Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Moto mkubwa umeibuka katika shule ya sekendari ya Iyunga ya jijini Mbeya na kuteketeza mabweni mawili na mali zote za wanafunzi zilizokuwa ndani ya mabweni hayo.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 3:00 asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa darasani, ambapo baadhi ya wanafunzi hao wanadai kuwa chanzo cha moto huo ni hitlafu ya umeme ambayo imetokea ndani ya mabweni hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa moto huo umeteketeza mali zao zote pamoja na vitanda vya kulalia, hivyo wakaiomba serikali kuona uwezekano wa kuwasaidia namna watakavyoishi shuleni hapo.
Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya, Charles Mwakalila amesema kuwa katika tukio hilo hakuna mwanafunzi ambaye amejeruhiwa wala kifo, na kwamba athari za moto huo zimeanza kufanyiwa kazi.
Chanzo: itv