Morogoro: Suzan Kiwanga na Peter Lijualikali, washinda kesi za Uchaguzi katika Majimbo yao

Inawezekana huyu jaji alipitia ile habari ya Moise Katumbi na ikamgusa!
 
Haya Bawacha rudini hapa mseme mahakama imetenda haki maana asubuhi mlitukana sana.
 
ndomana nimeaanisha hilo neno sasa nisingekuwa najua kusoma ningeliletaje hilo neno ndugu yangu,hapo sijaelewa hizo sababu za mtu kupewa ushindi,nieleweshe kama umeelewa
pamoja na uliyemnukuu kuandika kwa wino mwekundu "Mashahidi kujichanganya" wewe unasema "mshindi kujichanganya".umegeuza simu?
 
....yes nina hakika na nilichokiandika, kulingana na taarifa ya awali iliyoletwa hapa; kwamba wote wameshindwa!
Naona unaona aibu basi sema mahakama imetenda haki.. Teh teh
 
View attachment 372825
Leo ni hukumu kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Kilombero na Mlimba.

Kutokana na majimbo hayo kuwa na historia ya Vurugu zinazotokana na matukio ya kisisasa, jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi mkali katika viwanja ya ukumbi wa Halmashauri ya Kilombero inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo hilo na katika mahakama ya wilaya, inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo la Mlimba.

Kesi ya Kilombero na Mlimba zinasikiliziwa Sehemu moja.

View attachment 372830
Mbunge wa jimbo la Mlimba Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA)

View attachment 372892
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (CHADEMA)

UPDATES;

1. Mh. PETER AMBROS LIJUALIKALI ametangazwa kuwa Mbunge halali wa Ifakara mjini.

SABABU ZA USHINDI;
  • Mashahidi Kujichanganya.
  • Kutopeleka Malalamiko Kamati ya Maadili.
2. Mbunge wa jimbo la Mlimba kupitia CHADEMA Suzan Kiwanga, ameshinda kesi ya uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
Hiyo safi sanaaa............

Ukichanganya na ushindi wa kishindo wa uchaguzi wa viongozi wa vitongoji huko pande za huko huko Moro - Doma.............

Ukichanganya na zile 'mvua' 15 alizopata yule Askari aliyemuua Mwangosi kwenye hukumu ya majuzi kule Iringa.........

Ukichanganya kuweweseka kwa hali ya juu kwa makada wa CCM na Msajili wao wa vyama vya siasa kuhusu operesheni Ukuta inayotazamiwa kuanza Septemba mosi......

Hiyo tafsiri yake ni kuwa ni ushindi kwa Ukawa kwa kila pande za nchi............
 
Walipe faini zinazowastahili kutupotezea muda & resources !! Hongera Makamanda!!
 
Waliokuwa wanasema Polisi Morogoro wameshaona matokeo ya Kesi (Kwamba wagombea wa CCM wameshinda) na hivyo wanajiandaa kudhibiti wafuasi wa CHADEMA waliombe radhi jeshi la polisi.
 
Polisi labda hawakutaka makamanda wajazane kortini halafu wangeleta maandamano na mikutano ya ghafla.
 
Hahahahahaa abubakari Asenga abaki kuwa kipaza sauti tu
 
Back
Top Bottom