tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,240
- 4,466
Watu tuna roho mbaya sana. Hata kama umeibiwa why do you kill? Utakuta kati ya walioua wengi ni wezi serikalini, wengine wanaiba wake za watu n.k.Vijana watatu wa familia moja katika kijiji cha Manushi kati wilaya ya moshi vijijini wamechomwa moto hadi kufa na wanakijiji wenye hasira kali baada ya kuiba pikipiki kutoka machame.
Vijana hao wajulikanao kama ombeni kasamu, Anorld kasamu, na Marius kasamu wamechomwa moto nyumbani kwao manushi kati na wanakijiji kutoka machame baada ya kuiba piki pikipiki moja huko machame.
Wanakijiji kutoka machame waliwatafuta vijana hao na kwa kushirikiana na wenyeji wa kijiji hicho waliwatoa ndani ya nyumba na kuwachoma moto vijana wawili kati ya watatu ambao ni wa familia moja.,na baadae wenyeji wa kijiji wakamchukua na mdogo wao na. Kuanza kumkata kata mapanga hadi kufariki.
Tukio hilo limeleta furaha kijijini hapo baada ya wananchi kuchoshwa na ujambazi wa vijana hao hapo kijijini.
Tukio hilo limetokea jana kijijini hapo na polisi walipewa taarifa na kuja kuchukua miili ya marehemu hao na Kupelekwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti moshi mjini.
Hadi sasa haijajulikana miili hiyo itazikwa lini
Hakuna Mwanakijiji yoyote aliyekamtwa kutokana na tukio hilo.
Update
Mazishi ya vijana hao ni kesho jumamosi,
Habari zaidi nitazisogeza hapa
Tusiyachekelee mauaji kama haya, mtu yeyote naweza kuwa victim wakati wowote. Mauaji kama haya yamesababisha watu wasio na makosa/hatia wauawe.
Binamu ya wife aliuwawa mkoa fulani nyanda za juu alipokuwa akifanya kazi serikalini, huku akitoa mikopo midogo isiyo rasmi ili kuongeza kipato.
Siku moja alienda kwa wadeni waliokuwa wakimsumbua kijijini pembeni ya mji. Wakopwaji waliwaambia wanakijiji wenzao kuwa huyo mkopeshaji ndio mhalifu wa tukio la kupotea mtoto pale kijijini siku za karibuni, hivyo wakapiga yote kuitana na kisha kumwua. Haki hadi leo haijapatikana.
From nowhere mbaya wako anaweza kukufanya uuawe na kundi la watu.