Morogoro: Vijana 34 wakamatwa kwa tuhuma za wizi wa kukwapua mali za wananchi kwa kutumia pikipiki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia vijana 34 kwa tuhuma za wizi wa kukwapua mali za wananchi kwa kutumia pikipiki ambapo jumla ya pikipiki nane zinashikiliwa na jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu, amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika maeneo ya Mtawala, Kidabaga, Mwembesongo na Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, ambapo inadaiwa hutumia njia ya kupakizana vijana wawili kwenye pikipiki hizo na kuvizia watembea kwa miguu wanaoongea na simu au walioshika mikoba na kuikwapua.

Katika hatua nyingine SACP Musilimu, amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ikiwemo vipande vya nyaya za shaba mpya na zilizounguzwa huku nyingine zikiwa zimefumuliwa kwenye 'transfomer' zenye jumla ya uzito wa kilogramu77.9 zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Ahmed lililopo mtaa wa Modeco Manispaa ya Morogoro.

Muungwana
 
Hapa ndio ujue polisi ndio mwizi namba moja maana kwa nini wanakamata sasa hivi baada ya amri ya Rais wakati hii ni kazi yao ya kila siku?
 
Back
Top Bottom