Morogoro: Suzan Kiwanga na Peter Lijualikali, washinda kesi za Uchaguzi katika Majimbo yao

Hiyo safi sanaaa............

Ukichanganya na ushindi wa kishindo wa uchaguzi wa viongozi wa vitongoji huko pande za huko huko Moro - Doma.............

Ukichanganya na zile 'mvua' 15 alizopata yule Askari aliyemuua Mwangosi kwenye hukumu ya majuzi kule Iringa.........

Ukichanganya kuweweseka kwa hali ya juu kwa makada wa CCM na Msajili wao wa vyama vya siasa kuhusu operesheni Ukuta inayotazamiwa kuanza Septemba mosi......

Hiyo tafsiri yake ni kuwa ni ushindi kwa Ukawa kwa kila pande za nchi............

Yule askari hatofungwa. Ni zuga tu. unaweza kukuta anaenda kuishi loliondo na kazi yake kama kawa.
 
Nitakua nasubira..
Hakii haipokwii Daima..
Kumbe mwajua haki haipokwi ukienda mahakamani. Kama ukweli ni huo, kususia vikao vya Bunge, kuziba midomo, mikutano na maandamano ya nini kama siyo uchochezi.

Viongozi wa CHADEMA waheshimu uamuzi wa Watanzania waliomchagua Dr Magufuli Rais wao nao watahesimika
 
Ondoa shaka,utajua muda si mrefu. Nunua kifurushi kingine ubaki humu JF. Utajua hatma ya Mbunge Suzan Kiwanga wa Mlimba. Watani zangu CHADEMA leo wana mechi ngumu. Moja tayari!

Mzee Tupatupa
Mkuu Mechi bado ni ngumu?
 
Mapolisi na mkuu wa Mkoa wasinge anza kutangaza maamuzi ya mahakama Ccm wangeshinda kesi.
Haya maamuzi ya mahakama yamekuwa hivi baada ya hukumu kuvuja.
Siku zote numbers do not lie.
 
UKUTA!!
Kama alibomoa nyumba,milima ya mawe na kuchimba barabara nchi nzima UKUTA Atashindwa!!!!
Watakao ushabikia Huo UKUTA watashikishwa Ukuta wao.
Naona umeingia ubaridi kwenye kidonda chako ulichokatwa mkia baada ya UKAWA kushinda kesi kinyume na ulivyoamini wewe?
 
Umebadili kauli ghafla.
Msiwe na tabia za kukurupuka kama ...
Hebu weka kauli yangu hapa ambayo nimeibadili kinyume na kusema haki imetendeka. Nyie ndio mlianza kulalamika hat kabla ya matokeo.
Hebu weka hapa hiyo kauli. Nyie mkishinda ndio mahakama imetenda haki na mkishindwa haijatenda haki.
 
View attachment 372825
Leo ni hukumu kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Kilombero na Mlimba.

Kutokana na majimbo hayo kuwa na historia ya Vurugu zinazotokana na matukio ya kisisasa, jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi mkali katika viwanja ya ukumbi wa Halmashauri ya Kilombero inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo hilo na katika mahakama ya wilaya, inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo la Mlimba.

Kesi ya Kilombero na Mlimba zinasikiliziwa Sehemu moja.

View attachment 372830
Mbunge wa jimbo la Mlimba Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA)

View attachment 372892
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (CHADEMA)

UPDATES;

1. Mh. PETER AMBROS LIJUALIKALI ametangazwa kuwa Mbunge halali wa Ifakara mjini.

SABABU ZA USHINDI;
  • Mashahidi Kujichanganya.
  • Kutopeleka Malalamiko Kamati ya Maadili.
2. Mbunge wa jimbo la Mlimba kupitia CHADEMA Suzan Kiwanga, ameshinda kesi ya uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
View attachment 372894
Mawakili waliosimamia Kesi za Suzan pamoja na Peter.

Katika Uchaguzi mkuu wa 2015 Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga alishinda kwa kupata kura 40,068 dhidi ya Mpinzani wake wa karibu Godwin Kunambi wa CCM aliyepata kura 34,883.

Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali wa CHADEMA alishinda kiti cha ubunge kwa kupata kura 62,158 wakati mpinzani wake wa karibu, Abubakar Assenga wa CCM alipata kura 44,092.
Tu-mwanasheria tu-vijana tumeyagaragaza masisiemu yote nyoooooo!! CCM wamekojoleshwa!!
 
CHADEMA bana ingetokea mmoja wao angevuliwa Ubunge wangeilaumu sana Mahakama
Wameshinda kesi zao basi hapo kwako ndiyo watasema Mahakama za Tanzania zipo huru

Kwa CHADEMA Mahakama za Tanzania zinakuwa HURU kama zita amua kesi ku wa favor wao tu
Ehehehe
 
Hapa Haki imetendeka. Ila jambo linalonikera kwenye mahakama ...eti mtu kishindwa kesi kisa kukosea 'teknikalities' za kimahakama wakati alikuwa na haki ya kishinda kesi.
 
mwenye taarifa sahihi jamani wengine tuko porini tunasafiri kwenda Dodoma kuwahi dead line ya kuhamia huko
sasa wewe unataka taarifa gani nyingine umeambiwa chadema wameshinda au mwenzangu wewe ni ccm kama mimi tunaotafuta pesa ya kulipa gharama za kesi.....tumeshindwa kesi tunajipanga next time
#ccm_mbele_kwa_mbele
#hapakazitu....
 
Back
Top Bottom