Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,606
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imempa mfanyabiashara anayemiliki klabu mashuhuri ya Meku’s Bistro Bar & Restaurant muda wa saa 24 kuifunga klabu hiyo kwa kukiuka sheria za nchi.
Klabu hiyo ambayo ni moja kati ya klabu mashuhuri mjini Moshi, inadaiwa kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kwa kupiga muziki kwa sauti kubwa na kuwa kero kwa majirani.
Barua ya halmashauri hiyo ya Machi 8, 2018 iliyotiwa saini na Danford Kamenya kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa, imesisitiza klabu hiyo kufungwa ndani ya saa 24 baada ya kupokea barua hiyo.
“Pamoja na ushauri wa mara kwa mara kuhusu kuzingatia masharti bado juhudi zetu zimekwama. Aidha imebainika biashara yako ya baa na mgahawa iko eneo hatarishi ambalo ni kituo cha mafuta.
“Kulingana na aina ya biashara unayoifanya kukusanya watu wengi na kuhitaji eneo kubwa zaidi unashauriwa kutafuta eneo linalofaa kwa shughuli hiyo.
“Unatahadharishwa kuwa kukaidi kutekeleza amri hii kunailazimisha ofisi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yako bila kukupa onyo lingine lolote pamoja na kukufikisha mahakamani,” imesema.
Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Michael Mwandezi alipoulizwa na MCL Digital leo, amekiri ofisi yake kutoa amri hiyo na kwamba hiyo ni baada ya njia zote za kidiplomasia kushindikana.
Mwandezi alisema halmashauri ilikuwa haina jinsi nyingine ya kufanya kwa kuwa mmiliki wake alishapewa onyo mara kadhaa na hata kutozwa faini, lakini hakutaka kujirekebisha.