voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,551
- 11,881
Nii wazi kabisa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba waziri wa fedha JMT.
Yuko katika wakati mgumu kuelekea kwenye mjadala wa uchambuzi wa hoja ya ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali.CAG huko bungeni Dodoma.
Mambo yameanza kumkalia shingoni,kabla hata ya ripoti yenyewe.
Ni pale ambapo mjadala wa uchambuzi wa hotuba ya waziri mkuu ulipokuwa ukiendelea.
Alianza kukiwasha Ester Matiko na ikampelekea Mwigulu kulazimika kusimama na kutoa taarifa kwa mchangiaji.
Mwigulu nae akajikoroga kwa kumhusisha Rais kuhusiana na ile kadhia ya ongezeko la malipo ya ndege ya mizigo!
Kabla ya Ole sendeka kusimama na kutaka muongozo wa spika,kwa kitendo cha Waziri wa fedha kumhusisha rais na uidhinishaji wa malipo ya kiserikali.
Video clips zinaongea hapo juu!