Moto mkubwa katika kituo cha Bamaga

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Habari Wana JF,Kituo maarufu cha mafuta cha Bamaga kinawaka moto asubuhi hii kwa wale watumiaji wa Barabara ya Ally Hassan Mwinyi nawaomba wasipite maeneo hayo Foleni ni kubwa na kuna risk kubwa kwani kuna mitungi ya Gesi.
 
Duu zahama kubwa hiyo, Mungu wetu aupushe yasitokee madhara makubwa kwa viumbe wake!
 
ila watanzania kama kawaida yetu, wamejaa sana kushuhudia watakavyo lipuka na mitungi ya gesi
ni hatari kwakweli
 
Ndugu zangu JF, mnajua siku hizi message za simu zimeshakuwa chombo cha habari maarufu kuliko vingine. Nimepata message kwamba Bamaga Shell iliyopo D"Salaam karibu na Baraza la Mitihani inaungua moto sasa hivi. Siko karibu na tukio lakini tunaweza kushirikiana kiabari kama tulivyoshirikiana kwenye taarifa za ajali ya Dr. Harisson Mwakyembe. Natumaini habari zaidi.
 
Asante kwa taarifa mkuu, kwa zima moto na disaster management ya Tanzania kwa ujumla sidhani kama hiyo petrol station itasalimika... Au bima inatafutwa hapo?
 
ila watanzania kama kawaida yetu, wamejaa sana kushuhudia watakavyo lipuka na mitungi ya gesi
ni hatari kwakweli

Tukio km hilo lisilo la kawaida ni lazima kushudiwa ila ni muhimu kuchukua tahadhali. Wanafunzi wa ustawi vipi, take care moto usije kuwafikia na ukaleta madhara. Hope Fire brigade watakuwepo kudhibiti kwani location wise Bamaga panafikika kwa urahisi
 
Moto umeshadhibitiwa,japo vibaka na wananchi walifurika kwa wingi sana jambo ambalo ni la hatari sana.
 
ila watanzania kama kawaida yetu, wamejaa sana kushuhudia watakavyo lipuka na mitungi ya gesi
ni hatari kwakweli

Sasa hapo na wewe si unangoja kulipuliwa ama? Dah sijui ni uhujumu huo ama maana hicho kituo si ndio kimefunguliwa tena kwa kasi sana kikiwa na mabadiliko kadhaa na bei za kuwavuta walalahoi wengi kukimbilia huduma zake? Kazi ipo...
 
Jamani hakuna mtu aliyeweza kupata picha? Hata kwa kutumia simu? Aliye na picha aziposti jamvini ili na sisi tuelewe ukubwa wa tatizo kuliko kubaki na imagination.
 
Tukio km hilo lisilo la kawaida ni lazima kushudiwa ila ni muhimu kuchukua tahadhali. Wanafunzi wa ustawi vipi, take care moto usije kuwafikia na ukaleta madhara. Hope Fire brigade watakuwepo kudhibiti kwani location wise Bamaga panafikika kwa urahisi

kama kawaida yao, kwenda bila maji na huku wakiwa wamechelewa.
 
Sasa kilichoungua ni kipi sasa kile kipya au cha zamani hapa kwenye kona kabisa ya kuelekea Sinza? Duh masikini nimepiat asubuhi ya saa mbili palikuwa shwari!
 
kama kawaida yao, kwenda bila maji na huku wakiwa wamechelewa.

Hawa wanakera hivi kwa nini kila siku wanapata lawama kwa makosa yale yale? Mimi nafikiri sasa imefika wakati wa watu kutambua haki zetu ikiwapo hii ya kulindwa na hawa mafire brigade! Hivi haiwezekani kuwasue kwa makosa ya kuchelewa eneo la tukio au kuja bila kuwa na zama kamili kwa sababu za uzembe?
 
wajemeni.... mbona nasikia jamaa wala hakukatia kituo chake bima??
je hasara inakadiriwa ya kiasi gani??
uhai na usalama wa watu, wafanyakazi na wateja?/
vp kuhusu mali za wateja??
 
yah picha muhimu pia,jamaa wapinzani wake maweamua kumlostisha nini au ndo mambo ya insurance hayo?
 
Hii moto inayo zuka gafla binu vuu iwa kuna nyepesi nyepesi nyuma ya pazia yawezekana kuna madudu yanafichwa hapo nyie mtasema chanzo cha moto bado kinachunguzwa.
 
Tena pale wanauza mitungi ya gas....itakuwa balaa kama mbagala vile...yakishika moto ........twaomba uzima pale kwa wakazi wa jirani na wafanyakazi....
 
Tusiwalaumu sana FIRE, ENZI ZA MWALIMU walikuwa na sehemu zao za kujazia maji. Zote zimevamiwa hawana sehemu hizo tena.
Magari yao yanabeba maji kidogo wakifika tu na kuanza kuzima yanaisha (hivyo wanarudi kituoni kwao kilometa 20, ongeza na foleni hapo kuchukua maji) sisi tunafikiri hawakuwa nayo.
 
Moto sasa hivi tayari uko under control na hali ni shwari kabisa .Nimepita hapo 30 min ago
 
Back
Top Bottom