Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Status
Not open for further replies.

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
ppf tower inawaka moto asubuhi hii
"Ni JENGO LA ppf" LILOKO MAKUTANO YA MTAA WA OHIO NA GARDEN AVENUE katikati ya jiji la Dar es Salaam, mtaa wa Garden avenue linawaka moto mkali.
Kwa sasa moto unatoke kwa juu ya paa ya jengo hilo.
Gari la zima moto na wafanyakazi wa zimamoto wanahagaika kutafuta mbinu na jinsi ya kuweza kufika juu ya jengo, lakini kufuatana na vifaa duni wanapata shida jinsi yakuweza kufika eneo lenye moto.

Vijana wazimamoto wamejitahidi kupunguza kasi ya moto, lakini bado kuna dalili za moshi mzito upande wa kusini mwa jengo.

Hatimaye moto umezimwa eneo lote la jengo. Kwa sasa hakuna dalili zozote za moshi juu ya jengo.

Taarifa zinasema kuwa,hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi wa jengo hilo walishuhudia moshi mzito ukitoka ndani ya jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi ghorofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo. Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo kuzima kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.


attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • IMG-20130203-WA002.jpg
    IMG-20130203-WA002.jpg
    16.3 KB · Views: 8,996
Ppf tower ya wapi? Mbona huweki mambo yaeleweke!
 
PPF tower inawaka moto asubuhi hii.
Jengo jipya liliko katikati ya jiji la Dar es Salaam, mtaa wa Garden avenue linawaka moto mkali.
Kwa sasa moto unatoke kwa juu ya paa ya jengo hilo.

ngoja nikaokoe pipi
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme
 
Nipo hapa posta mpya now. Magari ya zimamoto yanahangaika kutaka kuzima moto unaowaka ndani ya chimba kimoja ghorofa za juu hapa.
Jitihada zao zinaonekana ngumu kutokana na ugumu wa mabomba yao kufika katika chumba hicho
 
Tatizo nini au watu washatia moto nyaraka za siri kuficha ushhidi wa wizi wao kama ilivyofanyika mika ya 80 enzi zile za wizi wa beni na yule muheshimiwa naniliu......
 
Pokofame;

Duh! Acha hasira Mkubwa wetu! Haya majanga ya moto ni tishio sana!


Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme
 
Halafu jamaa wanafika wanashangaa shangaa,eti ngazi zao fupi kufika kule juu! Ngoja usambae...
 
wajinga utawasikia tu ati huo ni mpango wa FREEMASON hivi sasa hivi wanakalukuleti tarehe ya leo mwezi na mwaka na saa ilipoanza kuungua ili waje na data za kijinga na kihuni...kila kitu FREEMASON ,mtuache tupumue jaman kaah
 
lol hapo itabidi zima moto warudi kuchukua ngazi
 
Namsikia kupitia radio one mtangazaji wao Sam Mahela anaripoti na anasema chanzo hakijajulikana! Anasema chanzo kinaweza kuwa ni minara iliyoko juu na anazidi kubwabwaja ya kwamba hakuna mtu aliyepata madhara mpaka sasa!
 
na hiki kikosi chetu cha zimamoto kilivyo hopeless,hilo jengo sidhani kama litasurvive!?!
 
Namsikia kupitia radio one mtangazaji wao Sam Mahela anaripoti na anasema chanzo hakijajulikana! Anasema chanzo kinaweza kuwa ni minara iliyoko juu na anazidi kubwabwaja ya kwamba hakuna mtu aliyepata madhara mpaka sasa!

Kwa akili yake madhara ni kuumia tu!!! Kwani hicho kinachoungua kilinunuliwa kwa kutumia simbi, ebu kama hajui mambo aache kubwabwaja. Angesema madhara ya moto huu hayajulikani hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika. Watangazaji makanjanja ni janga la kitaifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom