Motor ya 3 phase

Motor ya 3 phase

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
26,597
Reaction score
29,528
Hivi nikichukua motor ya 3 phase niakaiweka sehemu alafu umeme huu wa 2 phase yakawaida kwenye ile L(live) nikakata vipande 3 vyenye urefu wa mita moja moja nikavichuna kidogo huku na huku alafu zile ncha 3 za upande mmoja wa hizo waya nikaziunga pamoja alafu niunganishe kwenye ile L (live) alafu hizi ncha nyingine nizilishe kila ncha kwenye live zote za ile motor alafu N (neutral) niinganishe kama kawaida kwenye motor.

Swali hapa: Je, nikienda kuwasha hii motor itawaka? Na je, isipowaka ni kwanini wakati nimeilisha moto kama inavyotakiwa?

Karibuni mnifundishe.
 
Mbona naona tu phase moja hapo hiyo ya pili ipo wapi, hata hivyo motor haitofanya kazi maana imetengenezwa ipate three phase.
 
HAITAWAKA,

ukisema '3 phase', ina maana una L1 na L2 na L3 zote zikipishana kwa electrical angle (phase shift/angle) ya 120 deg

ambayo ina maana, L1 ikiwa peak, L2 ipo somewhere katikati na L3 ipo chini au somewhere chini, hapo ndio utapata mzunguko

ulichofanya wewe ni kwamba una L1,L2 na L3 ambazo zina phase angle ya 0 deg , maana ni waya uleule umeugawa mara 3,

by the way, bado kuna 3phase motor ambayo inatumia neutral ?

most 3phase motors ( kama sio zote ) ziko 'balanced' , hakuna haja ya neutral, maana itabeba 0A
 
Kwa kumsaidia ni kuwa iyo mizunguko 3 inatengeneza zaidi ya volt 400 wakati single phase inatengeneza mwisho volt 240
 
Kuna namna ya ku loop ila capacitor itaitajika,check na fundi wa motor rewinding au mtandaoni utapata maelekezo lakini itategemea na HP ya motor ili iweze ku maintain RPM yake katika single phase.
 
Labda utumie capacitors kutengeneza phase angles tatu tofauti japokuwa motor inaweza isiwe na nguvu ya kutosha!
 
Hio kitu haitawezekana Kwasababu ili motor izunguke inahitaji mpishano wa angle Three phase kila line inasoma 120 na kwa vile zipo tatu zina form 360 sasa huu mpishano ndo unaanzisha rotation na ndio mana tunasema Three phase ni Self starting kwa single phase inahitajika Mechanicsm nyingine kuswitch kama capacitor au split phase ila kama una motor ya 3 phase na unataka ui operate katika Single phase unaweza add capacitor ila tu pia HP ya motor itakuwa reduced
 
3 phase volts ni 380/400v,2phase volts ni 380/400v,wewe una 1phase ambayo ni 220/240volts,experiment za umeme haziendi kienyeji hivyo,kama za useremala au ujenzi wa tofali,utapoteza maisha,kasomee kwanza..
 
Back
Top Bottom