umeme wa bei rahisi

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
hallo people,kwa siku kadhaa sasa nimekua nikiwaza jambo ili niweze kutengeneza umeme bila running costs kubwa,hivi kwa mfano nikawa na motor yangu kubwa inayotumia battery za gari then niiwekee fan-belt,na hiyo fan belt izungushe a bigger dynamo,because ile dynamo itaform umeme,ule umeme wake niugawanye urudi kwenye zile battety za motor ili kuongeza charge,na surplus yake niitumie kwa matumizi yangu binafsi,,,,je hii itafaa kweli?nahitaji maoni yenu kwani ni muhimu sana kwangu,,,,,,ahsanteni
 
Nenda Ubungo external wapo jamaa wanatengeneza wind mill zinazozungusha mota, inafua umeme hadi wa kupikia.
 
hallo people,kwa siku kadhaa sasa nimekua nikiwaza jambo ili niweze kutengeneza umeme bila running costs kubwa,hivi kwa mfano nikawa na motor yangu kubwa inayotumia battery za gari then niiwekee fan-belt,na hiyo fan belt izungushe a bigger dynamo,because ile dynamo itaform umeme,ule umeme wake niugawanye urudi kwenye zile battety za motor ili kuongeza charge,na surplus yake niitumie kwa matumizi yangu binafsi,,,,je hii itafaa kweli?nahitaji maoni yenu kwani ni muhimu sana kwangu,,,,,,ahsanteni

Kwa kifupi tu ni kwamba hilo halitafanikiwa au niseme haliwezekani. Kulingana na laws of energy kama umesoma physics, huwezi kupata 'energy' (nguvu) kubwa kutoka kwenye nguvu ndogo zaidi. mzigo wa kilo 1 hauwezi kunyayua mzigo wa kilo 2. Mambo haya kwa urahisi ni sawa na kusema maji hayawezi kupanda kilimani, labda kuwe na force kubwa itakayosukuma maji ndipo yapande. Hiyo mota yako kama inatoa umeme wa kVa 5 utazungusha dynamo ya kva 5 na dynamo hii haitaweza kutoa umeme wa kva 5! Lazima utakuwa pungufu labda kva 3.5 kwasababu kuna kiasi cha nguvu kinapotea kama msuguano, joto, na sauti na hizi zote ni aina za nguvu (forms of energy). Ingelikuwa inawezekana kusingelikuwa na tatizo la ememe duniani!

Kwa kifupi uwezi kupata kitu kutoka si kitu.
 
At last someone is thinking in this blog! Usisikilize wapumbavu wanaokatisha tamaa, jaribu na jaribu tena, cha muhimu kila unapojaribu baada ya matokeo fikiria umejifunza nini na utafanya nini kuboresha ulichokifanya. Tanzania inahitaji watu kama wewe, watu wanaofikiria namna ya kuboresha mazingira sio tu watu wanaofikiria mapenzi na siasa. aliyegundua umeme alijaribu 10,000 times kabla hajapata umeme tunaotumia leo, angesikiliza mijinga miataisha tamaa, tungekuwa wapi? au angeka tamaa kaika jaribio la 2,000 tungekuwa wapi? Watanzania its time to star thinking differently!
 
duh! Brilliant idea, but as one said above the very basic principle of energy translated in a simple and commoner language is "you can't get something out of nothing" but keep trying....unaweza kuvumbua mengine
 
Mkuu wazo lako ni zuri!!

Halihitaji kuuliza hapa jamvini vinginevyo tutakukatisha tamaa mpaka uchanganyikiwe. Si unaona jamaa wameshaanza na kukuuliza unasoma wapi? Na Kozi gani?

Kama umepata wazo anza kufanya utafiti wako kimya kimya!! Mfano unaanza na battery 1, 2, n.k Mpaka mwisho wa siku utakuwa umepata jibu sahihi kuhusu huo utafiti wako na baadae unatuwekea hapa jamvini nini kimetokea.

Lakini ukikalia ushauri wa hapa jamvini kama wazo linawezekana au la? Hautapata jibu sahihi!!!

Nakutakia mafanikio.
 
science ni Dynamics na watu wanaweza kukukatisha tamaa kwa sababu walikaririshwa mavyuoni, science ni practicals na mwisho unakuja na kitu timilifu, kuna vitu vingi tulivyosoma kwenye science miakaya nyuma ambavyo vilikuwa haviwezekani lakini kwa sasa vina wezekana kutokana na watu kufikiria na kujaribu
Tukitoa umeme wa Solar, vyanzo vingi vya umeme ni rotation+-coil na sumaku, kama una dyanamo ambayo inaweza kuzalisha umeme, hapo kinachokosekana ni mzunguko tu, sasa mzunguko unaweza kuwa wa maji, upepo ama huo unaofikiria wa engine ndogo. ni kweli unaweza kupata umeme mdogo, lakini unaweza kuongeza na tranfoma ya kukuza umeme,

Hii kitu inawezekana na itakuwa nzuri zaidi kama ukifanya system ya kuweka na ototena kwa kuchajia battery

Chukua mfano wa betri ya gari ya 24volt ambayo inaweza kuwasha taa zaidi ya kumi za gari,inapiga mziki na inaweza kungurumisha coldroom(kwa magari yenye freezer)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom