figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Vifo vya Watanzania 20 huko Moshi, ni uzembe wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni.
Huyu Hamduni ndiye katoa kibali cha kufanyika mkutano na akaahidi usalama wa wa watu na mali zao vitakuwa salama.
Muda wote Mwamposa alijua mambo yapo poa na Polisi wapo wa kutosha wa kuhakikisha watu wanatulizana.
Kwanini Salum hukupeleka Askari wa kutosha?
Kwanini hukuzuia mkutano kwasababu hukua na askari wa kutosha wa kulinda mkutano?
Kwanini taarifa za Kiintelejensia hujazifanyia kazi hadi tumepoteza wapendwa wetu?
Kwanini hamsemi ukweli kwamba watu wamekufa kwa kukanyagana badala yake mnasema Makanisa ya kiroho yanahubiri uongo? Mambo ya imani yanahusiana vipi na watu kukanyagana?
Kukanyagana inasababishwa na watu kuwa wengi. Hata mazishi yaQasem Soleimani huko Iran, watu 50 Walifariki na wengine 200 kujeruhiwa baada ya kukanyagana, je ilikuwa ni ilisababishwa na Walokole?
Hivi karibuni zaidi ya Mahujaji 717 baada ya kutokea makanyagano karibu na mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia. Je nao ni Walokole?
Kukanyagana haihusiani ni imani ya mtu bali ni wanausalama kutojipanga kusimamia utaratibu.
Huu ni Uzembe kazini, namuomba IGP Sirro akitumbue na kukushusha cheo.
Mikutano ya kisiasa umekua ukisema huna Askari wa kutosha unakataza mkutano, Sijui una taarifa za kiintelejensia unasitisha mikutano.
Uzembe wako ndo umeua watu. Nashangaa kuona bado upo Ofisini.
Unamtafuta Mwamposa ndo mwenye dhamana ya kulinda raia na Mali zao?
Hii kesi ni ya Polisi. Kwanini mlitoa kibali?
Au Polisi walimtega Baba Mwamposa ili kuchafua kanisa lake?
Haya Mambo ya kufa kwa kukanyagana nayasikia huko Maka sio Moshi.
Rais Magufuli kwa Mamlaka uliyopewa, Ikifika Jumanne huyu RPC wa Kilimanjaro hajachukuliwa hatua, Tumia Mamlaka uliyopewa na katiba kumuondoa Ofisini IGP Sirro na apangiwe kazi nyingine.
Polisi wanajua kusingizia sana. Tunaomba rais utusaidie ili kuwakumbusha iwajibikaji.
Rais Magufuli Sekta zote uwajibikaji upo isipokuwa Polisi tu.
Tunataka kujua kwanini Askari hawajapelekwa kulinda mkutano wakati wametoa kibari?
Mwamposa hana kosa. Mwamposa alitakiwa kulindwa yeye na Waumini wake.
Uzembe wa Polisi kulinda Mikutano ya Kiroho ndo sababu wanaamua kujilinda wenyewe.
Tunataka uwajibikaji