Moshi: Kijana akutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Emmanuel Alex, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28, amekutwa amefariki dunia shambani huku mwili wake ukiwa hauna nguo yoyote.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Orori kata ya Machame Mashariki, limezua taharuki miongoni mwa watu katika eneo hilo huku chanzo cha kifo kikiwa bado hakijajulikana.

Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.
 
Moshi ndo mji pekee wenye majambazi sugu mahuligani na walevi wakutosha

Sitasahau siku majambazi yalinivaa mitaa ya PASUA yalikuwa manene marefu afu panga ndefu kama ulimi wa twiga.. Nilibak na nguo tu nilizovaa
Mkuu walikuvua nguo usiku halafu wakakuacha hivi hivi tuu au hahahhaa
Moshi majambazi ilikuwa zamani bhn, siku hizi wengi wao walishauawa na wachache waliobaki kustaafu.
 
Moshi ndo mji pekee wenye majambazi sugu mahuligani na walevi wakutosha

Sitasahau siku majambazi yalinivaa mitaa ya PASUA yalikuwa manene marefu afu panga ndefu kama ulimi wa twiga.. Nilibak na nguo tu nilizovaa
Nakumbuka kuna baa Moja ndogo tu hapo Msaranga ilivaamiwa na majambazi jioni, watu wawili walikula Risasi baada ya kubisha kutoa vitu, mzee mmoja alikufa hapo hapo! nakumbuka huyo mzee alikua ndo amestaafu karibuni alafu akaanza kumfundisha mke wake kuendesha Hilux yake kumbe ndio ilikuwa kwaheri Mwalimu...
 
Nilitaka kusikitika ila nimecheka kisenge kumbe alikuwa TICHA
 
Moshi ndo mji pekee wenye majambazi sugu mahuligani na walevi wakutosha

Sitasahau siku majambazi yalinivaa mitaa ya PASUA yalikuwa manene marefu afu panga ndefu kama ulimi wa twiga.. Nilibak na nguo tu nilizovaa
emoji1374.png
Ashukuriwe Mungu walikuachia nguo, pasua ya sasa imepoa, njoro ndo Stori nyingi
 
Back
Top Bottom