Moto mkubwa wateketeza jengo refu la makazi London

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,178
2,000
Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London, watu walio shuhudia tukio hilo wanasema,moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.

Taarifa zinadai kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo linalo waka moto.

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza na karibu wazima 200 wanapambana nao.

Hadi sasa moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo vikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo.

Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo

Polisi wanamesema kuwa hadi sasa imebainika kuwa ni watu wawili tu ambao wameathirika na moshi wa moto huo na wanapata matibabu huku idadi ya waliokwama ndani ya jengo hilo ikiwa haijulikani. .

Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyepo katika eneo la tukio kwa sasa anasema jengo hilo lina wasiwasi wa kuanguka wakati wowote.
 

usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
11,958
2,000
Dhaaa!! Pole yao
Nairobi nako jana
Jengo lmeanguka
Na kuuwa watu 2
 

Ohooo

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
807
1,000
Dah nimelishudia jengo hilo likiwaka kupitia CNN na BBC dah ni hatari
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
10,382
2,000
Huwa nawaza tu ule mjengo pale katikati ya mji wenye gorofa 21 na mie ndio niko juu na moto kama huo unawaka,sijui nipite tu kwenye ngazi huku moto ukiwaka labda nitasalimika au niruke naweza nikapona....?
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,411
2,000
Moto ulianzia floor ya pili hadi 27.

95% ya wakazi wake ni non Westerners.

Hivi inawezekana moto uteketeze floor 25 kwenye jiji kama London bila kudhibitiwa?

Nahisi waingereza wameamua kuishi jino kwa Jino.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,107
2,000
Moto ulianzia floor ya pili hadi 27.

95% ya wakazi wake ni non Westerners.

Hivi inawezekana moto uteketeze floor 25 kwenye jiji kama London bila kudhibitiwa?

Nahisi waingereza wameamua kuishi jino kwa Jino.
Inawezekana Gesi itakuwa imehusika maana jengo kimeshika kasi chini ya dakika 40 ukawa umefika juu
Wakazi wa hilo jengo ni zaidi ya 600
Walio hospital ni 50
Waliokufa haijulikani
Walio ndani ya jengo hawajulikani
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,107
2,000
Hadi sasa ule msemo kuwa kile jengo la WTC lilibomolewa kwa makusudi unaingia akilini
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,411
2,000
Inawezekana Gesi itakuwa imehusika maana jengo kimeshika kasi chini ya dakika 40 ukawa umefika juu
Wakazi wa hilo jengo ni zaidi ya 600
Walio hospital ni 50
Waliokufa haijulikani
Walio ndani ya jengo hawajulikani
Kuna registration mkuu.Wanajua mtaa fulani una majengo mangapi, na kila jengo lina wakaaji wangapi na ni kina nani.

Ila kujua idadi ya waliokufa ndio itakuwa ngumu hadi uchunguzi utakapokamilika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom