MOROGORO: Polisi inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za ubakaji na udhalilishaji wa mwanamke

Hivi kuna watu bado hawaamini kama sheria ya mitandao inafanya' majambazi wenyewe sikuhizi hawatumii cm wanakutana kimya kimya wanafanya yao wanaondoka alafu wanaokota kavocha kaliko tumika kanatupwa eneo la tukio police wakianza upelelezi wanaokota kale kavocha anakamatwa mtu alie katumia anaenda ozea jela wao wanapeta tu' tuwe makini jamani zama zimebadilika.
Hilo suala la vocha huwa linaniumiza kichwa kwamba jambazi ameenda kufanya tukio anafika pale anaongeza kwanza muda wa maongezi anaendelea kufanya uhalifu Tanzania ya maajabu.
 
Hilo suala la vocha huwa linaniumiza kichwa kwamba jambazi ameenda kufanya tukio anafika pale anaongeza kwanza muda wa maongezi anaendelea kufanya uhalifu Tanzania ya maajabu.
Kuna watu wengi sana wanatumikia adhabu zisizo zao.

Tunafanya mambo kienyeji sana.

Hii nchi nishapoteza hata morali ya kuiombea.

Acha tuishi tu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu kumi na mmoja kwa tuhuma za kumdhalilisha mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kwa kumtishia kwa kisu,kumbaka na kusambaza picha za kudhalilisha za tukio hilo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao 11, ni pamoja na mmoja Idd Adam (32) mkazi wa Makambako mkoani Iringa,aliyehusika kumtishia kwa kisu ili abakwe na kumrekodi video binti huyo,na mtuhumiwa Zuberi Thabit (30) mkazi wa mbarali mkoa ni Mbeya aliyembaka binti huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda Mateo amesema watuhumiwa wengine tisa wakiwemo wanaume saba na wanawake wawili,wakazi wa dakawa mkoani Morogoro wanashikiliwa kwa tuhuma za kusambaza kwenye mitandao ya kijamii picha za utupu za tukio hilo la ukatili na udhalilishaji dhidi ya mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mjamzito.

Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa hisia tofauti tukio hilo la ubakaji na udhalilishaji wakitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa,huku wengine wakishauri ndugu jamaa na marafiki kuwa karibu na binti huyo ili kumfariji na kumshauri awe mvumilivu katika wakati huu mgumu kwake .
Safi sana!!! Polisi bwana inafanya kazi ukiacha changamoto zilizopo pia. Bravo polisi!!!!! Hao wafungwe miaka 50 badala ya 30 kwa kubaka. Waliosambaza wafungwe kulingana na sheria. Ila wabaki jela plus viboko 100 kila mmoja. 5o wanapoingia 5o wanapotoka wakaonyeshe wake zao.
 
Nililuwa napinga shelia ya mtandao kwa hili Leo nimejikuta nashangilia sana
Mtu sio mkeo uchungu umeutoa wapi ?dada wa watu mpaka anaomba msamaa analalamika mnaniumiza jamanii! Bado tu hata huruma amna mkaona aitoshi mlivyotoka kumfanyia tendo la kinyama amjafikilia madhala mara2 mbili mkamdhalilisha mitandaoni nae kwa Hutu wake na heshima yake alikuwa analalamika na kujitetea msinipige Picha wala kutuma mtandaoni kuna kipindi ukiisikiliza clip unasikia anasema yukotayali kutii lolote lakini msinipige Picha wala msiitume mitandaoni bado wahovu walitupia mitandaoni na wengine wanawake wasio na haya wakaamua kusambaza Picha mwenyezimungu awalaanii duniani na akhera!

Inauma sana mkuuu ila Bora wameisambaza . Kwa sbb wahalifu wamepatikana
 
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho Aprili 28 mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku katika nyumba ya kulala wageni yenye jina la ‘Titii’ iliyopo Dakawa.

Kamanda Matei alisema kuwa binti huyo aliitwa kwenye nyumba hiyo ya wageni na Thabiti ambaye ni mkazi wa Mbarali wilaya ya Mbeya ambaye alikuwa na uhusiano naye kimapenzi. Baada ya kuingia chumbani alimkuta pia Adamu mkazi wa Makambako, Njombe ambao walimlazimisha kufanya mapenzi huku mmoja akimrekodi picha za video na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Wanaoshikiliwa kwa kosa la kusambaza picha za utupu ni Rajabu Salehe (26), Said Athman (26), Musi Ngai (36), Said Muhammed (24), John Peter (24), Hassan Ramadhan (27), Ramadhan Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjone (30).

Wote ni wakazi wa Dakawa, Morogoro na wamevunja Sheria ya Makosa ya Mitandao, kifungu namba 14, kifungu kidogo (1) (a)

Kamanda Matei alisema wakati wa tukio hilo watuhumiwa hao walimtisha binti huyo kwa kisu ili asipige kelele wakati akidhalilishwa na walimtaka asitoe siri hiyo vinginevyo watamuua.

Kamanda alisema wawili hao ni marafiki wa msichana huyo na kwamba Thabiti ambaye ni mpenzi wa sasa wa msichana huyo alipanga na Adamu ambaye ni mpenzi wake wa zamani kumkomesha.

Alisema Thabiti alimwambia mpenzi wake wakutane hotelini. Msichana alipofika aliwakuta chumbani huku Adamu akiwa ameshika kisu na kamera. “Wakamlazimisha afanye vile na kumtishia kumuua kama angekataa,”alisema Matei.

Hata hivyo, Betty alisimulia kisa hicho na kusema watuhumiwa hao walifanya unyama huo kwa sababu ya usaliti wa mapenzi. Alisema msichana alidaiwa kujihusisha kimapenzi na dereva wa mpenzi wake.

Kwa mujibu wa Betty, baada ya mpenzi wake kugundua alipanga njama ili kuwakomoa wote wawili. Alisema mpenzi wake alimwambia wakutane hotelini na alipofika alimkuta Zuberi pamoja na dereva wa mchumba wake hotelini.

“Akawambia wafanye kile kitendo huku akirekodi video,”alisema Betty. “Nia yake ilikuwa kuwakomoa…kwa nini atembee na dereva wake,”alisema Betty na kwamba baada ya hapo picha hizo zilianza kusambaa.
 
Watu wenye hayo majina ni makatili sana,wengine huwa wanajitoa muhanga,hii dini hii ni hatari
Jina sio dini,tumia akili,kuna Wenye majina ya dini lakini hawendi kanisani wala msikitini,wale waliouwa watu saba,ni wa majina ya dini fulani,lakini hatujasema dini yao ndio imewatuma hivyo.
 
Back
Top Bottom