Moshi: Vijana watatu wa familia moja wauliwa na wanakijiji kwa tuhuma ya wizi wa pikipiki

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,257
Vijana watatu wa familia moja katika kijiji cha Manushi kati wilaya ya moshi vijijini wamechomwa moto hadi kufa na wanakijiji wenye hasira kali baada ya kuiba pikipiki kutoka machame.

Vijana hao wajulikanao kama ombeni kasamu, Anorld kasamu, na Marius kasamu wamechomwa moto nyumbani kwao manushi kati na wanakijiji kutoka machame baada ya kuiba piki pikipiki moja huko machame.

Wanakijiji kutoka machame waliwatafuta vijana hao na kwa kushirikiana na wenyeji wa kijiji hicho waliwatoa ndani ya nyumba na kuwachoma moto vijana wawili kati ya watatu ambao ni wa familia moja.,na baadae wenyeji wa kijiji wakamchukua na mdogo wao na. Kuanza kumkata kata mapanga hadi kufariki.

Tukio hilo limeleta furaha kijijini hapo baada ya wananchi kuchoshwa na ujambazi wa vijana hao hapo kijijini.

Tukio hilo limetokea jana kijijini hapo na polisi walipewa taarifa na kuja kuchukua miili ya marehemu hao na Kupelekwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti moshi mjini.

Hadi sasa haijajulikana miili hiyo itazikwa lini

Hakuna Mwanakijiji yoyote aliyekamtwa kutokana na tukio hilo.

Update
Mazishi ya vijana hao ni kesho jumamosi,
Habari zaidi nitazisogeza hapa
 
Huko ni Nyumbani kwetu.

Actually, mob justice ya aina hii imedumu toka enzi.

Kuna mmoja aliwahi kukatwa sikio na plaiz (pliers) na kuamriwa alitafune.

Matukio kama haya yalinifunza mengi sana ikiwemo kuheshimu kitu cha mtu na kuacha udokozi.

Manushi Kati, Manushi Sinde, Manushi Mashariki na Manushi Ndoo ni vijiji katika Kata ya Kibosho Magharibi, Tarafa ya Kibosho, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Raia wa huko wana misimamo mikali sana.
 
dah pole sana kwa familia hiyo...unaweza kuonea huruma wezi lakini siku ukiingia kwenye anga zao nao wanakumaliza tu..

kuna mwaka zama fulani enzi za bilicans, majamaa matatu yalinitight na mapanga, dah nilikula bapa, enzi hizo nina simu kali tritel na siemens ya kidole nafukuzia demu Ifm...kama sio mrusi wangu ningeumia siku ile...ila waliteseka sana..
 
#MACHAME Si ndio huko liliko jimbo la HAI.

Nyumbani kwa mwenyekiti, watu wa Machame ni wenye Roho Mbaya Sana.
Lakini linaongozwa na mbunge wa CCM pamoja na serikali yake dhalimu. Huu ni udhalimu wa CCM ndio unawafundisha hao wananchi wawe wakatili Kama yule jiwe aliuekufa katili aliyemuweka Sabaya kwenye hilo jimbo afanye ule ukatili na kufundisha hao wananchi ukatili.
 
Back
Top Bottom