Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Status
Not open for further replies.
Mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto ni muhimu sana kutolewa kwa wanausalama. Moto wa PPF Tower ulikuwa unazimika kwa kutumia mitungi ya kuzimia moto tu!...
 
Unajua gari moja la zimamoto ni shillingi ngapi?na wao wamusanya mpaka sasa hivi shillingi ngapi?acha kuongea pumba ili na wewe uonekane umechangia hoja
 
fire safety ni darasa pekee
sijui kama kuna jumba hapa nyumbani lililonalo fire pump na sprinkler system au kwenye Data room kuwa na FM 200 kunapotokea majanga ya moto,
Hivi vitu ni vya lazima kwenye maofisi yote sasa sijui wanaoekeza mabilioni kwenye majumba makubwa kama haya bila ya kuekeza hela ya usalama wa mali.
Hata watu wa Bima wanatakiwa wasikubali kutoa bima bila ya kueko usalama wa kutosha
 
acha liungue tujenge christapen tower tehetehetehe......||||||||||||||
 
kama sikosei gari la zima moto lililokamilika gharama yake haipungui $ milioni moja kuendea juu.

Nasema tena lililotimia na jipya
Unajua gari moja la zimamoto ni shillingi ngapi?na wao wamusanya mpaka sasa hivi shillingi ngapi?acha kuongea pumba ili na wewe uonekane umechangia hoja
 
Wajanja washaiba sasa kazi ni moja tu, kupoteza kumbukumbu.
.
 
Iliungua WTC
unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af
utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au
kule hakuna umeme

umesahau tu. makazi ya rais wakati huo mkapa yaliwahi kuteketea kwa moto ulioanzia kwenye pasi ya umeme iliyoachwa ikiwaka.
 
Hawakulipia sticker za zimamoto ndio maana moto umetokea....lol!!
 
Huu moto mi naona ni watu wanatengeneza madili wapige hela.
 
Nyaraka mhimu zitakuwa zimechomwa kwa manufaa ya makupe machache.

Mkuu kwa haraka na kuangalia hizo picha, naona moto umewaka juu kabisa ya jengo zilipofungwa BTS za makampuni ya simu ambazo kimfumo huwa zinakuwa na mfumo wa umeme...
 
Duh mpaka ATM zimegoma kufanya kazi kuuliza tukaambiwa mitambo imeungua ipo PPf Tower hii ni hatari nchi inaweza kusimama pakiungua sehemu nyeti majengo marefu hakuna fire fighter na vifaa vya uhakika
 
Wale wote mlio na mtazamo tofauti juu ya ajari hii ya moto. Je ajari hii ingetokea majumbani mwenu mngesema nini? Ajari kama ajari ipo tu! Na haitabiliki.
 
Kufika sio, tatizo ni maeneo mangapi wanafika na kushindwa kufanya kazi yao kikamilifu, kwa madai ya upungufu wa vifaa, kuna kipindi zima moto zinafika maeneo ya tukio na hazifanyi zilichokipekeleka eneo husika na wakawa kama hawajafika tu na ili ushahidi upo maeneo mengi yamekumbwa na matatizo ya namna hii. Nilichotaka kujua si kufika tu, na kuanza kutoa mipira ya umwagaji maji na mbwembwe zao zisizo na impact katika kazi husika, ni sawa na bure na kutofika. Ndicho nilicho kua namaanisha.
Hivi wewe ynakuwa unacomment kabla ya kusoma habari yenyewe? Mbona ameeleza kuhusu zima moto na jitihada zao za kuuzima? Acha kukurupukaa
 

Wewe siku nyingi hupo Dar.

Unajuaje kwamba hakuna jengo refu lisilo na sprinkler system?
 
kama sikosei gari la zima moto lililokamilika gharama yake haipungui $ milioni moja kuendea juu.

Nasema tena lililotimia na jipya
Uko sahihi ss je kwa dar peke yake tunahitaji gari ngapi?na je hela inayokusanywa kpitia tra itatosha kufanikisha hili kwa sasa?jibu ni hapana tunahitaji tuwape muda hawa zimamoto wajipange vyema
 
Ndio maana wengi wanasema WaTanzania tuna akili ya masaburi samahani kwa kusema hivyo lakini ndivyo ilivyo,hapa Tanzania sekta ya ujenzi imekuwa kama kichwa cha mwenda wazimu,kwani tumekuwa tunajenga majengo makubwa na marefu bila kufikiria uwezo wa mambo mengine iwapo yatatokea kwa mfano maafa ya moto,utakuta panajengwa jengo la ghorofa 26 wakati vyombo vya zima moto ambavyo kwa mfano vinaweza kuzima moto kwenye ghorofa la 26 pindi ukitokea kama ulivyotokea PPF tower,hebu pia angalia ujenzi wa maghorofa Kariakoo sijui moto ukitokea kwenye hayo maghorofa kama hata zima moto wanaweza kufika hizo sehemu.Hebu pia tuangalia uimara wa misingi ya hayo maghorofa je kweli yanasitahili kubeba hizo ghorofa kweli,mengi ya maghorofa ya Kariakoo yana simamiwa na mafundi mchundo na hakuna anayejali,mpaka zikitokea ajali ndio hukimbilia kuunda tume ambazo hazina jipya lolote zaidi za kula posho.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…