Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,377
- 8,075
Licha ya zaidi ya Sh100 milioni kukutwa zikiwa zimehifadhiwa ndani ya nyumba iliyopo Mtaa wa Lumumba jijini Mwanza, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kililazimika kutumia lita 39,000 za maji kufanikisha kazi hiyo iliyoanza saa 12:00 jioni hadi tatu usiku. Maduhu maarufu kama Mzee Shinyanga alikuwa akimiliki nyumba za kuishi, za biashara na hoteli jijini Mwanza.
Akizungumzia tukio hilo la Juni 10, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Andrew Mbate alisema magari matatu, moja la kikosi chake, lingine la kikosi cha Uwanja wa Ndege na la maji ya kuwasha la Polisi yalitumika kuzima moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana.
“Magari mawili kati ya hayo yalikuwa na uwezo wa kubeba lita 7,000 za maji na lingine lita 4,500 kwa wakati mmoja. Yote yaliisha na mengine kufuatwa,” alisema Mbate.
Alisema gari la lita 4,500 lilirudia kufuata maji mara nne, huku moja lenye uwezo wa kubeba lita 7,000 lilifuata mara mbili, hivyo kufanya idadi ya maji yote yaliyotumika kufikia lita 39,000. “Tulikuwa tukifanikiwa kuuzima upande mmoja, mwingine tulikotoka kunalipuka; tukihamia huko upande tuliomaliza kuuzima nao unaanza kuwaka upya. Tulifanya kazi ya ziada kufanikiwa,” alisema.
Kuhusu fedha, Mbate alisema walikuta ndoo kubwa nne zilizojaa noti za Sh10,000 zikiwa zimefungwa kwenye maburungutu na kwamba, watu aliodai ni ‘wazee’ na wafanyabiashara wenzake wa marehemu na watoto wake waliondoka nazo kwenda kuzihesabu.
Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa marehemu, Mboje Maduhu aliiambia gazeti hili jana kuwa kiwango kilichotangazwa msibani ni Sh230 milioni.
Katibu wa Uenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, Simon Mangeleka alisema kifo cha Mzee Shinyanga ni pigo kwa chama hicho kwa sababu alikuwa mmoja wa makada na mfadhili wa chama hicho.