo kati ya walionacho na wasio nacho.

Tumekuwa na malalamiko mengi juu ya sekta ya elimu, tunataka Rais ajaye ashughulikie suala hili na sio kushusha alama za ufaulu ili wanafunzi wengi waonekane wamefaulu.

Nimesikia wagombea wenzangu wakizungumza kuhusu rushwa, lakini kama upo serikalini na kuna rushwa kwanini hawaelezi wamepigana nayo kiasi gani?

Tunashuhudia watawanya rushwa na fedha wakisema eti watakomesha rushwa kwa kisingizio cha kupewa na rafiki zao lakini tujiulize nani anaweza kutoa fedha bila kujua atazirudishaje?

Nimeshangaa sana mtu anasema eti hatutaki kiongozi masikini yaani unashindwa kusema tu "tunataka Rais tajiri" hii ni hatari sana mtu anayesema yeye si tajiri na hataki Rais awe masikini.

Mimi nimejipima, nimetafakari na nimejiridhisha kuwa natosha, bahati nzuri watanzania wananijua na sifa ambazo watanzania wanazihitaji kwa Rais wao mimi ninajitosheleza.

Nilikuwa mbunge tokea 1985, nimekuwa Naibu waziri, nimekua waziri na nimekuwa waziri mkuu kwa miaka 10 kama ni jeshini tunasema mimi nimepanda kwa ranks and files na kama kuna mtu mwingine kati ya waliojitokeza ananizidi kwa hizo sifa nipo tayari kumpisha(anashangiliwa)...

Mimi si mpenda vyeo, Rais aliponiita na kuniambia nimekuteua kuwa waziri mkuu nilikataa nikamwambia naomba uteue mtu mwingine, Rais akakataa, hii inakuonyesha mimi si mpenda vyeo.

Ni mimi niliyekuwa kinara wa utekelezwaji wa mambo yote makubwa yaliyofanywa na awamu yetu ya tatu.
tulikuza uchumi na kuondoa inflation kutoka asilimia 27 mpaka asilimia 4, ndio maana hakuna mfumuko wa bei uliotokea.

Mapato ya serikali ilikuwa bil.27 lakini ilipanda mpaka bil. 280
Mishahara ilikuwa kima cha chini 17 elfu lakini tulipambana na kuondoa suala hilo.
Tulipambana na kuhakikisha madeni yote sugu yanakomeshwa.

Umeme unakata, watu wanatania na kusema ni richmond hiyo.

Tulisimamia uchumi seriously mpaka tukapata msamaha wa madeni kutokana na appreciation tulivyokuwa tukikuza uchumi.

Tuliunda tume ya Warioba ipambane na rushwa.
tulianzisha kura ya maoni kwa wala rushwa ili wananchi wakapige na kuwataja wala rushwa kisha ambaye jina linatokea mara nyingi PCCB.

Mhe. Sumaye anataja idadi ya waliofukuzwa, na kusimamishwa kazi kutokana na rushwa, wengine wanasema tu lakini hawasemi waliikabili vipi rushwa.

Nilifanya maamuzi bila uoga, nilivunja halmashauri ya jiji la Dar es salaam na kuliboresha jiji kwa kiasi chake. Nilipandisha mapato ya jiji kutoka milioni 800 mpaka bilioni 800 mpaka 900.

Inshalah nikijaliwa kuwa Rais majiji yetu yataboreshwa zaidi.
Wakati tunaingia watoto wrngi walikuwa wakikaa chini lakini tuliongeza madawati kwa kasi sana mpaka tukafikia kipindi tukawa na akiba.

Leo hii tuna televisheni ya taifa kwa kuwa nilisimamia ikapatikana ambapo kwa miaka yote ilishindikana.

Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, watu wanatuhumu eti tuliuza mashirika ya umma.
Kwanza sera ya ubinafsishaji iliundwa kabla ya Mkapa kuingia madarakani na sisi tulisimamia sera ya chama leo hii eti tunalaumiwa.
Wafanyakazi wa mashirika ya umma hawakulipwa mpaka mwaka mzima kwa kuwa viwanda na mashirika yalikuwa hayapati faida zaidi ya hasara.

timu ya wataalamu(si wanasiasa) iliendesha mchakato wa ubinafsishaji na ni asilimia 20 tu ya mashirika yaliyonuniliwa na wageni, mengi yalinunuliwa na Watanzania.
Ubinafsishaji upo hata marekani, ndio maana kampuni kama General Motors imenunuliwa na wageni kutoka China na maeneo mengine.

Nimekumbana na mambo magumu kwa miaka kumi, ikiwemo ukame wa 1997 ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania mto Ruvu uliacha kupeleka hata tone moja baharini, tulipambana kwa kuchimba visima zaidi ya 300 Dar ndio watu wa Dar wakaweza kujisitiri.
Mvua za elninho pia zilitutikisa sana, reli nyingi ziling'olewa lakini tulipambana na kutumia hata wanajeshi wetu kuzijenga upya.

Leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita, serikali ipo wapi?
Nilifika kuamulia ugomvi wa makabila Tarime na nilishuka na helicopter katikati ya mapambano huku kila upande ukiwa umeshika silaha.

"Mimi nasema, kama kuna mtu amepikika kuliko mimi aseme, nimpishe. Na kama ni Afya ninayo.

NITAFANYA NINI NIKIWA RAIS?

Kwangu, Suala la uchumi ndio litakuwa la kwanza.
Huwezi kuboresha elimu, Afya, wala amani bila nchi kuwa na uchumi imara.

Tatizo la uchumi wetu tunaangalia takwimu badala ya uhalisia. Nitqshughulikia na kuwekeza katika kilimo, sipingi.kuwa na matrekta lakini hata kipindi cha Mwalimu yalikuwemo lakini hayakusaidia kukuza kilimo.

Leo tunasikia wakulima wanauza mazao yao kwa bei ya kutupa kwahiyo lazima tuwatafutie soko la uhakika.

Lazima tuimarishe viwanda vyetu na kuvilinda viwanda vyetu vya ndani.
Kuna viwanda vinauza nguo nzuri kabisa lakini tunaingiza kutoka nje tena bila kuchukua kodi. Hili ni lazima zikome.

Mimi kipaumbele changu kitakuwa ni uchumi na kupitia ukuaji wa kilimo mambo mengi yataimarika.

Nitaboresha huduma za jamii(afya na elimu).
Nitarudisha shule za vipaji maalumu ili vijana wenye uwezo mzuri kutoka shule za serikali, sasa hv shule zinazofanya vizuri za binafsi zinataka kupunguzwa nguvu.

Nitapunguza idadi ya robo tatu ya wanaoenda kutibiwa nje kwa kuboresha hospitali zetu.

Jambo lingine ninaloahidi ni kupambana na maovu ikiwemo rushwa. Mimi ni "zero tolerance katika rushwa na nina moral authority.
Nitaunda vyombo vya uchunguzi lakini pia nitaanzisha mahakama maalumu ya kushughikia masuala haya na hakika sitamuangalia mtu usoni wala cheo chake.

Mwisho, nasema "komesha rushwa, jenga uchumi na huu ndio motto(kauli mbiu) yangu.

Waandishi wa habari sambazeni taarifa hizi na watanzania watupime kwa uwezo wetu wa kujenga hoja na kutatua matatizo yao.
Ahsanteni.

Anaruhusu maswali kama yapo.

MC anasema maeneo mengi ya nchi hii umeme umekatwa.

Ibrahim Yamola Tanzania Daima anauliza. "Katika awamu uliyoongoza ziliibuka kashifa kama Meremeta, uuzwaji.wa NBC, Rada na uuzwaji wa mgodi wa Kiwira haya yalikushindaje?

Mwandishi wa mwananchi anauliza
1."umekuwa ukinukuliwa kuwa CCM ikipitisha mla rushwa utajitoa, jee watanzania wategemee kukuona nje ya CCM?.

Mariam Mziwanda wa Uhuru anauliza.
"Eleza mali unazomiliki ili watanzania wajue na pia tuambie nani anakupa homa miongoni mwa wagombea unaogombea nao.

SUMAYE ANAANZA KUJIBU.
1. Kuhusu kashfa zilizojitokeza, kwanza niseme ni kweli mimi nilikuwa mshauri wa Rais.
kuna vitu vimeitwa kashfa lakin mimi sioni kama kashfa mfano, NBC si kashfa, hii benki haikua ikitoa kodi yoyote hazina, gavana wa benki alitoa tahadhari kuwa kwa madeni ya NBC ukipanga noti za elfu kumi zinazidi urefu wa mlima Kilimanjaro.
Ubinafsishwaji wake ulitangazwa lakini pia haikuuzwa yote na ndio iliyozaa NMB ya leo.

Hakuna mwehu aliyekaa na mwenzake wakauzina NBC hotelini. Hakuna.

Zingine zote zinafanana. Rada, ndege ya Rais na mengineyo.

Nchi ilikuwa haikuwa na rada, Museveni alitaka kugongana na ndege zingine na kuna mashirika makubwa yalitaka kuondoa ndege zao Tanzania kwa kuwa ndege zilikuwa zikitazamwa kwa macho
Kama kuna mtu alifanya wizi na tulipotoka ndio wamebainika washughulikiwe.
Kiwira ilikuwa hivyo hivyo, bahati mbaya Mkapa akaingia na akatoka baada ya siku tatu.

Pili. Sitaungana na wala rushwa, nitatoka ndani ya CCM kama CCM watapitisha mla rushwa na siamini kama chama hiki kitachagua mla rushwa.
Sijajiandaa kutoka lakini iwapo watapitisha mla rushwa nitatoka kwa kuwa siwezi kuungana na wala rushwa.

Tatu, ninatajwa kuwa tajiri. muda unatoa jawabu, tujiulize hivi huo utajiri nilionao nataka kwenda kuulia mbinguni.

Mnakumbuka Mtikila alinitukana lakini akaja akasema watu wasafi nchi hii ni Sumaye, Warioba na Mwakyembe.
Walionituhumu nilipomaliza uongozi niliwaburuza kortini na nikashinda na fedha nilizopata kama fidia nilisomesha nyie wana habari.

"Hivi ningekuwa mla rushwa ningejitokezaje kuikemea rushwa?"

Kwa waliojitokeza sasa hivi hakuna hata mmoja ambaye ni tishio kwangu.

MASWALI YANARUHUSIWA TENA.

Pendo Omari(mwananchi online).
Tumekwama kwenye mchakato wa katiba, unawaahidi nini wananchi ambao maoni yao yaliyotupwa?

Mwandishi wa Mtanzania anauliza. "inasemekana unamiliki ardhi kubwa, hili lipoje?

Saed Kubenea anauliza.
"Ukiwa serikali ndio nyumba za serikali ziliuzwa, unasemaje kuhusu hili?

ANAJIBU.
Kuhusu katiba mpya. Tangu mchakato unaanza nilisema usimamizi ni muhimu kuliko hata katiba kwasababu hata ikiwa nzuri wasipokuwepo wasimamizi wazuri mambo yatakwenda hovyo.

Suala la Ardhi, wapo watanzania wengi tu wenye ardhi kubwal kuliko mimi.

Gazeti liliandika nina ardhi kubwa na siliendelezi, sikuiendeleza kwa kuwa bado sijapatiwa hati.

Sisi wengine tumejikita kwenye kilimo hatutakiwi kuandamwa, tunafanya kile tunachokihubiri ili tuone na tu experience adha wanazokumbana nazo wananchi.

Kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali, Rais alishauri na cabinet na akakubali.

Kuna tume tatu zilifanyia kazi suala hili kwa muda tofauti na zote zilikuja na mapendekezo kuwa nyumba za serikali ni nyingi na serikali inagharamia fedha nyingi kuzikarabati na hivyo tuwauzie watumishi wa Umma.

Tulikuwa na nyumba nyingi mfano Breweries na bandari walikuwa na nyumba zaidi ya elfu moja.

Nyumba nyingi zilinunuliwa mpaka na wananchi wa kawaida, Rais alishituka kuona ghorofa zinainuka Oysterbay zilipokuwepo nyumba za serikali.
Rais akasema lazima paper iandikwe wauziwe wafanyakazi waliokuwa wakiishi humo na hakuna kuuzwa mpaka baada ya miaka 25, na gvt valuer akafanya tathimini na watumishi wa serikali wadogo kabisa wakauziwa.

Kuhusu kupambana na rushwa kubwa.
Hakuna rushwa amabyo ni kubwa kuliko Rais, huwezi ukapewa Urais alaf ukasema kuna rushwa kubwa.
nyie nipeni Urais alaf mtaona ninavyowashughulikia wala rushwa.

Mhe. Fredrick Sumaye amemaliza na shughuli imeisha.
 
Last edited by a moderator:
Waziri mkuu mstaafu ndugu Frederick Sumaye yupo live sasa hivi ITV akitangaza nia ya kugombea uraisi kwa tiketi ya ccm. ITV na radio one wapo Live.
 
Sumaye: wagombea urais wawe tayari kupimwa na umma hadharani kama wanaweza kumudu nafasi ya urais.
 
Ameongea mambo mengi sasa anasema kile kilicho msukuma kugombea urais.

Kwanza anasema amejipima na kuona unaweza kuwatumikia watanzania.

Anasema yeye ndio anashika rekodi ya kuwa waziri mkuu kwa miaka 10, na kama kuna MTU anamzidi yupo tayari kumwachia
 
Nimejaribu wasikiliza watangaza nia ya kwenda magogoni, mpaka huyu ambae yuko kilimanjaro hotel leo sasa hivi, ndio wanatangaza sera wengine naona kabisa kuwa na dhamira ya dhati kututoa hapa tulipo, namimi nasema vizuri sana.

Ila nasikitishwa sana na tabia ya kupigana vijembe , cha kushangaza wanampiga mwenzao mmoja ambaye ameonekana kuwa na ushawishi mkubwa ingawa si rahisi kuteuliwa katika chama chake kwa jinsi tu picha inavyooenda mpaka sasa. Lakini mimi ningemshauri

"Angesoma alama za nyakati fasta" kwani pale si rahisi kupenya kama kweli anataka urais.
 
Wamekata umeme mwanza mjini
Nilikuwa namsikiliza mzee akitiririka siri za serekali


Kumbe huwa wanajua maisha ni magumu na vitu vinavyopanda bei ila ukishawapa tu wanaanza safari za ulaya
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom