Moshi: Vigogo wa Jeshi la Polisi wakamatwa na magari 3 ya wizi Himo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Wakazi wa Mji mdogo wa Himo wilayani Moshi wameshangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani humo kutowachukulia hatua maofisa wake wawili wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa magari.

Maofisa hao wawili wanaotuhumiwa, mmoja anacheo cha Mrakibu wa Polisi (ASP) na mwingine Koplo walikamatwa na magari matatu ambayo waliyasafirisha hadi jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya Polisi zinaeleza kuwa maofisa hao walikamatwa na kikosi kazi maalum kutoka Dar es Salaam tangu mwezi uliopita lakini hadi leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa mwingine ambaye ni raia alikamatwa nyumbani kwa Koplo huyo akiwa na gari moja la wizi na vibao vya namba za magari 70.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa alipoulizwa na gazeti la Mwananchi alikiri maofisa hao kukamatwa na magari hayo akasema lakini mtu hawezi kupewa adhabu kabla ya kuthibitika kuwa kafanya uhalifu.

Chanzo: Swahili Times

=======

UPDATE


Mkuu wa jeshi la polisi nchi Ernest mangu amemshusha cheo mkuu wa kituo cha polisi Himo (ocs) mrakibu msaidizi wa polisi (ASP) zuhura suleman kwa kukamatwa na gari la wizi aina ya toyota rv4 lililoibiwa. Habari zaidi soma=>Kigogo wa jeshi la polisi ashushwa cheo na mwingine atumbuliwa kwa wizi wa magari

 
yaani nchi hii, mtukufu alisihasema mtu ushakamatwa na kidhibiti, uchunguzi wa nini, watafungwa sana wanaoiba penseli, lakini sio hao, hii nchi aisee, angekuwa mpinzani hapo, ingekuwa ni kosa la marehemu
 
Exhibit,mambo ya sheria hapo,unaweza shangaa pamoja na kukutwa na magari lakini bado wakaonekana hawana hatia.
 
Kwanza Hadi Hapo Hakuna Kesi Ninavyowajua Police
Kwa Kutupiana Taulo (Fair ) Itageuzwa Hiyo Mambo Haraka Sana Mtashangaa Mno.

Kuna Ile Kauli Ya Kubrash Viatu Ndiyo Inayotumika Ikumbukwe Hao Pongo Kwasasa Wamepewa Kiburi Sana Kiasi Cha Kujiona Wako Juu Ya Sheria.

Ambaye Haamini Aendelee Kungoja
Hadi Sasa Rpc Yupo Tu Halafu Umesikia Majibu Yake Yalivyo.
Wanaiba Kilimanjaro Wanauza Dar Haaa
Kweli Mbuzi Wa Bwana Seif Kala Mahindi Ya Seif Kwa Vyovyote Hakuna Kesi
 
Exhibit,mambo ya sheria hapo,unaweza shangaa pamoja na kukutwa na magari lakini bado wakaonekana hawana hatia.
Hapa ndio kwenye Tatizo.
Sasa sipatipicha lile Harrier la juzi sijui lilikuwa linataka kuingizwa Chimbo gani.

Aisee,inafikia hatua hujui nani wa kukusaidia
Madawa ya kulevya,Ujambazi,Wizi wa Magari,mhhhh haya,ndio maana hata Panya road nao wanaona watumie fursa
 
Back
Top Bottom