Moto kwenye jengo la wahamiaji Johannesburg

Teknocrat

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
3,816
8,470
Kumetokea moto katika jiji la Johannesburg kwenye jengo linalotumika na wakaazi na idadi kubwa ya wahamiaji, na kuua watu 74 ambapo kuna uwezekano wa ndugu zetu wa Tanzania.

Pia huwa wanajibanza haya majengo ni maarufu kwa wahamiaji kwa sababu, wengi huwa hawalipi kodi kuishi au kulipa kodi ndogo kwa matapeli waliojimilikisha haya majengo.

Watanzania wanaokaa Johannesburg watatujuza zaidi

1693498783549.png

1693498845507.png

1693498873642.png


---
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameungana na watu mbalimbali kuomboleza vifo vya zaidi ya watu 70, vilivyotokana na kuungua kwa jengo la ghorofa tano jijini Johannesburg, akisema kuwa ni janga kubwa.

Ikiwa ndiyo tamko lake la kwanza kulitoa hadharani kufuatia tukio hilo la moto, mtandao wa BBC umemnukuu Rais huyo akiwa katika ziara jimbo la Eastern Cape akisema: "Tunaungana na watu waliopoteza wapendwa wao katika na janga hili."

BBC imeeleza kuwa kati ya waliofariki, wamo watoto saba, miongoni mwao, yumo mtoto wa mwaka mmoja.

Ramaphosa ameendelea kusema: “Tukio hili linatutaka sote kuwaombea walionusurika ili wapate utulivu wa kimwili na kisaikolojia, nina matumaini kwamba uchunguzi kuhusu moto huo utawezesha jamii na mamlaka kuzuia kutokea tena kwa janga kama hilo.”
 
Back
Top Bottom