saidi kindole
JF-Expert Member
- Sep 21, 2012
- 311
- 796
Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali kufuatia kauli ya Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kufuatia kauli yake kuwa kuwa ili wabunge wanane wa majimbo ya Mkoa wa Kigoma waweze kushinda katika uchaguzi Mkuu ujao lazima wajiunge na chama hicho kipya.
"Zitto anapaswa kuwa na nidhamu na angeelekeza nguvu zake katika kujenga umoja wa wapinzani. Kwanza sijui anatoa kauli hii kwa kutumia msingi upi? Mwaka 2010 alipita jimboni kwangu kuwapigia debe wagombea wa CHADEMA lakini nilishinda," alisema Machali.
Machali aliendelea kusema "Nilipata ubunge siyo kwa sababu ya Zitto, walionipa ubunge ni wananchi. Zitto hana msaada wowote kwangu na asidhani kwamba yeye ni maarufu kuliko wabunge wengine, asitushushe."